Pole yake marehemu. Lakini alishindwa nini kung'amua hatari iliyopo mbele yake iwapo alishakoswa koswa na petrol mara ya kwanza kama mwanajamvi mmoja alivyoeleza kwenye huu uzi? Pia marehemu alishindwa nini kujua mapema kama ana "date" na kichaa kabisa? Huyo mwanamke kwangu mimi ni kichaa kabisa ni wale machizi fresh ambao wapo wengi wa kike na kiume huku mitaani. Mpaka kufikia kuchoma nyumba ni lazima huyu mwanamke alishafika levo za kuongea mwenyewe kwa sauti na lazima alikuwa anataja jina la merehemu na kujiapiza mara nyingi tena kwa ubaya. Kama marehemu na watu waliokuuwa karibu naye walichukulia poa basi matokeo ndiyo hayo.
Kwa binadamu mwenye akili timamu hawezi choma nyumba ambayo ina wapangaji wengine ndani tena tunaambiwa hapa mama na mtoto walikuwa ndani chumba kingine wakatoka salama, kuna fremu ya fundi piki piki na duka la dagaa achilia mbali hasara aliyompa mmiliki wa nyumba. Mtu ambaye amewapa hasara zisizo na fidia wenzake waliodunduliza kupata mitaji kisa huyo Mario wake aliyekuwa anampa bia za bure huyo sio mzima wa akili na ni mbinafsi kwa kiwango cha juu.
Angalizo kwenye mahusiano; ukiwa mme au mke ukiona mbele hakuna mwanga basi chukua maamuzi magumu ya kuondoka au kuachana bila kujali mali, vitega uchumi na muda uliowekeza kwani uhai ni mali zaidi ya hivyo vyote. Ukipuuza na kuona ngoja nivumilie au watu watasemaje basi ndiyo hayo ya petroli na gunia za mbili za mkaa yatakukuta.