Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Sasa naamini kuna uwezekano mkubwa serikali ikawa inahusika na haya matukio ya moto unaounguza masoko ya nchi hii usiku tu, hawa hawawezi kujichunguza ndio maana huwa hawatoi majibu ya ripoti za tume wanazounda, hawa ni corrupt.
Hivi zile shule zikizokuwa zinaungua kila wiki kipindi kile
Inaweza kuwa na yenyewe ni hujuma?
Eeh
 
Je historia ya eneo la Karume ni ipi? Kama walivamia wahesabu maumivi. Kama halipo kwenye master plan ya jiji kama eneo la biashara ndio imekwisha hivyo.
 
Moto umekuwa unafuatana sana na Makala. Kote alikopita masoko yaliwaka moto. Waanze na Makala kwanza ana weza kuwa na kiberiti chake maalum kuumiza wahangaikaji kwa lengo la kuwahamisha 😔😔😔😔
 
Katambi amekusikia!
 
Bora mkolon arudi kwnye hii nchi kulko mkolon ccm
Hayo yote ni kuonesh jinsi gani serikali inashindwa kuwapa kipaumbele watu wake nakutatua matatizo on time. Haina haja yakuja mkoloni bali nyinyi wenyewe wananchi mnaweza sema ndio hivyo wakianzisha wenzenu nyinyi mnajifungia ndani mnasema kaandamaneni wenyewe. Kwa style hiyo wacha CCM iendelee kuwanyoosha.
 
Umekariri kila machinga katoka mkoani!? Machinga kibao wa hapa hapa Dar na hawakujui huko mikoani. Hao watu kwani serikali ndio huwa inawalisha kabla ya hili tukio!? Waachwe wajitafutie wenyewe wala haeaendi ikulu magogoni kuomba.
 
Wamachinga wa nchi hii tunapata tabu sana. Nafikiri wanataka kuweka STAND ya DALADALA pale maana mpaka sasa hivi stendi za daladala zimekuwa adimu sana.
Hadi mtakapojitambua ndiyo hamtapata tabu, vinginevyo acheni mpigwe tu.
 
mammmamae waliependa wenyewe chaguo lao wenyewe, wacha waisome namba ccm mbele kwa mbele.
 
Pamoja na yooote tukubaliane kurudisha tena mabanda pale ni upunguani, pale ni kati kati ya mji pajengwe soko lenye hadhi ya eneo husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…