Dar: Baba adaiwa kuwapa sumu watoto wake watatu

Dar: Baba adaiwa kuwapa sumu watoto wake watatu


Dar: Karim Shabani mwenyeji wa Chanika jijini Dar es Salaam, anadaiwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwapa sumu aliyoiweka kwenye juisi, baada ya kutuhumu mtoto wa mwisho aliyezaliwa na mkewe sio wake na hafanani naye.

Juma Mohammed ambaye ni msemaji wa familia ya marehemu, amesema Karim aligombana na mkewe kutokana na sababu hiyo ya mtoto wa mwisho na kupelekea kutengana miaka miaka miwili iliyopita na watoto kwenda kuishi kwa bibi yao mzaa baba.

Inaelezwa mtuhumiwa huyo juzi alifika kwa wazazi wake na kuwachukua watoto wake watatu kwa lengo la kwenda kusherehekea nao Sikukuu ya Eid sehemu anayoishi lakini aliamua kuwapa watoto wote juisi yenye sumu, watoto wawili walifariki dunia na mmoja anaendelea kupatiwa matibabu katika Hosptali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa wa tukio hilo tayari anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo.

Chanzo: GADI TV
Dah
Jamii imelishana ujinga na kuna watu humu mitandaoni hushabikia njia za mkato za kutatua changamoto za ndoa.

Familia imepoteza baba na watoto.

Sasa kama alikuwa anamtuhumu mtoto mmoja si wake, kwa nini aliamua kuua hadi wanae halali?

Kuna jambo nikilisema hapa walami watasema naingiza siasa. Anyways wacha niseme kama mbwai iwe mbuayi

Hali duni ya uchumi wa mtu kwa mtu nchini inqpelekea sonona na mzio kuwa mkubwa
 
Kwahiyo baada ya kugundua mtoto mmoja sio wake ndiyo aamue kuua, kwani hao watoto wana kosa gani?

Biblia inasema huwezi kumuacha mke/kumtaliki isipokuwa kwa Uzinzi tu yaani kuchepuka.

Yeye alishindwa nini kumtaliki mkewe/kumuacha baada ya kugundua hayo.

Alafu yeye amewezaje ku conclude kuwa mtoto sio wake baada ya kujua kuwa hafanani naye, vipi kama anafanana na Babu yake ama ndugu yake hata wa Ukikeni huko.

Sometimes ni vyema kujipa muda wa kutafakari kabla hujafanya maamuzi yeyote mazito kama haya.

Mungu awarehemu watoto hawa na awape pumziko la milele 😭
 
Wabinafsi, Wanapenda kushindana, wanapenda vitu kuliko utu..
Wanawake ni mashetani yanayo tembea hapa duniani na tunaishi nayo mimi nawachukia sana wanawake wana roho mbaya sana i speak from experience
 
Wanawake ni mashetani yanayo tembea hapa duniani na tunaishi nayo mimi nawachukia sana wanawake wana roho mbaya sana i speak from experience
Mama yako, dada zako, mashangazi zako unawachukia pia.
 
Kabla hajafunguliwa mashitaka apimwe akili kwanza!
Ndoa za kizazi hiki!
 
Back
Top Bottom