Yuko sahihi sana japo mnamshambulia na kumkejeli maana hela ile ya boom kwa matumizi ni ndogo sana ila ukijibana ukaitunza nusu kwa semister 2(2×2) halafu ukawekeza pazuri na kujumlisha hela TP 600,000/=kwa tuliosoma Bead ni hela kubwa na kwa wale tuliotoka familia maskini na tuliokuwa tunauchukia umaskini ilituokoa.
Mimi nilipewa mkopo 78% kati ya ada 1,000,000/= nilikuwa nalipa 220,000/= na kwa muda ule {2013-2015} tulikuwa tunapata 450,000×2 kwa semister na ukiongeza semister ya pili 450,000×2 ina maana kwa mwaka wa masomo ni 1,800,000/= hapo tunapewa stationary 200,000/= na TP 600,000/=ambapo tulikuwa tunatafuta shule zinazotoa accomodations
Kwa mwaka mmoja wa masomo nilikuwa nanunua ng`ombe 6 wenye thamani ya 150,000/= kila mmoja na mpaka naingia 2015-2016 ambapo boom lilipanda na kufikia 520,000x4 kwa mwaka wa masomo (2,080,000) tayari nilikuwa na ng'ombe 12 na mwaka wa mwisho nilipamba kutunza hela keshi ambapo nilipata 1,100,000/= ambayo nilipanga nianzie mtaji punde nitakapoingia mtaani
na nipiweza kufanikisha hilo
NILIWEZAJE KUFANYA HIVYO NIKIWA CHUO?
Kwenye miaka yangu yote mitatu niliyokaa chuoni (Udsm) niliishi mabibo hostel ambapo tulikuwa tunashea chumba na wenzangu ambapo gharama ni nafuu lakini pia nilikuwa napiga shuttle pori daily labda itokee dharura ya mvua na kuhusu chakula bajeti yangu ilikuwa ina range 1,800-2,000 ambapo bajeti ya chai niliitoa kabisa maana kwetu sikuwahi kuiona na nilizoea kula mchana tu,hivyo mchana nilikuwa nakula RB mwanzo ilikuwa 600 baadaye ikapanda ikawa 800 na jioni nilikuwa nakula ugali mboga mboga au dagaa ilikuwa 1,000 mtaani (mama kifusi waliokaa mabibo hostel wanamjua).Kwa mfumo kiukweli niliweza kuishi japo ni maisha ya shida chuoni ila huwa nakaa najipiga kifua na kujisemea isingelikuwa CHUO nisingelikuwa naishi maisha haya ya leo.
NILIFANYA NINI BAADA YA CHUO?
Niliingia mtaani bahati nzuri nikaajiriwa kampuni binafsi sep 2016 nikafanya kwa muda wa miezi 6 nikapata uzoefu na nikaona ile kazi naweza kuifanya mwenyewe japo kwa mtaji niliokuwa nao, nilikuwa nilikuwa nalipwa 300,000/= kwa miezi hio linikusanya 700,000/= nikauza wale ng'ombe wangu 10 ambapo nilipata 4,800,000 na nikajumlisha ile akiba ya mwaka wa mwisho japo nilikuwa nimeitumia imebaki 800,000/= ukawa mtaji wangu nikaanza rasmi biashara yangu mwenyewe May 2017.
Kiukweli kwa sasa najiendesha vizuri na sijawahi kupata wazo la kuomba ajira serikalini na kile nachopata kimenipa heshima katika jamii na hata nyumbani kwetu nilishabadilisha maisha ya wazazi kutoka nyumba za nyasi kwenda nyumb za kisasa na siku zote naamini maono ya mtu ndo humfanya aone kidogo kwako ni kikubwa kwake na akakifanya hata kikawa kikubwa machoni pako.
TUSIDHARAU BOOM ILA TUJITHATHMINI MATUMIZI YETU TUWAPO CHUONI