Daniel Chongolo wa CCM: Watu Wanataka Katiba Mpya Kwa Maslahi Binafsi

Na CCM inang'ang'ania katiba iliyopo kwa maslahi ya Chama.
 
Maridhiano hayana maana yeyote kwa upuuzi huu wa kina chongolo, hii KATIBA AMBAYO ITASIMAMIWA NA CCM HII YAKINA NCHEMBA, ITAKUWA BORA YA ILE YA 1977, HAPA BORA JINO KWA JINO MPAKA KATIBA YA HAKI IPATIKANE.
 
Mimi pia naunga mkono hoja, ningependa katiba mpya ingeundwa na viongozi wa dini, wakimila na asasi za kiraia, vyama vya siasa visihusike kabisa.
 
Wajinga ni wengi sana nchi hii, hiyo katiba ya 1977 iliandikwa kwasababu gani? Wakati kabla ya 1977 nchi ilikuwa ikiendeshwa. Wajinga wa sasa wangekwepo kabla ya uhuru sijui kama uhuru ungepatikana make hoja zao zingetupiliwa mbali sana na watawala wa kikoloni.
Punguzeni ujinga wanaCCM
 
Kweli wew ni zuzu kweli kwerii
Huo ujinga unao uonesha ni afdhari ungekaa kimya. Wew sio wa kwanza kusimamia uchaguzi kuna watu tumesimamia uchaguzi tena hata wapinzani hawakuwa na mawakala badala yake msimamizi wa uchaguzi ndio unahesabu kura zao na kuziandika.

Niliwahi simamia uchaguzi ktk kituo changu Chadema hawakuwa na mawakala lakini waliongoza ktk kituo changu na mawakala wa vyama vingine wakasaini kuwa ni kura halali.
Kilichotokea 2020 hakukuwa na uchaguzi kama hujui kaa kimyaaa.
Kwa tume hii iliyopo sasa siwezi poteza muda kusimama kwenda kupiga kura.
 
Kama mtu kama jpm akiridi ten kwa katiba hii si atanyonga raia wote. Tunataka katiba mpya ili rais mwenye kaliba ya jpm asijipenyeze mana nchi ilikuwa hoi bin taaban chini yake
 
Kama mtu kama jpm akiridi ten kwa katiba hii si atanyonga raia wote. Tunataka katiba mpya ili rais mwenye kaliba ya jpm asijipenyeze mana nchi ilikuwa hoi bin taaban chini yake
Katiba mpya ni muhimu sikatai ila sio kwa viongozi wa serikali hii, uwezo wa kuleta katiba mpya imara hawawezi hamna kiongozi serious hata mmoja achilia mbali kiongozi mwenye sifa ya kuwa intelectual labda kama wakina Mtikila au Mvungi wangekuwepo
 
Kwa akili zenu finyu mlitaka vyama vya siasa visubiri Asasi hizo ndiyo zitangulie ?!.

Kama hawana utashi ndiyo basi tena.
Kila upande upiganie yale mapungufu yaliopo wanayoyaona yaondolewe.
 
Hayo aliyoyasema Chongolo kama agenda muhimu ndizo wanazotumia CCM kufubaza uwezo wa wananchi kufikiri.

Chongolo atuelezee kuanzia uhuru hadi leo suala la pembejeo lipoje? CCM imetekelezaje?
Huyu Chongolo yeye hataki katiba mpya kwa maslahi binafsi yake pia.
Siku hizi hajui hata anaongea nini.
 
Ngombe
 
Hata yeye Chongolo na chawa wenzake katiba iliyopo inawanufaisha sana ndio maana hawataki katiba mpya.
 
Chama kisicho taka katiba kinaipenda ya Sasa maana ya Sasa inawapa uhakika wa kuiba uchaguzi
 
Ndio maana huu mchakato unatakiwa uondolewe mikononi mwa wanasiasa, hawa watalilainisha hili jambo, waligeuze la kisiasa, waanze kurushiana maneno na vijembe, siku ziende, matokeo yake tuendelee kubaki hapa tulipo.

Inawezekana kabisa hawa CCM wameshazoea Chadema ndio wako mbele kwenye madai ya Katiba Mpya, sasa wanachofanya wameshaanza kuwatafutia majibu mepesi ya madai yao, watanzania lazima tupate suluhisho na njia mbadala ya kuwezesha kuipata Katiba Mpya tuitakayo kwa vitendo.
 
Nakubaliana na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…