Dar: Amchoma mpenzi wake na Petroli kisa wivu wa mapenzi

Dar: Amchoma mpenzi wake na Petroli kisa wivu wa mapenzi

Well said member. Ndio maana naendelea kumshangaa huyu Bwana Mshana Jr kwa kutetea unyama huu tena kwa makala zake ndefu.
katoa boko yaani anashabikia kutoa uhai wa mtu? hapana aisee napingana na kila aina hili maumivu ya mapenz yapo yanapita na hata huyo dem sio kwamba huyo marehem ndio alikuwa jamaa yake wa kwanza hiyo ngumu sana kwa vizaz vya sasa kuna watu wamefungua njia hapo
 
  • Thanks
Reactions: BRB
Aisee sikia moto kwa mwenzio ila usikupate, fahamu tu hata ile hewa ukiivuta tu inatosha kutoa uhai.
itakuwa pombe mkuu jamaa alilewa sana kwa umr ule mlango angetoka nao labda kama nje kulikuwa na geti la chuma ya kuchomea
 
Sikilizia povuuu la wanaume humu sasa[emoji1787][emoji1787][emoji14]

Wanawake sasa wameamka, huu ndo uanamke wa shoka, sio kuja kulia lia humu sijui napigwa, sijui nanyanyaswa! Piga petrol[emoji16][emoji16]
wameamka kwa kuua? hata mwanaume kuua mwanamke ni ujinga unapambania mtu ambae hakupendi jamani huu si ujinga? ukishagundua mtu hakupend tafuta njia nyingine utayopata pumziko sasa anateseka maisha yake yote jela na roho ya kuua inamuandama
 
kwenye maisha kuna changamoto kubwa sana niliwahi kuchukua mkopo na mwanamke ambae angekuwa mke wangu hapo ieleweke hatua zote zilifuatwa ilibaki ndoa tu tuliwekeza ktk biashara kwa bahat mbaya zilikufa vibaya sana kisha akaanza kutoka nje ya mahusiano tuliachana kwa aman nilikuwa na maumivu mawili makubwa kwanza kupoteza pesa kisha kusalitiwa ila roho yangu haikuingiwa na tamaa ya visasi kwake na kwa jamaa zake bado naishi napambana sikati tamaa ila yeye analia sasa kwa hiyo kuna baadhi ya changamoto zinakujenga kufika sehem fulani sasa kama pengine kaona jamaa ni msaliti ilikuwa ni alarm ya yeye kusonga mbele sio kulilia uhusiano usio na tija Mungu ana lengo lake kukuonesha uovu mapema ujipange kutafuta njia yako sahihi.

Ktk maisha yangu naumia sana kuona mtu anatoa uhai wa mwanadamu mwenzie ni hatua mbaya sana huwa naendesha gar nawaza sana kama ikitokea nimegonga mtu nitafanyaje? kisha akafa naomba sana kwa Mungu nisipate hiyo kitu nasema hivyo kwa sababu naona watu wanavyolea watoto wanapata tabu sana halafu unakuja kutoa uhai wa mtu kirahisi sana tujifunze kusoma alama za nyakati endapo unaona sehem uliyopo unapata tabu.

kuua mtu ni dhambi moja mbaya sana siamini kama neema angekosa mtu.
Watu wanachukulia vitu tofauti. Moyo wako ulivyoumbwa ni tofauti na mwingine. Mioyo ya wengine hadi ilipe visasi ndio inatulia. Binafsi nikiumizwa ninavyozidi kulia ndo nautoa uchungu mwisho uchungu unaisha wote mwishowake nasahau
 
Jamaa kakamatika kizembe sana,ila hakutegemea.

Hela yenyewe huyu mwanamke alipokea ya mchezo kutoka kwa wapika supu wenzake tuliwahoji wakasema hivyo.
Hisia za kusalitiwa ➡️ Kikundi cha wauza supu ➡️ hela ya mchezo ➡️ Mauwaji ➡️ jela

Kuna mambo mengi sana yanajificha kwa huyu killer, haiwezekani ikawa kirahisi hivo
 
kibiashara wako vizuri, lakini wana roho za mafarakano, chuki, ulipaji visasi na ukatili =UPALESTINA
 
  • Kicheko
Reactions: BRB
Hamiwezi jua alipitia mateso kiasi gani hadi kufanya hivyo. Kuna wanaume wanajua kutesa wanawake kisaikolojia hadi ujiulize kama alizaliwa au aliokotwa
Mwanamke siaende kwao kuliko kuozea jela
 
Huyu dada namfahamu vizuri, na muda mrefu nilimuona ana matatizo fulani ya kisaikolijia isipokuwa inavyoonekana jamii inayomzunguka ilimchukulia kama mtu fulani mkorofi so akakosa tiba sahihi. Hata ulikuwa ukienda pale njia panda ya Makabe alipokuwa anauza kongoro alikuwa ni mtu mkorofi mkorofi hivi, kidogo tu kagombana na mteja. Huyo zungu hakuwa mumewe bali hawara tu, kilichomuuzi nafikiri ni kugundua kwamba Zungu alikuwa na mwanamke wake mwingine na mtoto.
kumbe unamjua?? mwenye picha ya Zungu waiweke
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787] mkuu tulia kwanza...ya magunia imexpire hiyo

Habari ya mjini ni petrol

Jokes aside....ukiona mpaka mwanamke kafikia hatua hiyo ujue yalimfika hapaa, huwa sisi ni wavumilivu sana sana
kuvumilia mume kucheat au?
 
Hakuwa mumewe ni vimada tu na walikuwa wameshaachana ila huyu mwanamke jana akamtega dogo Zungu kwa bia za bure kisha akampeleka chumbani kwake tena kwenye nyumba anayomiliki baba yake akaenda kumtia kiberiti nilisikitika sana alitolewa mule ndani kawa kama kuku aliyebanikwa.

Zungu tunamzika saa kumi hii hapa Msakuzi makaburi ya Makamba.
Zungu alikuwa ana miaka mingapi?
 
Bibi zetu walikuwa wakishaona wamezeeka walikuwa wanamtafutia Mzee kabinti kama mke mdogo anapata chenona ili ndoa iwepo na maisha ya songe. Sasa hawa wa siku hizi tena Mchaga hamu hapati mpaka amalize marejesho wewe ukae tu unaangalia kisa mlisaidiana maishani?
mabibi wa kabila gani mbona sijawahi sikia
 
Mungu ni mwema alitoka na anasema alitoka nje ili akajisaidie haja ndogo kurudi akakuta chumba cha mtoto wa mwenye nyumba ndani mnafuka moshi huku mtu anagonga kwa ndani afunguliwe alichofanya akaenda kumwamsha mwanae wakatoka nje kuomba msaada kwa majirani kurudi corridor nzima imeshajaa moto.

Hata huyu aliyefanya unyama huu aliungua miguuni akatoka nje mbio uchi,vitu vya ajabu sana.
duu!!! ilikuwa saa ngapi?
 
Back
Top Bottom