Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu
Tanzania ni special case
Hatuna
  1. Raisi
  2. Mahakama
  3. Bunge
Tuna jeshi pekee ambalo linafanya lolote kwa yeyote bila huruma wala kufuata shetia
 
So sad! Serikali iangalie kwa jicho la kipekee hili swala la watu kukamatwa au kuchukuliwa kwa utaratibu wa kiuni maana watu wasio na nia nzuri wataweza kupitia huo upande wa kujiita polisi na kufanya mambo ambayo Baade hayataweza kutovumilikaa katika jamii.
 
Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu
Fisiem kwa sasa wanacho weza kufanya Ni utekaji wa wapinzani, wizi wa uchaguzi na kuuza raslimali za nchi basi!
 
1. Milishindwa kupiga picha wahusika?
2. Mlishindwa kupiga picha gari lao?
3. Hakuna alie weza hata kuchukua video ya tukio?
4. Walikua na silaha za moto?
5. Walikua wangapi?
6. Mlishindwa kuwahoji?
7. Mlishimdwa kuwazuwia wasimchukue?

Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu
MLISHINDWA KUBLICK NJIA?

MLISHINDWA KUTOBOA MATAIRI KWA MISUMARI?

MLISHINDWA KUTIA PANCHA MATAIRI???.

UZOMBI WENU TENA MUENDELEE KUTEKWA
 
So sad! Serikali iangalie kwa jicho la kipekee hili swala la watu kukamatwa au kuchukuliwa kwa utaratibu wa kiuni maana watu wasio na nia nzuri wataweza kupitia huo upande wa kujiita polisi na kufanya mambo ambayo Baade hayataweza kutovumilikaa katika jamii.
Point kubwa sana hii
 
Kwenye hii nchi ni watu au taasisi gani zinaruhusiwa kumiliki pingu? Maana taarifa kila ya aliyetekwa inasemekana watekaji walikuja na pingu na silaha 🔫
 
Namshukuru Mungu jana jioni nilikomesha jaribio la utekaji maeneo fulani jamaa walikuwa na pingu ila wamevaa kiraia wanakomaa na mchizi wampakie kwenye ndinga nikaingilia kati kujua sababu. Ilikuwa ni varangati hawakuamini. Njemba nyingine zinajipitia tu hazijali wala nini wanaona mchizi anapiga makelele anakomaa na jamaa zaidi ya watatu wamuingize kwenye Noah. Mwisho tuliwazidi wakasepa zao.

Aisee hawa jamaa nilikuwa sijawahi kuona live. Wanakuja sehemu ulipo wanakuchukua mzobe mzobe hata hawaogopi raia. Raia nao hawana habari yoyote. Tubadilike siku hizi hawaji hata na uniform wala hawahitaji maelezo. Wanakuburuza wakikuzidi wanakutupa kwenye gari kama mzoga haoooo.. Jana tuliwashinda na mapingu yao yakabaki mkononi mwa jamaa maana walifanikiwa kufunga mkono mmoja.
 
Na Mkashindwa kuwazuia hapo kituoni mpo wengi

Wanaume wa Dar ovyo kweli
Ujue nilikua Taifa siku chache nyuma, sasa tulikuwa kwenye folen ya kuingia uwanjani. Askari wakawa wanaruhusu watu kwa mafungu.

Sisi fungu letu lilisimamishwa kitambo kidogo, basi kwenye ule msongamano kuna wana wawili kutokea nyuma wakawa wanauliza kwa ghadhabu, "Oya kuna nini huko mbele?". Na askari anawaona vizuri tu wameshikilia foleni.

Ikabidi mwana mmoja awaulize, "Tuwaachie njia muje kuwauliza? Inaonekana wenzetu mna haraka sana.", jamaa wakapunguza sauti halafu baadae kimya.

Nikajifunza kitu kimoja, Mbongo ni muoga asikuzuge ana hasira.
 
Namshukuru Mungu jana jioni nilikomesha jaribio la utekaji maeneo fulani jamaa walikuwa na pingu ila wamevaa kiraia wanakomaa na mchizi wampakie kwenye ndinga nikaingilia kati kujua sababu. Ilikuwa ni varangati hawakuamini. Njemba nyingine zinajipitia tu hazijali wala nini wanaona mchizi anapiga makelele anakomaa na jamaa zaidi ya watatu wamuingize kwenye Noah. Mwisho tuliwazidi wakasepa zao.

Aisee hawa jamaa nilikuwa sijawahi kuona live. Wanakuja sehemu ulipo wanakuchukua mzobe mzobe hata hawaogopi raia. Raia nao hawana habari yoyote. Tubadilike siku hizi hawaji hata na uniform wala hawahitaji maelezo. Wanakuburuza wakikuzidi wanakutupa kwenye gari kama mzoga haoooo.. Jana tuliwashinda na mapingu yao yakabaki mkononi mwa jamaa maana walifanikiwa kufunga mkono mmoja.
Kwa hili utabarikiwa. Sema kiukweli Watanzania tunaishi kama Manyumbu.
 
Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu

====

UPDATE

JamiiForums imewasiliana na Shangwe wa ACT ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza Nondo alikuwa ametokea Kigoma baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kumalizika, ambapo wakati anashuka kwenye basi Stendi ya Magufuli watu wasiyojulikana watatu walimfuata kukawa na purukushani Nondo akijitahidi kujinasua lakini walifanikiwa kumchukua na kuangusha pingu walizokuwa wameenda nazo pamoja na begi alilokuwanalo Nondo

Matukio mengine ya utekaji kuwahi kufanyika nchini haya hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Shangwe ameeleza pia gari lililomteka Nondo ni Land Cruiser nyeupe yenye namba za usajili T 249 EMV. Taarifa za awali walizitoa kwa mashuhuda ambao walikuwa wanamfagamu Nondo, baada ya kufungua begi lake kulikuwa na note book ambayo nayo ilithibisha kumilikiwa na Abdul Nondo

Pia shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema gari hilo lililokuja kumteka Abdul Nondo lilikuwa na watu 4, wawili wakiwa na bunduki na wawili wakiwa mikono mitupu, watu walipoenda kuangalia kuna nini na kujaribu kuhoji waliwanyooshea bastola na hivyo watu kubaki wanaangalia tukio hilo likitokea na Abdul Nondo akawa ametekwa! Katika purukushani hizo kwa maelezo ya shuhuda mbali na pingu na bengi la Nondo, ilianguka pia inadaiwa simu ya moja ya watekaji ambavyo vyote vimechukuliwa na Polisi.
Hii namba ya gari alilotekwa Nondo bado hatuzafikia, inaama ni Special Number, hapa inaonesha 100% kazi imefanywa na kitengo
 
Back
Top Bottom