Dar es Salaam kilo moja ya mchele wanashiba watu wanne, Mikoani kilo moja mtu mmoja tatizo liko wapi?

Watu wenye uchumi mzuri hawawezi kula kilo moja ya wali watu wawili,
Nnavyojua mimi ukiwa na uhakika wa kula basi utakuwa huli sana

Yaani unatembea na 300k mfukoni ipo tu kama dharula, yaani una 300k haina bajeti ipo ipo tu kwenye waleti home umeacha mazaga kama yote na una uhakika wa kula, basi amini huwezi kula hovyo hovyo
 
Hiyo ni kweli
 
Kweli kabisa.

Cc Smart911
 
Binadamu anayejielewa vizuri ndio anatakiwa kula hivyo, sio kujishindilia wali au ugali tu kama tumbo lako ni debe, kula vitu vingi vyenye virutubisho mbalimbali hakuna shida ila kujaza tumbo kwa mlo wenye virutubisho vya aina moja ni matatizo.
Sawa, endelea kula hiyo miguu ya kuku na mishikaki ukashike jembe.
 
Kula karanga, korosho, pweza, sambusa, mishikaki, maziwa, mayai, matunda kwa muda tofauti katika siku sio kula hovyo hovyo, hivi ni aina ya vyakula vyenye virutubisho vingi muhimu lakini pia visivyo na side effects nyingi vikizidi. Kula hovyo ni ulaji wa vyakula vya sukari, junk foods na kushindilia tumbo mikate, chapati, ugali au wali katika mlo mmoja.
 
Sawa, endelea kula hiyo miguu ya kuku na mishikaki ukashike jembe.
Ukulima wa kushika jembe ni kilimo cha ujima cha zamani sana kilichopitwa na wakati, hakuna sifa katika kilimo cha hivyo.
 
Mkuu mm hata uwe umenidanganya nitafanya maana imekuwa noma sasa
 
Si useme tu kuwa upo Shinyanga!
 
Yuko sahihi nimewahi ishi Tukuyu pale ni baridi nilikuwa nachapa msosi hadi najishangaa,wakati home ni Kyela kule ni joto , msosi hatufukii kihivyoo .
Nilizani kanipiga na kitu kizito πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ila tatizo linakuwa wapi hadi inatokea hivyo ??πŸ€”
 
Hao wote hamna kitu.Waje hapa ninapoishi wapate tuisheni.Unga kilo kadhaa unapikwa ugali halafu unakatwa kidogo ndiyo unakuwa mboga.Yaani tunakula ugali mkubwa kwa kutoeza kwenye ugali mdogo kama mboga.
 
Hapo unakuwa unakula wali peke yake au pamoja na vyakula vingine kama nyama/samaki, mboga za majani na matunda pamoja na vinywaji?



Yes , Ila naona umegusia classic family and not commoners families

Kama utapata
Nyama
Matunda
Maji safi

Basi wali robo utakuwa mwingi Ila ukila wali robo na finyango moja au mbili za nyama bila matunda n.k basi robo ya wali itakuwa nyingi Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…