Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Haikuhitaji kuwa mfuasi wa chama au dini Bali ubinadamu tu unatosha kujua kiwango cha unyama waliofanyiwa na wanaoendelea kufanyiwa......

Itikadi zao au mitazamo ya kisiasa hailalishi unyama waliofanyiwa........
 
Serikali ya CCM pamoja na madhila yote wanayo wafanyia wananchi bado wameona haitoshi Sasa wameona hata ugali wao pia wautie mchanga.......

Endeleeni tu watawala wa CCM hili bomu mnalolisuka likija kulipuka litaleta maafa makubwa sana sio kwa wananchi bali hata kwenu pia........

Ukandamizaji, unyanyasaji, na uonevu dhidi ya wenye haki ndio chimbuko la ugaidi na vita vya wenyewe kwa wenyewe......hatuna haja ya kufikia huko kama badala yake lakini watawala wanawasukuma wananchi wafikie huko.......Mungu aepushie mbali.......
 
Wanaandamanaje wakati mkuu wa mkoa yuko pale pale
 
"Tunataka soko letu"..... hiyo ardhi ni yao?
 
Ni jambo la kawaida faida na hasara kwenye biashara.
 
Hio ndio ile moment unaweza kumtia mtu ngumi jabali ukamzimisha sababu una stress mbaya kmmmmke
 
Hakuna mmachinga mwenye ubavu wa kuandamana.
Tutamkanyaga mpaka atamtaja aliyemtuma.
Team Jiwe a.k.a Sukuma gang kwisha habari zenu
 
Ccm ni chaka la maadui wa watanzania.
 
Wamachinga wa nchi hii tunapata tabu sana. Nafikiri wanataka kuweka STAND ya DALADALA pale maana mpaka sasa hivi stendi za daladala zimekuwa adimu sana.
Wacha wawafukuze ili wajue kuwa ccm ni sawa na jini mahaba wakati wa uchaguzi
 
Wewe endelea kuwacheka kwa kuchekeshwa na vilio vya watu uliowataja mamalishe, machinga, wakulima

Ila utambue ndo kundi la walio wengi nchi hii kama si wazazi wako ni ndugu zako pia wamo humo sasa endelea tu kuwacheka Mkuu bilionea.
 
Mwenyekiti wa machinga kuambatana na CCM, haimaanishi machinga wote Ni CCM
Mfano sheikh wa Dar muda wote yupo na CCM, hii maana yake waislamu wote wa dar Ni CCM?
Ndio maana yake hiyo kwa kuwa alikuwa anasema katumwa kuwawakilisha machinga wote
 
Machinga hawawezi kuiondoa ccm maana ndiyo chama chao.

Hao hao walitumika na ccm chini ya mwenyekiti wao kuwatukana viongozi wa upinzani na wapinzani kwa ujumla wao.

Mungu huwa analipa hapa hapa duniani na ukisha kufa ni mahesabu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…