Dar es Salaam: Vijana wawili wafariki mikononi mwa polisi

Arusha ndo balaa, vijana wanapewa vilema na kuuawa sana.

Kuna siku kidogo nidakwe aisee nilikimbia kidogo nigongwe na gari[emoji1787]

Eti nimekosea kuvuka barabara kidogo anigonge na defender yake akataka anipakize, kidogo nijikojolee

[emoji81] Pole sana Mkuu, Nime imagine the situation, nimeishia kucheka tu.
 
Police hawa hawa ndio wanasema tukiwa na mali yenye gharama kama madini au hela nyingi tuombe ulinzi kwao.
 
Arusha ndo balaa, vijana wanapewa vilema na kuuawa sana.

Kuna siku kidogo nidakwe aisee nilikimbia kidogo nigongwe na gari🤣

Eti nimekosea kuvuka barabara kidogo anigonge na defender yake akataka anipakize, kidogo nijikojolee
kumbe ndio ww siku ile ulikimbia

bahati yako maana tungekufinya kende 😂
 
Vijana wawili ambao ni Bakari Ismail (21) na Shomari Kacheuka maarufu Babuu (22) wamefariki dunia huku vifo vyao vikigubikwa na utata kwakuwa mara ya mwisho December 27,2023 walichukuliwa kwa nguvu nyumbani kwao Vingunguti Jijini Dar es salaam na Watu waliojitambulisha kuwa ni Askari na kisha kupelekwa kusikojulikana na baada ya Familia kuwatafuta bila mafanikio hatimaye December 28,2023 asubuhi miili yao ikafikishwa Amana Hospital na Watu waliojitambulisha ni Askari wakidai miili hiyo wameiokota.

Mzee Swalehe Kacheuka ambaye ni Baba Mzazi wa Shomari ameiambia @AyoTV_ kuwa “Babuu alikuwa anafanya kazi Kariakoo kampuni ya kuuza pikipiki, aliporudi kazini wakaja Wat waliojitambulisha ni Askari ila hawajavaa sare wakamsimamisha kwamba upo chini ya ulinzi akawauliza nimefanyaje wakawa wanabishana wakampiga risasi ya mguu, Kaka yake katoka wakamnyooshea bastola, akaja Rafiki yake Ismail wakati wanamkunja akasogea wakampiga risasi ya mguuni na wakawachukua wote wakaondoka nao, Ismail walimpakia kwenye IST, Bakari wakampakia kwenye Defender”

Kwa upande wake Mzazi wa Shemeji wa Bakari Ismail amesema “Tulipopata taarifa asubuhi December 28,2023 tukaamkia Polisi Buguruni tukaambiwa hawajaletwa, tukazunguka vituo vya polisi karibu sita hatukufanikiwa, tukazunguka Hospitali tukaambiwa hawajaletwa, mida ya saa 8 mchana tukaambiwa kuna miili Amana ambayo imepelekwa na Polisi wakisema wameowakota Vingunguti”

Familia hizo mbili zimesema miili ya Vijana hao imekutwa na matundu ya risasi na macho yao yametobelewa, Ayo TV imefanya jitihada za kulitafuta Jeshi la Polis Kanda Maalum ya Dar es salaam ili kupata taarifa zaidi kuhusu tukio hilo lakini hatujafanikiwa ingawa bado tunaendelea na jitihada za kuwatafuta.
View attachment 2857458

©MillardAyo
Hakuna polisi hapo, na kama wapo basi wahanfmga wana hatia.
 
Arusha ndo balaa, vijana wanapewa vilema na kuuawa sana.

Kuna siku kidogo nidakwe aisee nilikimbia kidogo nigongwe na gari[emoji1787]

Eti nimekosea kuvuka barabara kidogo anigonge na defender yake akataka anipakize, kidogo nijikojolee

[emoji23][emoji23][emoji23]
Yani wakubebe bila sababu ya msingi
Au mwenzetu una turasta twa kiduku kichwani

Pole sana lakini.
 
Ukiwapeleka mahakamani hao wanakaa jela kwa muda, mwenendo wa Kesi raia hawaendi kutowa ushahidi mahakamai na Mahakama haiwezi kumuhukumu mtu pasipo na ushahidi usio na Shaka ndio unakuta wanaachiwa wanaendelea kusumbuwa RAIA mtaani.

Sasa ukiona Polisi wanakamata na kuuwa huwa msipende kuwalaumu Polisi hayo ndio maamuzi Sahihi Kwa mtu aliyekataa kustaarabika.

