Duu! Yaani hii awamu ya tano imeumiza karibu kila sekta! Wakulima hoi, watumishi hoi, wafanyabiashara choka mbaya! Wavuvi ni vilio vitupu! Afya nako ni majanga matupu na sasa hata watumishi wenye BIMA kuna madawa ya ghara yameondolewa kulipiwa na mfuko nao sasa watalazmika kuyalipia pamoja na kukatwa fedha zao kila mwezi! Ni wakati sasa tufanye mabadiliko yenye tija kwa taifa letu! Nawasihi sana CCM tambueni kuwa wananchi wameumizwa vya kutosha na serikali zenu, kubalini kukaa kando ili mkajitathmini na kujipanga upya! Hata nje ya kuwa chama tawala kuna maisha mbona vyama vingine vilianzishwa tangu 1995 lakini vipo na vinadunda na havijawahi kuwa vyama tawala! Shime ndugu hasa wale ambao huwa hamjitokezi kupiga kura tafadhari mwaka huu kura yako itakuwa na thamani ileile unayoitaka kwani Mungu ameshabariki uchaguzi wetu hakuna wa kupindisha mambo atakayefanikiwa!