Dar es Salaam kilo moja ya mchele wanashiba watu wanne, Mikoani kilo moja mtu mmoja tatizo liko wapi?

Dar es Salaam kilo moja ya mchele wanashiba watu wanne, Mikoani kilo moja mtu mmoja tatizo liko wapi?

Mm nakulaga kdg sana na kwakwel sipend kula kdg, mm napenda nle sana yan nijaze bas tu madonda ya tumbo yananinyima appetite
Hayo madonda yanataka antioxidant,

Tumia alkaline kwa wingi kupitia limao, tumia pilipili usidanganywe kwamba pilipili haifai kwa hayo madonda, dawa ya moto ni moto.

Tumia na Acid reducer hayobmadonda yatakukoma kabisa, utakula misosi yote pilau, dagaa maharagwe.

Ila machungwa na juice yake achana nayo yana citric acid nyingi mbaya kwako.

Dawa yako kuu ni limao, Alkaline ndio anti diseas namba one muulize daktari yeyote unayemuamini.
 
Kaka kwenye swala la kula inategemeana na hali ya kiuchumi huk huk mjini kuna watu uchumi umekaa vizuri kilo moja inaliwa na watu wawili japo unakuta kuna mazaga zaga kibao sasa njoo huku mkoa wa mara WATU HAWAAMINI KAMA WALI NA CHAKULA CHA KUSHINDIA yaani wanaamini wali ni kifungua kinywa tu means ukipika wali lazima upike na ugali au aidha aanze na ugali ndio amalizie cha mtume. The same na watu wa kilombero njoo huku malinyi ndani ndani maeneo kama biro, ngoheranga, tanga, kilosa kwa mpepo wat wanaamini wakila ugali wanakojoa saana hvyo chakula chao ni ubwabwa tu. Hvyo ni mazingira tu.
 
Inategemea ntu na ntu.
Inapendeza zaidi mtu akila akashiba


Cc Smart911
Ukienda kwenye restaurant standard mfano ukaagiza ugali na sato, unaletewa kaugali kadogo sato rost mkubwa na mbogamboga lazima ushibe vizuri tu.

Lakini ule ulaji wa mjumbani kwetu ugali na nyama na finyango mbili ni lazima utakula ugali mwingi.

Kimsingi mboga hazitakiwi kupunguwa tatu na shida siyo umaskini bali uvivu wa majumbani mwetu hawataki kupika muda mrefu, mimi ni kawaida kwangu kwenye friji kabichi na mchicha bwasi kukuta vimeharibika navitupa kwenye dustbin.
 
Mapishi nayo yanachangia. Kuna mtu anapika nusu kilo ya mchele mnakula watu wanne na mnashiba vizuri na kunaweza baki.

Wengine wameenda mbali wanahusisha na roho ya mtu, mara ukarimu. Mambo ni mengi hapo.

Ni kama ilivyo kuna mtu akipika chakula kinaweza kukaa hadi siku mbili kisiharibike ila mwengine kikilala tu kishaharibika.
Wife akipika chakula huwa akibaki

Siku za sikukuu huwa anaalika watu, hawaji wote aliowaalika lakini cha ajabu waliopo watakula mpaka kinaisha

Ila anajua kupika maana sijawahi kula chakula chenye ladha nzuri kama anachopika yeye
 
Watu masikini wanakula vyakula vyenye wanga mwingi (ugali, wali) kujaza matumbo na kupata energy.

Wakati lishe bora haitaki wanga mwingi sana, inataka virutubisho, protein, vitamins, minerals. Ambazo hizi zinapatikana katika mboga/ kitoweo.
Ni umasikini kwa kiasi kikubwa na pia kuna suala la ukosefu wa elimu bora ya lishe, mikoa mingi ambayo ina utapiamlo huwa wanazalisha sana mahindi na mchele pamoja na maharage pia, wanaweza kufuga kuku pia wakapata hata mayai ya kuweka kwenye uji wa watoto wao, sasa cha ajabu hawayapi umuhimu maharage kwenye diet zao, wamekaririshwa utoshelevu wa chakula ni kuwa na magunia ya mahindi na mchele tu ndani. Hata serikali sidhani kama huwa inanunua maharage, mbaazi, dengu na kunde kuhifadhi kama sehemu ya kuweka akiba ya chakula katika nchi.
 
Kaka kwenye swala la kula inategemeana na hali ya kiuchumi huk huk mjini kuna watu uchumi umekaa vizuri kilo moja inaliwa na watu wawili japo unakuta kuna mazaga zaga kibao sasa njoo huku mkoa wa mara WATU HAWAAMINI KAMA WALI NA CHAKULA CHA KUSHINDIA yaani wanaamini wali ni kifungua kinywa tu means ukipika wali lazima upike na ugali au aidha aanze na ugali ndio amalizie cha mtume. The same na watu wa kilombero njoo huku malinyi ndani ndani maeneo kama biro, ngoheranga, tanga, kilosa kwa mpepo wat wanaamini wakila ugali wanakojoa saana hvyo chakula chao ni ubwabwa tu. Hvyo ni mazingira tu.
Watu wenye uchumi mzuri hawawezi kula kilo moja ya wali watu wawili,
 
Sasa huko Dar kila muda wanakula tu na hawana kipimo. Mtu akitoka mishe kabla ya kufika nyumbani unakuta kashabugia sambusa, mishkaki, uji na pweza. Unategemea ukimpa huo wali ½ atamaliza?
Binadamu anayejielewa vizuri ndio anatakiwa kula hivyo, sio kujishindilia wali au ugali tu kama tumbo lako ni debe, kula vitu vingi vyenye virutubisho mbalimbali hakuna shida ila kujaza tumbo kwa mlo wenye virutubisho vya aina moja ni matatizo.
 
Nadhani aina ya kazi MTU anafanya then aina ya mapishi .

Kiufupi robo ya mchele inamtosha MTU mmoja ikiwa haufanyi Kazi ngumu.
 
Mfumo wa maisha unabadilisha mtu na mtu
Ukizoea ugali miaka halafu ukabadili life style na kuanza kula chips mayai na burger 🍔 basi ukiwekea ugali tena utashindwa kula kama zamani
Nilikuwa nakula saa saba mchana msosi
Ila siku hizi nakula saa 10 jioni
Ni mfumo wako tu
 
Back
Top Bottom