Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

NAAMINI BADO REFINARY ITAJENGWA TANZANIA.

SABABU

1. UWEPO WA EACOP.
2. UPATIKANAJI RAISI WA ARTHI.
3.BANDARI YA TANGA.


IKIJENGWA MOMBASA.

CRUDE ITATOTOKA WAPI?
JE LITAJENGWA BOMBA JIPYA KUTOKA UGANDA?

NAAMNINI HAPA WANACHEZA MCHEZO ILI WAPATE MASHARTI NAFUU...
 
Wakenya wanapenyeza fitina.ila bado sisi tunayo karata . Hapa ndo pa kuchangamka sasa

Wakenya lazima watuzidi kwenye uchumi kwa sababu kwa Kenya, suala la uchumi ni kipaumbele chao namba moja, wakati sisi kipaumbele namba moja ni kuteka na kuua watu.

Hukusikia kwenye hotuba? Wa kwetu, kipaumbele namba moja alichokiona, na ambacho aliona ni muhimu kupata ushirikiano kutoka kwa Rais wa Kenya, ni ushirikiano katika kuteka na kuwapiga mikwaju wakosoaji. Lakini hotuba ya wenzetu wa Kenya, toka mwanzo mpaka mwisho, ilikuwa ni masuala ya uchumi.

Dangote ni mchumi mkubwa kivitendo, anajua ni wapi aweke kiwanda chake ili apate faida ya kiuchumi.

Kwetu akitokea mtu anataka kuwekeza katika kutengeneza systems za kuwapata na kuwateka wakosoaji wote wa watawala, bila shaka huyo mwekezaji atapewa ushirikiano wa kipekee.
 
Nafikiri kwa mtazamo wa mbali... Naiona nchi kama itaendelea na misimamo yake hii hii, tunaenda kuua diplomasia na ndio maana hata yeye mwenyewe kaona hilo na haoni umuhimu wa ku risk fedha zake hapo baadae
 

Fanya utafiti wa kina kuhusiana na biashara ya mafuta Duniani. Sehemu kubwa ya biashara ya mafuta ni crude oil, siyo refined oil. Dangote akiweka kiwanda chake Mombasa, mafuta yanaweza kuchukuliwa kutoka bandari ya Tanga, nchi za Kiarabu, hata Russia. Kama mafuta yatatoka Tanga, kwenda ufaransa, yanaenda kuchakatwa, halafu yanauzwa Duniani kote, nini kitazuia yasifike Mombasa halafu yakauzwa Afrika Mashariki yote? Hiyo Uganda yenyewe itaenda kununua mafuta Mombasa. Kuyachukua mafuta kwa meli toka Tanga mpaka Mombasa, ni jambo rahisi sana.
 
Watanzania bhana watu kwenye pitching iliyofanyika Kenya ya viongozi WA WA east Africa hamkuepo (kosa) raisi wa Kenya kuja tz kuongea na raisi wenu Hadi bunge (ujinga na upuuzi mwingi ulionekana Kwa viongozi wetu ) hata Sisi wananchi tuliona japokuwa hatukuona mengi kama ruto (very smart man ) .....moja ya vita za kiuchumi magu alikuwa anazungumzia ni hizi occasionally nilishawai ona dangote anaelekea Kwa raisi kipindi cha magu at the time anapitia changamoto ila haikua first wala second SASA Kwa viongozi wetu wako slow Sana kuproces na kufanya maamuzi tena yaa maana ...refenery maana yake nikuendesha uchumi sababu vitu vingi au uchumi mzima unatokana na bidhaa za crude ,.....ila sababu ya
 
Nafikiri kwa mtazamo wa mbali... Naiona nchi kama itaendelea na misimamo yake hii hii, tunaenda kuua diplomasia na ndio maana hata yeye mwenyewe kaona hilo na haoni umuhimu wa ku risk fedha zake hapo baadae

Katika uwekezaji, kati ya vigezo muhimu, kimojawapo ni uthabiti wa Serikali, na huo uthabiti kimojawapo kinachoangaliwa ni jinsi Serikali inavyozingatia haki na usawa. Wataalamu wa masuala ya utawala wanadai kuwa utawala wowote usiotenda haki, unasababisha kila kitu, pamoja na uwekezaji, kuwa kwenye risk. Kwa sababu asili ya mwanadamu ni kuchukia na kupinga dhuluma. Mahali penye dhuluma, hapana usalama wa kudumu katika uwekezaji kwa sababu siku zote watawala huwa karibu na wawekezaji, hivyo wanaodhulumiwa wanapopambana na watawala, wawekezaji kwa kiasi kikubwa huwekwa upande wa watawala, hivyo uwekezaji unakuwa kwenye hatari ya kushambuliwa.

Kwa upande wa Afrika Mashariki, kwa sasa, ni Kenya pekee ndiyo inayoonekana kuwa na utawala ambao kwa kiasi kikubwa unazingatia haki na usawa. Tanzania kwa sasa, linapokuja suala la ulinzi wa haki, usawa na uhuru wa watu binafsi, inashikilia nafasi ya mwisho. Ni ngumu sana wawekezaji wakubwa walio makini kuja kuwekeza Tanzania, tutawapata wababaishaji na wale wajanjawajanja toka China na Uarabuni tu.
 
