Dar es Salaam: Vijana wawili wafariki mikononi mwa polisi

Dar es Salaam: Vijana wawili wafariki mikononi mwa polisi

Siku hizi kila mtu ana simu piga picha chukua video kwa siri hao vibaka wanaojiita askari tunawashtaki kwa mauwaji ya kutumia silaha kama walivyo bila kulihusisha jeshi la polisi
 
Tupe CV ya hao vijana Kwanza hapo mtaani, kuna wakati Polisi wanafanya maamuzi Sahihi Kwa Amani na usalama wa wanazengo.

Usikute hao walishashindikana hapo mtaani kwao RAIA wanacelebrety vifo vyao.
Rekodi za hao vijana zikoje?

Alafu vingunguti kipande hicho kina uhuni,usela mav sana huko watu wanakabwa asubuhi na mapema
Watu wakuona

Ova
Hata kama kweli walikuwa ni Wahalifu, hawakustahili kuuawa na Polisi kwa namna hiyo. Kwa kuwa tayari walishawatia mbaroni na walikuwa chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi, basi walitakiwa kufikishwa Mahakamani ili waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria za nchi. Aidha, Katiba yetu iliyopo bado haijafuta adhabu ya kifo, hivyo endapo kama hao vijana Wana makosa yanayostahili adhabu ya kifo, basi Jeshi la Polisi lilitakiwa kuwasilisha ushahidi usio na shaka Mahakamani ili watuhumiwa hao waweze kutiwa hatiani na mwishowe walitakiwa kunyongwa chini ya mfumo wa Mahakama baada ya tuhuma zao kuthibitishwa. Huu ndio utaratibu uliotakiwa na unaotakiwa kufuatwa na Jeshi la Polisi, lakini siyo kujitwalia Mamlaka mikononi mwao ya Kuua watu bila ya idhini ya Mahakama.
Kamwe, suala hili halikubaliki mahali popote pale, siyo duniani wala siyo mbinguni!
"Injustice somewhere is the threat to justice everywhere."( Martin Luther King Jr.)
 
Hata kama kweli walikuwa ni Wahalifu, hawakustahili kuuawa na Polisi kwa namna hiyo. Kwa kuwa tayari walishawatia mbaroni na walikuwa chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi, basi walitakiwa kufikishwa Mahakamani ili waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria za nchi.
Huu ni utaratibu wa miaka mingi unatumiwa na Polisi, ukisumbuwa Sana wanamalizana na wewe tu basi.

Tena hao ni Kwa sababu walichukuliwa wakionekana, ukifinywa kimyakimya hata maiti yako haitokaa ionekane.

Nyinyi hamjakutana na wahanga wa matukio ya kihalifu wengine wamebakwa mbele ya Baba zao kabisa.
 
Unawajuwa wahuni wa vingunguti lakini?
Hao hata wakienda jela hawakai wanarudi mtaani

Ova
 
Huu ni utaratibu wa miaka mingi unatumiwa na Polisi, ukisumbuwa Sana wanamalizana na wewe tu basi.

Tena hao ni Kwa sababu walichukuliwa wakionekana, ukifinywa kimyakimya hata maiti yako haitokaa ionekane.

Nyinyi hamjakutana na wahanga wa matukio ya kihalifu wengine wamebakwa mbele ya Baba zao kabisa.
Huko vingunguti watu wanakabwa asubuhi na mapema huku raia wakiangalia
Kipande hicho kuna watoto watukutu

Ova
 
Inasikitsha sana
R.I.E.P. Vijana
Na huko mkoani Kilimanjro,kijana mmoja aliyekuwa anashikiliwa kwenye kituo cha polisi cha Uru Mawella,Cornel Chuwa,amefariki dunia kwa kile polisi wanchodai alijinyonga akiwa mahabusu.

Hebu jiulize kama umewahi kuingia mahabusu yoyote hasa hizi za mijini,hakuna mahali mahabusu atatumia nguo yake kujinyonga,kwanza dali za mahabussu nyingi zimemiminwa zege kwa maana ya kuondoa uwezekano wa mahabusu kutumia nguo zake kunyonga.

Hii tabia ya polisi ;kuua ' na kusingizia mahabusu kajinyonga inaanza kuota mizizi na huko tuendako utakuwa sasa ni utamaduni wa mtu kufia mikononi mwa polisi na kuja na hadithi ya 'amejinyonga'akiwa mahabusu.

Afande RPC Maigwa,tolea kauli hili tukio maana familia imekataa kuzika ikisubiri majibu sahihi ya polisi na wewe ndiye msemaji wa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro,au ule usemi wako mkoa wa Kilimanjaro ni mkoa wa kimkakati bado unatembea nao?
 
Huu ni utaratibu wa miaka mingi unatumiwa na Polisi, ukisumbuwa Sana wanamalizana na wewe tu basi.

Tena hao ni Kwa sababu walichukuliwa wakionekana, ukifinywa kimyakimya hata maiti yako haitokaa ionekane.

Nyinyi hamjakutana na wahanga wa matukio ya kihalifu wengine wamebakwa mbele ya Baba zao kabisa.
Umma/wananchi wanawafahamu watu wahalifu ambao wamekuwa wakijihusisha na uhalifu mbaya dhidi yao, hao hata wakiuawa na Polisi huwezi kusikia malalamiko ya hovyo yasiyokuwa na msingi kutoka kwa wananchi. Kwa sababu wananchi wenyewe kwa wingi wao wanakuwa tayari wameshawachoka wahalifu hao, kwenye hili ninayo mifano mingi iliyo hai.
 
Tupe CV ya hao vijana Kwanza hapo mtaani, kuna wakati Polisi wanafanya maamuzi Sahihi Kwa Amani na usalama wa wanazengo.

Usikute hao walishashindikana hapo mtaani kwao RAIA wanacelebrety vifo vyao.
Polisi wanaruhusiwa kujichukulia sheria mkononi?
 
Back
Top Bottom