Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
#HABARI Chama cha ACT Wazalendo kimethibitisha kuwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho Adbul Nondo ametekwa na watu ambao bado hawajajulikana katika Kituo cha mabasi cha Magufuli alipokuwa akitokea Mkoani Kigoma kwenye kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa asubuhi ya leo Disemba 1, 2024.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Chama hicho zilizothibitishwa na Naibu Katibu wa Haki za Binadabu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi ACT Wazalendo Mbarala Maharagande, zimeeleza kuwa baada ya viongozi wa chama chicho kupewa taarifa na wasamalia wema walifika katika eneo hilo, na kutambua vitu vilivyobaki baada ya purukushani iliyotokea ni vya Abdul Nondo.
ACT wamesema kuwa bado wanaendelea kufuatilia tukio hilo na wanatarajia kutoa taarifa rasmi na kwa sasa viongozi wa chama hicho wapo katika kituo cha Polisi cha stendi ya Magufuli.
EATV inaendela na juhudu za kulitafuta Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam kuthibitisha taarifa hizi.
#EastAfricaTV