Kingine naona Dangote hajatarget hiyo EACOP yenu, naona ataexport crude kutoka Nigeria na middle East
Dangote anataka kujenga refinery itakayo chakata aina zote za crude oil kumbuka crude oil ya uganda ni medium light crude oil, kwa hiyo itabidi Aimport heavy crude oil na extra heavy crude oil ambazo hazipo East afrika
 
Hii deal Ruto ndio mtu Kati, Na kinachofanyika hapa ni sitaki na nataka, Dangote anapima Kina Cha Maji,

Yeye ajenge hio refinery hapo Mombasa Lakini at the end of the day hio pipe ya EACOP ukiwa completed tutaleta Investor mwingine

Hio Protection ya kisera anayoitaka sisi kama TZ haitatuhusu yeye aendelee na sisi tutajua pa Kupitia

Watu tuna judge Kwa vile Hatuna information sahihi ila alichofanya au ku adress Madam President ni Sahihi kabisa
 
Hakuna kitakachobadilika. Mengineyo ni majungu tu
 
Urasimu, rushwa na undumilakuwili aliokutana nao kwenye uanzishaji na uendeshaji wa Dangote Cement - Mtwara, nao umechangia kuchagiza mradi kwenda Kenya.

Naomba kufahamu kama Tanzania tunaye mtu "aggressive" sana kwenye negotiation na kupata miradi mikubwa kama James Rugemalira!!??
 
Unachoandika hivi Ni kama vile wewe na hao viongozi wako akili zenu zimetimia.

Wewe na hao viongozi wako hamna akili hata kidogo, hamuwezi kufanya jambo lolote la maana. Investors wite miaka yote wanawapiga kwa kila namna wanayopenda

Nakukumbusha tu uone mlivyo hamna akili.mwaka Jana mliwalipa IPTL bilion 380. Iptl ambao walipaswa kuwalipa nyie, nyie ndio mliwalipa
 
Hiyo diplomasia ya uchumi Tanzania Imewahi kutumika wapi? Naomba unipe mifano
 
"ulinzi wa soko lake dhidi ya uingizwaji holela wa nishati ya bei rahisi (dumping) kutoka mataifa kama Urusi na India".

Hili sharti la kipumbavu sana. Dangote anapenda apate yeye tu hataki ushindani. Monopoly ndo sera yake. Hata huko Nigeria anasumbuana sana na serikali. Pia kusema anataka usaidizi wa kifedha ni sharti la kishenzi. Atafutwe mwekezaji mwingine asiye na masharti ya kijinga.
 
Kwani kama tuna lengo la kujenga hiyo refinery plant hakuna mwekezaji mwingine zaidi ya Dangote?...

Kwani mpango wa kujenga hiyo Plant ushirikishwaji wake ulikuaje baina yetu Sisi na wao?.

Mbona kama inaonekana Kenya,Dangote walikaa wao peke Yao na kuamua plant ijengwe kwetu, Sisi nafasi yetu ilikuwa iko wapi kwenye majadilino hayo ya awali?, Ruto yeye alisimama kama Nani kusema kiwanda kijengwe Tanga (Tanzania)?, Mbona kama Ruto tayari alikuwa na Options mezani kwake ilihali Sisi imekuwa kama Suprise?

Kuna maswali mengi Sana ya kujiuliza, lakini Naamini kama kweli serikali ina Nia nzuri ya kufaidisha wananchi basi hii sintofahamu sio ngumu kuamua, maana still bado tuna karata zetu nzuri Tu za kucheza na kufaidika.
 
EACOP inapitisha mafuta ya Uganda, sio ya Tanzania. Uganda TotalEnergies na CNOOC ambao ndio wenye mafuta watauza mafuta yao kwa wateja wowote watakaowapa bei nzuri. Tanzania haina maamuzi yoyote na hayo mafuta.
 
Tatizo ni CCM tu hakuna kingine!
 
Nafikiri waendelee kushupaza shingo na kuhisi kila anaye ishauri Serikali ni kuwa anaihujumu....
 
Gullible East Africans kupenda kujadili mambo kiwepesi. All there is at best kwenye hii refinery saga is politics. Ruto inaonekana anatafuta political mileage Kenya; na mafuta labda ni sensitive issue kwa sasa ndio msingi wa hii suddenly refinery project.

Sidhani kama project kama hiyo inatoka kuwa concept week mbili nyuma na kuwa investment decisions leo (it takes a lot of planning). Wakati hii refinery ya EAC hata huyo mwenyeji (Tanzania) hakuwa na habari ingeenda jengwa Tanga na yeye kaona tu kama wengine mitandaoni.

On the initial discussion day lilipoibuka swala la refinery; moja ya concern za Dangote ilikuwa source of stock feed; nchi zinazotajwa DRC, South Sudan na Uganda. DRC hata thoroughly exploration aijafanyika bado let kuanza kuuza crude, South Sudan uwezo wao wa kump mafuta kwa siku ni chini 80,000 kwa siku. Uganda uwezo wake ni 225000 barrels.

Sasa muulize huyo Dangote mwenyewe huko kwao kama anapata stock feed yote kutoka Nigeria? Jibu hapana kwao wana pump almost 1.4 million barrel kwa siku na wamiliki wa vitalu kwa umoja wao can only give him 250,000 crude per day. Wachimbaji wana masoko yao ya kupeleka crude pia nje ya Nigeria. Matokeo yake Dangote almost 60% ya stock feed ya refinery yake anaagiza nje ya nchi.

He is not stupid (Dangote) keshajifunza changamoto za kupata inventory ya mafuta. Kweli we unaamini Total hawana soko lao na mafuta ya Uganda, South Sudan hawana soko lao (achilia mbali political instability), DRC hakuna hata investments za kutoa mafuta from ground nor clear understanding of the reserves amount. Bado East Congo kwenye mafuta kuna political instability halafu mtu anakwambia anajenga refinery inventory itatoka huko.

Ni hivi seriousness ya EAC refinery haiwezi fanyika jukwaani kirahisi vile; Ruto anauchaguzi karibu Kenya ndio msingi wa hizi hadithi za refinery it’s all politics.
 
Reactions: Nus
Ni mapema mno kusema lolote juu ya ujenzi wa refinery
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…