Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Kwasasa ni mabomu ya machozi yanatembea. Gusa vyote usiguse ugali wa maskini!
 
Hapo mwishoni umeeleza vizuri....."na hii katiba kandamizi"

Kudai katiba mpya haiitajiki chama cha upinzani.Sisi kama wananchi tuna wajibu wa kudai katiba mpya ili tupate vyama vya siasa vyenye nguvu.Je,sisi kama wananchi tunatimiza wajibu wetu wa kudai katiba mpya?
Kwakweli hapana ,tunahitaji lakini tunashindwa kutimiza wajibu wetu kuidai...

Tungekuwa na mizizi imara hili hili tukio ndio lingekuwa sababu ya kuingia mtaani.wenzetu huko yule machinga aliyejiua kwa moto ndio ilikuwa sababu ya wao kutimiza hitaji la mabadiliko.

Kwa haya matukio ya sasa nchini kwetu bado kidogo tu uzalendo utatushinda.
 
Ni kweli wote walikenua meno? Nadhani tunasema uongo hapa, yani wafanyabiashara wote wa karume wawe ccm?
Linapokuja suala la kuiondoa madarakani serikali kandamizi yenye Bunduki,mabomu,polisi,jeshi,TISS na kadhalika siyo suala la huyu aliikataa CCM na huyu aliikubali CCM.

Ni suala la kuungana na kuwa kitu kimoja.Ni suala la kushawishi kila mtu aikatae serikali hiyo.

Hao wachache ambao unadai kuwa waliikataa CCM kosa lao ni kwamba walishindwa kumshawishi kila mmachinga aikatae CCM pia kwa hiyo wao pia wanadeserve adhabu hii.
 
Una uhakika kuwa hao wote walikenua hayo meno?
Linapokuja suala la kuiondoa madarakani serikali kandamizi yenye Bunduki,mabomu,polisi,jeshi,TISS na kadhalika siyo suala la huyu aliikataa CCM na huyu aliikubali CCM.

Ni suala la kuungana na kuwa kitu kimoja.Ni suala la kushawishi kila mtu aikatae serikali hiyo.

Hao wachache ambao unadai kuwa waliikataa CCM kosa lao ni kwamba walishindwa kumshawishi kila mmachinga aikatae CCM pia,kwa hiyo wao pia wanadeserve adhabu hii.
 
Kubomolea watu Ni Kama kula nyama ya mtu. Huwezi kuacha.
Baada ya kuwabomolea nyumba wananchi wa Kimara Mbezi kwa kisingizio kwamba wako upinzani Sasa Ni wale wale wamachinga, wanyonge, kundi pendwa. Na Hawataishia hapo.
 
Linapokuja suala la kuiondoa madarakani serikali kandamizi yenye Bunduki,mabomu,polisi,jeshi,TISS na kadhalika siyo suala la huyu aliikataa CCM na huyu aliikubali CCM.

Ni suala la kuungana na kuwa kitu kimoja.Ni suala la kushawishi kila mtu aikatae serikali hiyo.

Hao wachache ambao unadai kuwa waliikataa CCM kosa lao ni kwamba walishindwa kumshawishi kila mmachinga aikatae CCM pia kwa hiyo wao pia wanadeserve adhabu hii.
Walishindwa vipi kushawishi watu kuikataa CCM, wakati CCM walishindwa uchaguzi? Au unataka kusema ule uchaguzi CCM walishinda?
 
hali soon inaweza kuanza kuwa tete
maana jamaa wanataka wajenge soko kwa gharama zao wenyewe
20220117_134146.jpg
20220117_134143.jpg
 
Wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga wa soko la Karume (Mchikichini) wameandamana hadi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kushinikiza kiongozi huyo atoe tamko la kuwaruhusu waendelee kufanya shughuli zao kwenye soko hilo.

