Dar es Salaam: Vijana wawili wafariki mikononi mwa polisi

Dar es Salaam: Vijana wawili wafariki mikononi mwa polisi

Wewe unaishi wapi Mkuu mpaka ushindwe kuijua hiyo Sheria!

Sio kila Sheria ipo kwenye Makaratasi.
Ndio nalisikia Leo kwamba si kila sheria iwepo kwenye makaratasi!

INashangaza, polisi wana protocoli zao ndio maana nikaomba unifundishe na mm kuonyesha hiyo sheria.
 
sisi hapa kibaha polisi walitimba na silaha baada ya kupigiwa simu na raia kuwa kuna jamaa amemjeruhi nduguye na mapanga, askari walitaka kumuwasha jamaa risasi ila walimbeba na kuondoka nae ila hatuna feedbacks mpaka sasa
Naweza kubaliana na wewe, ila umefika tu ajakataa hana siraha kauliza tu anapigwa risasi?

Labda bana.
 
Rekodi za hao vijana zikoje?

Alafu vingunguti kipande hicho kina uhuni,usela mav sana huko watu wanakabwa asubuhi na mapema
Watu wakuona

Ova
Napongeza walichofanya Polisi, mengine huwa ni mihemko ya Raia
 
Mmmhh!
Kumekucha tena na Polisi wa Tz!
Hivi janga hili kubwa zaidi lililopo hapa Tz la hawa wanaoitwa Jeshi la Polisi Tanzania litaisha lini????Litaisha kwa njia gani??
Nini kifanyike ili kuondokana kabisa na janga hili ??????????????
Leeni vijana wenu vizuri
 
Ukiwapeleka mahakamani hao wanakaa jela kwa muda, mwenendo wa Kesi raia hawaendi kutowa ushahidi mahakamai na Mahakama haiwezi kumuhukumu mtu pasipo na ushahidi usio na Shaka ndio unakuta wanaachiwa wanaendelea kusumbuwa RAIA mtaani.

Sasa ukiona Polisi wanakamata na kuuwa huwa msipende kuwalaumu Polisi hayo ndio maamuzi Sahihi Kwa mtu aliyekataa kustaarabika.

Lakini tuweke akiba ya maneno mpaka tupate wasifu wa kweli wa hao vijana hapo mtaani au nje ya mtaa, maana kuna wengine Wana kazi zao kabisa kama cover lakini ni majambazi hatari na Polisi wanawajuwa vizuri, unapoona Polisi wanakamata na kuuwa elewa wanawajuwa vizuri hao watu.
Hata jela hawakai, wanaishia mahabusu maana mashahidi hawajitokezi
 
Tupe CV ya hao vijana Kwanza hapo mtaani, kuna wakati Polisi wanafanya maamuzi Sahihi Kwa Amani na usalama wa wanazengo.

Usikute hao walishashindikana hapo mtaani kwao RAIA wanacelebrety vifo vyao.
jina kubwa akili hauna mkuu
 
kule sio kuzuri kabisa,..asubuhi na mapema unazungukwa unambiwa utoe kila ulichonacho sivo unaitiwa mwizi..
Hapafai kabisa kuna kijana wangu mmoja alikuwa anaishi huko walimkatakata sana
Na mpaka leo wamemuachia maalama usoni yaani mwili mzima,kwa hao waliiyouliwa huko
Humu watu wana mihemuko tu ila ukweli unajulikana
Na tatizo la wazazi/watu huko wanapenda sana kuwalinda/kulinda ,kuwaficha wahalifu
Watu huko ni wa ovyo kabisa

Ova
 
Leeni vijana wenu vizuri
Siyo watu wote ambao wamekuwa wakiuawa na Polisi hawakupata malezi mazuri kutoka kwa wazazi au walezi wao.
Je, yule kijana mfanyabiashara wa madini aliyeuliwa kinyama na Mapolisi kule Mtwara alikuwa hakulelewa vizuri??? Hamza Mohamed wa tukio la pale Selander Bridge naye alikuwa na malezi mabaya???Je, na wale wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge Morogoro waliouliwa vibaya sana na Kamanda Abdallah Zombe pamoja na Kamanda Christopher Bageni nao walipata malezi mabaya kutoka kwa walezi wao????
Polisi wanatakiwa kuwa weledi ktk kazi zao na waache mauaji ya kiholela, vile vile wazazi na walezi nao watimize wajibu wao wa kufanya malezi mema.
Tanzania bila ya Mauaji ya kiholela Inawezekana, kila mtu atimize wajibu wake. Wote kwa pamoja, raia na Mapolisi Tutii Sheria Bila Shuruti. Aidha, Polisi Wana Wajibu mkubwa zaidi wa kutii Sheria bila shuruti ili kutoa mifano hai kwa vitendo kwa raia wa kawaida.
 
Back
Top Bottom