Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
#HABARI Chama cha ACT Wazalendo kimethibitisha kuwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho Adbul Nondo ametekwa na watu ambao bado hawajajulikana katika Kituo cha mabasi cha Magufuli alipokuwa akitokea Mkoani Kigoma kwenye kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa asubuhi ya leo Disemba 1, 2024.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Chama hicho zilizothibitishwa na Naibu Katibu wa Haki za Binadabu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi ACT Wazalendo Mbarala Maharagande, zimeeleza kuwa baada ya viongozi wa chama chicho kupewa taarifa na wasamalia wema walifika katika eneo hilo, na kutambua vitu vilivyobaki baada ya purukushani iliyotokea ni vya Abdul Nondo.

ACT wamesema kuwa bado wanaendelea kufuatilia tukio hilo na wanatarajia kutoa taarifa rasmi na kwa sasa viongozi wa chama hicho wapo katika kituo cha Polisi cha stendi ya Magufuli.

EATV inaendela na juhudu za kulitafuta Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam kuthibitisha taarifa hizi.

#EastAfricaTV
 
 
Kwa maelezo ya mtu aliyeshuhudia tendo Hilo lilifanyika Kwa haraka na aliposogea kuhoji ndipo walipoondoka eneo Hilo na kuiacha pingu iliyokabidhiwa kituo Cha Polisi Magufuli.Aidha gari la watekaji limetambuliwa Kwa namba zake na walioshuhudia ni Landcruise Nyeupe Kwa sasa utaratibu wa kumjua mmiliki unafanyika
 

Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu
Wakiambiwa waungane kutokomeza haya mambo wanadai maandamano ni ya chadema tuu, haya mmoja mmoja mpaka tuishe 😁😁
 
Back
Top Bottom