Wafanyabiashara hao wameandamana leo Jumatatu Januari 17, 2022 ambapo walikuwa wanaimba "Tunataka Soko letu" wakiwa wamezingira geti la ofisi hiyo, ikiwa ni siku moja imepita tangu soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana.

Wakizungumza katika tukio hilo, baadhi ya wafanyabishara hao wamesema wanafanya hivyo baada ya kukosa imani na maamuzi yaliyochukuliwa na viongozi hao huku wakionyesha kusikitishwa kwao na kitendo cha wenzao kuvunjiwa mabanda yao waliyojenga usiku wa kuamkia leo na jeshi la polisi.

Silvanus Mwakipesile amesema Mkuu wa Mkoa aliwaahidi leo saa 2:00 asubuhi angefika kwenye soko hilo kuwaona na kuwapa muongozo lakini wanashangaa kabla ya kiongozi huyo kwenda kuna watu wamevunjiwa mabanda yao na sehemu hiyo kuwekwa chini ya ulinzi mkali ukisimamiwa na Jeshi la Polisi.

"Tumekosa imani na viongozi jana alisema anakuja lakini hadi sasa hatujamuona na chakushangaza waliojenga vibanda vyao wamebomolewa, sisi hatuwezi kuwasubiri wao maisha yetu magumu watuache tujenge wenyewe ili tuendelee kufanya kazi zetu," amesema

"Siku zilizotolewa kwa ajili ya kufanya uchunguzi ni nyingi tunataka tuachwe tujenge mabanda wakati uchunguzi ukiendelea na si kubaki hivihivi tutakula Nini na tunawatoto wanatakiwa kwenda shule,"amesema Saida Mohamed


Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija amewaomba wafanyabishara hao kuwa wavumilivu na kufuata utaratibu uliotangazwa na Serikali kwamba waiachie kamati ifanye kazi kwa siku saba na kutoa ripoti badala ya kuandamana kutaka kushindana na Serikali.

"Mnatakiwa kujiongeza pamoja na kwamba mnadai haki lakini lazima mfuate utaratibu Jana Waziri tuiachie Kamati ifanye kazi na walete ripoti tunaomba kuweni na subira,"amesema.

Jana baada ya soko hilo kuungua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla aliwataka wafanyabiasha wa soko hilo kuwa watulivu huku akiahidi kuundwa kamati ambayo itachunguza chanzo cha moto huo kwa siku 14 akipiga marufuku shughuli zozote kuendelea wakati wa uchunguzi huo.

Muda mfupi baada ya RC Makalla kutoa tamko hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa aliagiza kamati hiyo kufanya uchunguzi kwa siku saba badala ya 14.

Chanzo;- Mwananchi
Wamachinga Mlikataa Kuungana na CDM kuyang'oa Ma Nduli CCM Madarakani
Sasa mnavuna Mlichopanda
 
Dah! Vipigo vimeanza huko...mabomu na virungu vinatembea.
 
Apo Karume akuna machinga atarudi wakabanane gorofa zile za machinga complex na soko la ilala boma.
 
Wanadeserve wanachokipata kwa kuwa wakati CCM inapora chaguzi walikenua meno.

Watulia hivyo hivyo sindano iingie vizuri hadi watakapopata akili ya kuikataa CCM na mambo yake yote.

Nashukuru sana Mungu kuwa leo wamepelekewa askari wa kikosi cha mbwa ambao wameenda kubomoa vile vibanda vyao ambavyo walikuwa wameshaanza kuvijenga jana.
Nashauri hao Polisi waongezewe Nguvu na wanajeshi
 
Kuna watu niliwambia Magufuli aliitoa CCM, kitendo cha Watu kumuaga vile kwa uchungu ilikuwa ni mara ya mwisho Watanzania kuonewa na CCM.

Hawa wa Machinga watakuja kuvuka stage na watakuja kumuua au kumjeruhi Askari hapo Ndio Serikali itaanza kutumia nguvu excessive
 
Back
Top Bottom