Dar es Salaam kilo moja ya mchele wanashiba watu wanne, Mikoani kilo moja mtu mmoja tatizo liko wapi?

Dar es Salaam kilo moja ya mchele wanashiba watu wanne, Mikoani kilo moja mtu mmoja tatizo liko wapi?

Dar msosi sio shida,vyakula masokoni havina bei
Dar vyakula ni vingi lakini bei ni kubwa na upatikanaji wa hivyo vyakula ni "lazima" uwe na pesa. Huko mnakoita mikoani wengi wana mashamba yao (hata wanaoishi mijini wanakuwa na mashamba vijijini au nje ya mji) hivyo wanajipatia majitaji yao bila kulazimika kwenda sokoni, huo ndiyo utofauti.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Sio kweli Dar wanakula vizuri kuliko wa mikoani
Wanakula vizuri kwa maana ya quality au quantity?

Huko Dar kilo moja ya nyama mnakula siku 3 hadi 4...

Huku mikoani kilo moja ya nyama tunakula mchana tu, usiku tunakula maboga na makande ya ntwiri...

Kimsingi Dar maisha magumu...

Ukitaka kuamini hilo, nenda Masaki uone wanavyokula vyakula vingi, maana hawawazi...
 
Mapishi nayo yanachangia. Kuna mtu anapika nusu kilo ya mchele mnakula watu wanne na mnashiba vizuri na kunaweza baki.

Wengine wameenda mbali wanahusisha na roho ya mtu, mara ukarimu. Mambo ni mengi hapo.

Ni kama ilivyo kuna mtu akipika chakula kinaweza kukaa hadi siku mbili kisiharibike ila mwengine kikilala tu kishaharibika.
Nakubishia aisee. Huku Usukumani hapana ndugu yangu. Nusu kilo ya mchele hiyo ni stata tu. Ndiyo chakula (ugali) sasa kije. Hata peke yangu hapa Misungwi siwezi kula wali nusu kilo halafu nilale. Hapana aisee labda kama nimefulia!😁
 
Mikoani ni wapi? Kwanini Dar mnaitenga na mikoa mingine? Nnachojua Dar ni mkoa kati ya mikoa mingi tuliyonayo, au Dar ni wilayani?

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
Kwasababu niko Dar, kwahiyo mikoa mingine nawaita wa mikoani. Nikiwa Mbeya, mikoa mingine huwa nasema wa mikoani na Dar ikiwemo haitengwi.
Nikiwa Moshi, mikoa mingine nawaita wa mikoani.
 
Duh Dar mchele unaanzia 2800? Ushawahi kwenda kununua sokoni au hata duka la mangi?
Mara nyingi huagiza wa kutosha mkoani but kuna kipindi niliwahi kununua ndo bei niliyoikuta

japo ulikuwepo wa mpaka 2400 lakini umekatika sana kama wa wapika vitumbua!!
 
Tuliozaliwa milimani lazima ule sana,baridi,mvua,kazi za shamba. Kuna kipindi nilisafiri kwenda Dar,sasa baada ya miezi michache nikarudi mkoani,kuna siku moja usiku nilikula half cake 2 zile za sh.200 pamoja na maziwa fresh. Aisee niliamka usiku njaa inaniuma balaa,nilikataa kula nikaiga kula ya Dar. Asubuhi cha kwanza nikachemsha mchaichai nikanywa,nikachukua asali nikalamba ili tumbo likae vizuri na baadae ilibidi nile kiporo chote. Sikurudia tena
 
Mjini tunakula zaidi mboga.
IMG-20240715-WA0050.jpg
 
Tuache wa mikoani bwan,, kwanz barid huku
 
Wale wataalam wa lishe au wale wataalam wa mahesabu, cross multiplication HiI Imekaaje.

Wote ni watanzania ila matumbo mengine yanapokea full tank.

Niko mkoa ambao sitautaja,nimeshuhudia mtu na mkewe wakipija wali kilo mbili na kubakiza kidogo sana,kwa uzoefu wangu wakuishi Dar kili mbili tulikuwa tukilafamilianzima ya watu nane na unabaki kidogo kiporo cha watoto asubuhí.

Hii imekaaje
Katika kishe wali hauna virutubisho vingi sana, sehemu kubwa ni carbohydrates/ wanga, ni kitu cha kukupa nguvu.

Virutubisho vingi vinatoka kwenye mboga utakazokula na wali.

Hivyo kika wali mwingi kunaweza kusikuoe virutubisho vingi kama mtu anayekula wali kidogo na virutubisho vingi.

Tati,o Watanzania wengi wanakula ili kujaza matumbo, hawali ili kupata virutubisho vingi.

Kwa hiyo anayekula wali mwingi na kijaza tumbo anaonekana kala sana, wakati kujaza tumbo kwa wanga si kujaza virutubisho mwilini.
 
Back
Top Bottom