Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Hao machinga wawe wapole tu wasubirie uchaguzi mkuu ndipo thamani yao itaonekana
 
Watu washakula 10 % zao na machinga msikate tamaa ,daini haki yenu
 
Ukisikia GSM kakabidhiwa hapo wala usishangae. Soko dogo la Kariakooza chini chini zinadai tayari kashakabidhiwa. Yale madai ya kuwa rimoti ameshikilia msoga naanza kuyaamini.
Huyo MSG Ndiyo mzoga mwenyewe kama ulikua hujui
 
Kwani wewe ukiwasaidia kunatatizo lolote? Wasaidie wanunulie maandazi na vitumbua wawapelekee watoto wao.
 
Kama nyumba yako imeungua moto na unaamua kuweka kibanda ujisitiri akija mtu kubomoa hicho kibanda ni wazi mtu huyo ndio aliechoma moto nyumba yako!
Kabisaaa........hapo lazima chinga wajiongeze hawana chao tena.
 
Hii ni baada ya Jeshi la Polisi kuamua kutumia nguvu ili kutawanya maandamano ya Wafanyabiashara waliounguliwa na bidhaa zao kwenye soko la Karume usiku wa kuamkia jana .

Bado tunaendelea kuchunguza ili kubaini idadi ya majeruhi na labda idadi ya waliokamatwa .
 
Kutumia nguvu hakusaidii kabisa, inatakiwa waangalie jinsi ya kuwaruhusu machinga wafanye biashara zao.
 
Kiukweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.

Wanasiasa hebu wasaidieni hawa wamachinga wanapita katika kipindi kigumu sana...
Sasa usiwe kigeugeu wa kisiasa.

Wamachinga wametoka wapi hapa nchini, kila mtu akkimbila Dar es salaam ili awe mchinga Jiji hili litakuwaje.

Halafu badala ya kusema siasa zetu zikirie kuendeleza kilimo ili kila mtu ajiajiri kwenye kilimo, wewe unataka wasidiwe watu mia moja u mia mbili watu ambao ni wachache mn kufikiriw kisera.

Viongozi waanzishe sera jumla jumla za kuwaendeleza Watanzania kue walo, kijijini.
 
Hili bomu la wamachinga ipo siku litalipuka na kusiwe na wa kulizima...
 
Eneo la breweries lile

Enzi za makamba,walipokuwa wanawatoa wamachinga kko,wakapepelekwa pale...
Sio eneo la brewaries, lilikua eneo la wazi na ndio maana kumetenganishwa na barabara kubwa inayoshuka chini mchikichini.
Brewaries eneo lao linaishia palepale, mpaka ni ile barabara.
 
Nawauliza machinga; Vipi hapo nani anafaa kupigiwa kura kwenye uchaguzi ujao?, maana nafikilia kuweka picha ya marehemu na hii ya sasa?.
 
 
Rekebisha kauli, machinga hawapo dar tu. Wapo mikoa yote nchi nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…