Dar es Salaam: Vijana wawili wafariki mikononi mwa polisi

Dar es Salaam: Vijana wawili wafariki mikononi mwa polisi

Kuna kitu hakiko sawa hao vijana bila shaka walikuwa ni wahalifu wa muda mrefu
Make matukio ya hivyo yaliyo mengi yamekuwa yanatokea sana na mara nyingi wanaopotezwa ukifuatilia record zao zinatisha
 
Hata kama kweli walikuwa ni Wahalifu, hawakustahili kuuawa na Polisi kwa namna hiyo. Kwa kuwa tayari walishawatia mbaroni na walikuwa chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi, basi walitakiwa kufikishwa Mahakamani ili waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria za nchi. Aidha, Katiba yetu iliyopo bado haijafuta adhabu ya kifo, hivyo endapo kama hao vijana Wana makosa yanayostahili adhabu ya kifo, basi Jeshi la Polisi lilitakiwa kuwasilisha ushahidi usio na shaka Mahakamani ili watuhumiwa hao waweze kutiwa hatiani na mwishowe walitakiwa kunyongwa chini ya mfumo wa Mahakama baada ya tuhuma zao kuthibitishwa. Huu ndio utaratibu uliotakiwa na unaotakiwa kufuatwa na Jeshi la Polisi, lakini siyo kujitwalia Mamlaka mikononi mwao ya Kuua watu bila ya idhini ya Mahakama.
Kamwe, suala hili halikubaliki mahali popote pale, siyo duniani wala siyo mbinguni!
"Injustice somewhere is the threat to justice everywhere."( Martin Luther King Jr.)
Tulia kwanza ww .
 
Tupe CV ya hao vijana Kwanza hapo mtaani, kuna wakati Polisi wanafanya maamuzi Sahihi Kwa Amani na usalama wa wanazengo.

Usikute hao walishashindikana hapo mtaani kwao RAIA wanacelebrety vifo vyao.
Unajua maana ya utawala wa sheria? Kama polisi wakiendelea kuwaua raia kihuni hivi na wananchi wenye hasira nao wakawaiga nchi hii itakalika? Usishabikie upumbavu mkuu.
 
Tupe CV ya hao vijana Kwanza hapo mtaani, kuna wakati Polisi wanafanya maamuzi Sahihi Kwa Amani na usalama wa wanazengo.

Usikute hao walishashindikana hapo mtaani kwao RAIA wanacelebrety vifo vyao.
Ili tubadilike na maendeleo mengine yafuatane lazima utawala wa Sheria uheshimiwe.

Ni kweli walikua wameshindikana ila tukiruhusu Askari aamue yupi kashindikana na yupi hajashindikana tunajitengenezea mazingira hata siku wewe binafsi Askari anaweza akaamua wewe umeshindikana na akakuua.

Jeshi letu la polisi ni waelewa sana na asilimia nyingi ya Askari wanapenda kusuluhisha matatizo yetu Kwa amani na kupatana bila kutumia nguvu zao ambazo wanazo,nawapongeza Kwa hilo.

Ila tukiruhusu Askari aamue yeye binafsi yupi wa kumpoteza na yupi wa kumsamehe ukijumlisha na masuala binafsi(most criminals wanasumbua sana Askari,wanapewa ushauri na ultimatum ila wanakaidi) Itafika sehemu Askari wa kawaida tu anaamua Kwa maamuzi yake kukupoteza sababu ulimkera na kumsumbua na alikua anakutafuta Kwa muda mrefu. hata Kwa faida yetu ila tusiruhusu kila kitu watu Fulani waamue hatma yetu hasa ya UHAI wetu.
 
PoliCCM wamefanya yao tena? Hivi hawa mbwa ni lini wataacha kuwaua raia wasiokuwa na hatia?
Wanaume wakiwa kazini tuliza kijambio utakuja kufilimbwa.

Kwani ukisikia askari basi ni polisi tu?!

Tuwe na subira wakati tukisubiri taarifa kamili.
 
Tupe CV ya hao vijana Kwanza hapo mtaani, kuna wakati Polisi wanafanya maamuzi Sahihi Kwa Amani na usalama wa wanazengo.

Usikute hao walishashindikana hapo mtaani kwao RAIA wanacelebrety vifo vyao.
Ndio waue Kwa staili hiyo? Je kama ni visasi au visa vya wake za watu n.k?
 
Bastola Bei gani hapo Tanganyika arms?
 
Aiseee yaani Askari anaruhusiwa kupiga raia amabaye hana silaha kwa sababu tu amehoji?

Tutafika tu, hali ilishakuwa mbaya!
sisi hapa kibaha polisi walitimba na silaha baada ya kupigiwa simu na raia kuwa kuna jamaa amemjeruhi nduguye na mapanga, askari walitaka kumuwasha jamaa risasi ila walimbeba na kuondoka nae ila hatuna feedbacks mpaka sasa
 
Back
Top Bottom