Lakini tuweke akiba ya maneno mpaka tupate wasifu wa kweli wa hao vijana hapo mtaani au nje ya mtaa, maana kuna wengine Wana kazi zao kabisa kama cover lakini ni majambazi hatari na Polisi wanawajuwa vizuri, unapoona Polisi wanakamata na kuuwa elewa wanawajuwa vizuri hao watu.

Ulichokisema ni kweli, ila kwa mantiki hiyo polisi atakua hana tofauti na mhalifu.
Mpaka umepewa mafunzo ya kipolisi lazma kuwe kuna namna ya kupatikana ushahidi ili ahukumiwe kihalali.
Bas wavunje magereza ili wahalifu wakikamatwa wawe wanapigwa risasi chap chap wasipoteze muda.
 
Mpuuzi mkubwa utakuja kufirŵa wewe na kuuawa kama mbwa liwe fundisho kwa wengine.
Wanaume wakiwa kazini tuliza kijambio utakuja kufilimbwa.

Kwani ukisikia askari basi ni polisi tu?!

Tuwe na subira wakati tukisubiri taarifa kamili.
 
Weledi Ni pamoja na kutuondolea vibaka uraiani
Sitetei vibaka,ila sikubaliani na huu uhuni wa kuua watu hovyo na kutoboa macho Kisha kutelekeza miili bila maelezo yeyote....ni rahisi sana ikitokea Kwa mwenzio ila siku ukiguswa ndio utaelewa ninachozingumzia
 
Hata kama wangekuwa ndugu zangu au wanangu kama ni watukutu na wanawaumiza watu wengine basi ni heri wakutane na mkono wa chuma
Kweli we much know!umeshajua Kwa Nini hao vijana wameuwawa?
 
Tena wale watukutu wanawamaliza kimya kimya tu

Ova
Sitetei vibaka,ila sikubaliani na huu uhuni wa kuua watu hovyo na kutoboa macho Kisha kutelekeza miili bila maelezo yeyote....ni rahisi sana ikitokea Kwa mwenzio ila siku ukiguswa ndio utaelewa ninachozingumzia
Alichoelezea Joannah ndicho nilitaka nikujibu
 
Vijana wawili ambao ni Bakari Ismail (21) na Shomari Kacheuka maarufu Babuu (22) wamefariki dunia huku vifo vyao vikigubikwa na utata kwakuwa mara ya mwisho December 27,2023 walichukuliwa kwa nguvu nyumbani kwao Vingunguti Jijini Dar es salaam na Watu waliojitambulisha kuwa ni Askari na kisha kupelekwa kusikojulikana na baada ya Familia kuwatafuta bila mafanikio hatimaye December 28,2023 asubuhi miili yao ikafikishwa Amana Hospital na Watu waliojitambulisha ni Askari wakidai miili hiyo wameiokota.

Mzee Swalehe Kacheuka ambaye ni Baba Mzazi wa Shomari ameiambia @AyoTV_ kuwa “Babuu alikuwa anafanya kazi Kariakoo kampuni ya kuuza pikipiki, aliporudi kazini wakaja Wat waliojitambulisha ni Askari ila hawajavaa sare wakamsimamisha kwamba upo chini ya ulinzi akawauliza nimefanyaje wakawa wanabishana wakampiga risasi ya mguu, Kaka yake katoka wakamnyooshea bastola, akaja Rafiki yake Ismail wakati wanamkunja akasogea wakampiga risasi ya mguuni na wakawachukua wote wakaondoka nao, Ismail walimpakia kwenye IST, Bakari wakampakia kwenye Defender”

Kwa upande wake Mzazi wa Shemeji wa Bakari Ismail amesema “Tulipopata taarifa asubuhi December 28,2023 tukaamkia Polisi Buguruni tukaambiwa hawajaletwa, tukazunguka vituo vya polisi karibu sita hatukufanikiwa, tukazunguka Hospitali tukaambiwa hawajaletwa, mida ya saa 8 mchana tukaambiwa kuna miili Amana ambayo imepelekwa na Polisi wakisema wameowakota Vingunguti”

Familia hizo mbili zimesema miili ya Vijana hao imekutwa na matundu ya risasi na macho yao yametobelewa, Ayo TV imefanya jitihada za kulitafuta Jeshi la Polis Kanda Maalum ya Dar es salaam ili kupata taarifa zaidi kuhusu tukio hilo lakini hatujafanikiwa ingawa bado tunaendelea na jitihada za kuwatafuta.
View attachment 2857458

©MillardAyo
CHAI YA MAZIWA YA MOTOO
 
Tena wale watukutu wanawamaliza kimya kimya tu

Ova
Kuna mmoja mwaka wa 5 huu haonekani.
Ndugu wanaogopa hata kumwulizia.
Ye polisi ilikua nyumbani,na anawapa vitasa njia nzima.
 
Back
Top Bottom