Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Karakana!?Nondo yuko Karakana Oysterbay kamchukueni
Kabisayule mhuni aliokubali sheria kubadilishwa ile ya mwaka 1996 kuhusu kukamata kwenye idara maalumu alikuwa na lengo ovu sana
Muoga ni muoga tuu ,,hata mkiambiwaje Bado mtakua waogaMimi nafiri government ingetoa tamko kua km mazingira yanautata na kunawatu wanaweza zuia wafanye kinachowezekana,wananchi wanahofia kufanya maamuzi kwakua hawana backup ila km kuna utata wananchi wanaruhusiwa kuingilia kati,sehemu km stand ya mbezi wapo watu wengi wanaoweza zuia but wanahofia usalama wao pia
Tangu nione Lymo amenusurika Kwa ubonge wake nmeachana na Dr.janabi na kula nakula sana liwalo na liweEndeleeni kula chips mayai msimsikilize Janabi,ubonge ndio silaha pekee ya watu wasiojulikana...
Inakumbusha hii StoryDogo ajajificha kule Iringa kwa pisi yake?
Wapi Kilima Nyege?Nondo yuko Karakana Oysterbay kamchukueni
Circumstantial evidenceTupe ushaidi
Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.
Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu
====
UPDATE
JamiiForums imewasiliana na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT Wazalendo Shangwe Ayo ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza Nondo alikuwa ametokea Kigoma baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kumalizika, ambapo wakati anashuka kwenye basi Stendi ya Magufuli watu wasiyojulikana watatu walimfuata kukawa na purukushani Nondo akijitahidi kujinasua lakini walifanikiwa kumchukua na kuangusha pingu walizokuwa wameenda nazo pamoja na begi alilokuwanalo Nondo
Matukio mengine ya utekaji kuwahi kufanyika nchini haya hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Shangwe ameeleza pia gari lililomteka Nondo ni Land Cruiser nyeupe yenye namba za usajili T 249 EMV. Taarifa za awali walizitoa kwa mashuhuda ambao walikuwa wanamfagamu Nondo, baada ya kufungua begi lake kulikuwa na note book ambayo nayo ilithibisha kumilikiwa na Abdul Nondo
Pia shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema gari hilo lililokuja kumteka Abdul Nondo lilikuwa na watu 4, wawili wakiwa na bunduki na wawili wakiwa mikono mitupu, watu walipoenda kuangalia kuna nini na kujaribu kuhoji waliwanyooshea bastola na hivyo watu kubaki wanaangalia tukio hilo likitokea na Abdul Nondo akawa ametekwa! Katika purukushani hizo kwa maelezo ya shuhuda mbali na pingu na bengi la Nondo, ilianguka pia inadaiwa simu ya moja ya watekaji ambavyo vyote vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Magufuli.
View attachment 3166434