Luv
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 2,739
- 6,099
Japo amekosea ila tujiulize.....
Imekuwaje hadi amefikia kumchoma mumewe aliyemchagua mwenyewe moto.
Wanaume "baadhi" epukeni kuwaumiza wanawake na Kisha kupuuza kumaliza migogoro, kwa kudhani huo ndio uanaume.
Mnawajaza hasira na hawana kwa kutemea nyongo. Mwisho wa siku wanafanya maamuzi ya kustaajabisha.
Wanandoa na nyie mkiona vurugu ni nyingi kuliko amani achaneni kila mtu aendelee na maisha yake. Acheni kuvumilia mnavyoona hamuwezi kuhimili.
Hakuna kaburi linaloandikwa "Aliolewa" au "Alioa" ni alizaliwa tarehe.... Na kafariki tarehe.....
Acheni upuuzi wa kuwaza jamii itauonaje tukiachana anzeni kuwaza tukiendelea kuishi kwa kuumizana mwisho wake nini!?
Ona sasa watoto wanakosa malezi ya baba na mama.
Wakati wangeachana watoto wangeweza kuendelea kuwaona wazazi wao hata kama ni kwa utaratibu maalum.