Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
mwakani kitawaka zaidi ya hapa
 
yule mhuni aliokubali sheria kubadilishwa ile ya mwaka 1996 kuhusu kukamata kwenye idara maalumu alikuwa na lengo ovu sana
Kabisa

Imefikia kipindi watu wanakamatwa kama Kuku kisha kupotezwa

It is very unfair
 
Mpk ss kiungo Gani cha mwili wake mmeshakitenguaa nyie police CCM...

Ni huzunii
 
Mimi nafiri government ingetoa tamko kua km mazingira yanautata na kunawatu wanaweza zuia wafanye kinachowezekana,wananchi wanahofia kufanya maamuzi kwakua hawana backup ila km kuna utata wananchi wanaruhusiwa kuingilia kati,sehemu km stand ya mbezi wapo watu wengi wanaoweza zuia but wanahofia usalama wao pia
Muoga ni muoga tuu ,,hata mkiambiwaje Bado mtakua waoga
 
Dogo ajajificha kule Iringa kwa pisi yake?
Inakumbusha hii Story
maxresdefault (2).jpg
 
Mtoto naye anaropoka sana,alikua hajui yupo dunia ya tatu lolote linaweza kumkuta.
Na si huyu kuna kipindi alijiteka akakutwa ifakara kwa mwanamke.
Shenzi kabisa.
 
Tatizo watu wengi wana nidhamu ya woga hivi kwel hata kama mtu katoa siraha anaweza kupiga watu wote? Huyo anaetumwa kazi pia anajua akileta ujuani wa kuuwa watu hadhalani hao waliomtuma watamgeuka na kumpeleka kwa pirato mwenyewe itokee siku watanzani wabadike na kushikamana katika huu ukamataji holela na sio kulalamika huku mitandaon nq kutoa kauli za kulaan tu ambapo mwisho wa siku tumeubaliki jina la wasiojulikana wauliwe na hata huo usafiri wao kuchomwa moto ikitokea hvyo hata mala tatu tofauti itapunguza haya matukio ya kijinga kwa sasa, na huku matukio siriasi vyombo vya usalama vinachukulia kama kimebebwa kifaranga mpaka sasa wanafatilia nn si wamchukue huyo mmiliki wa gar aeleze nan yupo na gar yake kama sio yeye au hili nalo linahitaji kupigiwa kelele?
 

Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu

====

UPDATE

JamiiForums imewasiliana na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT Wazalendo Shangwe Ayo ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza Nondo alikuwa ametokea Kigoma baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kumalizika, ambapo wakati anashuka kwenye basi Stendi ya Magufuli watu wasiyojulikana watatu walimfuata kukawa na purukushani Nondo akijitahidi kujinasua lakini walifanikiwa kumchukua na kuangusha pingu walizokuwa wameenda nazo pamoja na begi alilokuwanalo Nondo

Matukio mengine ya utekaji kuwahi kufanyika nchini haya hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Shangwe ameeleza pia gari lililomteka Nondo ni Land Cruiser nyeupe yenye namba za usajili T 249 EMV. Taarifa za awali walizitoa kwa mashuhuda ambao walikuwa wanamfagamu Nondo, baada ya kufungua begi lake kulikuwa na note book ambayo nayo ilithibisha kumilikiwa na Abdul Nondo

Pia shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema gari hilo lililokuja kumteka Abdul Nondo lilikuwa na watu 4, wawili wakiwa na bunduki na wawili wakiwa mikono mitupu, watu walipoenda kuangalia kuna nini na kujaribu kuhoji waliwanyooshea bastola na hivyo watu kubaki wanaangalia tukio hilo likitokea na Abdul Nondo akawa ametekwa! Katika purukushani hizo kwa maelezo ya shuhuda mbali na pingu na bengi la Nondo, ilianguka pia inadaiwa simu ya moja ya watekaji ambavyo vyote vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Magufuli.

View attachment 3166434
 

Attachments

  • 5893626-2743c7572c5881f04ae7c078e6602840.mp4
    3.6 MB
Back
Top Bottom