Dar: Flyover ya Mfugale yazinduliwa. Chang'ombe na Gerezani kujengwa flyover, Barabara njia 8 kujengwa Kimara hadi Kibaha

Rais Magufuli anaanza hotuba yake kwa kuwapa pole Watanzania wote kwa msiba wa kitaIfa kwa ajali ya meli huko mwanza. Anaongoza sala ya kimya kwa dakika moja. anaendelea kwa kuwaasa watanzania kuwa makini na matumizi ya vyombo vya usafiri ili kuepusha vifo.anaKumbusha kuhusu tukio la leo la uzinduzi wa flyover ya tazara.

Anawapongeza wazabuni na mafundi wa daraja hili kwa kumaliza ujenzi wa daraja hili ndani ya muda. anashukuru japan kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha ujenzi wa daraja hili
 
hii ni asante wafadhili..
huyu wizard weka ukuta unaohitaji kufunguliwa atakuja ila msiba ukitokea hata uwe wa mamia ya watanzania kupoteza maisha hutomuona..
 

Tunatakiwa tuwe na policy ya nchi kila mahali, policy ya nchi huandaliwa na wataalamu waliobobea, policy ya nchi katika kila uwanja itaandaliwa na wataalamu wa uwanja husika na itakuwa na time frame. Hii itasaidia kila Rais anayeingia ajue anaanzia wapi na nini cha kufanya baadala ya kila anayekuja kuja na yakwake kichwani mwisho wa siku tunalima nusu nusu.
 
eeh ikawaje sasa
 
Ngoja nione kama JPM atatambua mchango wa JK
Kama atatambua sawa na asipotambua ni sawa.lkn ni upotoshaji kusema huu mradi kajenga jk. Ukiingia kwenye ilani ya ccm kuna barabara nyingi sana zinatakiwa zifanyiwe kazi, so kiongoz anayekuja lzm apite humohumo akitaka kudeal na ishu za barabara na labda ka kuna mabadiriko kdg lkn sio naye aanze upya akitoka yy naye mwenzie akija aanze upya.Mtaani kwetu kuna mpango wa kujenga barabara kutokea gongo la mboto na huu mpango haujaanza leo lkn siku ukianza kujengwa huwez sema aliyejenga ahusiki. Kupanga au kuweka mikataba hakusaidii kitu kama hakuna utekelezaji.

Hapo ilipo mitambo ya kinyerezi hilo eneo ni la kitambo sana,tulikua tunaambiwa tu kuna mitambo itawekwa itawekwa, ndo huku mwishoni kabisa jk ndio akajenga kinyerezi one na magufuli kaongeza kinyerezi 2.Sasa leo ukisema kinyerezi yote ni mradi wa jk na jpm ahusiki sijui ka utakua sahihi.
 
Uko sahihi mkuu,lkn kwa hili liko kwenye ilani ya ccm 2015/20.Kuna dira inayomuongoza jpm licha ya kweli mengine hayafuati.Kuna miradi tayar imeshasanifiwa na kazi ya jpm ni kuanza na imeorodheshwa, kuna miradi jk kaiacha nusu na jpm anatakiwa aendeleze na huku kuendeleza maana yake kutoa msaada wa hali na mali kama inavyofanyika Airport, kinyerezi au mloganzila na kuna miradi jpm anatakiwa afanye usanifu. Haya yote yapo ktk ilani.Ingekua ajabu jpm ashindwe kuendeleza Airport kisa kaacha jk na nimetoa mfano Malawi ndio wanasiasa za kishenzi ka hizi.
 
Unazungumzia ilani wakati haina back up ya kisheria?Niambie mpango wa miaka mitano ambapo usipofuatwa sheria inawabana!

Halafu nashangaa unapolinganisha ilani na mkataba,once ukisaini mkataba basi kuuvunja kuna gharama zake!Ndio maana bomberdier yetu ilikamtwa kwa kuvunja mkataba kinyemela!
Mkataba ulisainiwa 2015,na kwa mujibu wa mkataba huo ndio maana leo waziri anasema kazi imekwenda na kumalizika ndani ya mkataba!
 
Mbona kikwete hasifiwi katika, hizi salamu kama mwanzilishi wa mradi?
Mi nadhani Kikwete aliridhika na sifa alizopata ndio maana akaachia madaraka. Kama angekuwa anahitaji kuendelea kupta sifa basi angebadili katiba ili aendelee kuongoza. Hata kama Kikwete aliomba pesa na Magufuli akakamilisha huo mradi basi Magufuri anastahili pongezi zaidi, inawezekana ulikuwa mdogo huko nyuma kuna rais alipewa hela kwa ajri ya ujenzi wa daraja la Mkapa, hela zikaja wakati yeye ametoka madarakani na rais aliyeopo akazitumia zile hela kufanya uchaguzi wa serikari za mitaa. Sasa hapo nadhani utaelewa kwanini Magufuri anastahili pongezi
 
Inaitwa exchange bridge,
 
Vizur umeongelea kwenda ndan ya mkataba, lkn kuna mazingira mradi unaweza usiende ndan ya mkataba. Miradi mingap ya serikali haikamiliki ndan ya mda uliopangwa na shida huwa ni nn?Unataka kusema jk alitoa pesa zote za flyover?
 
Hahahahaha nimecheka hapo kwenye TMA
 
Vizur umeongelea kwenda ndan ya mkataba, lkn kuna mazingira mradi unaweza usiende ndan ya mkataba. Miradi mingap ya serikali haikamiliki ndan ya mda uliopangwa na shida huwa ni nn?Unataka kusema jk alitoa pesa zote za flyover?
Basi mkuu,sifa zote ziende kwa JPM!
 
Mmeshasahau jinsi mlivyomuita JK Vasco da Gama mbembeaji.
Of course he was as you have described, but there are some issues to comprehend! alikuwa dhaifu sana, tena sana... lakini hakuwa dictator, hakuua watu, hakuna miili iliyookotwa Coco beach, Hakuna Ben Saanane, hakuna Mawazo etc.
 
Of course he was as you have described, but there are some issues to comprehend! alikuwa dhaifu sana, tena sana... lakini hakuwa dictator, hakuua watu, hakuna miili iliyookotwa Coco beach, Hakuna Ben Saanane, hakuna Mawazo etc.
Mwangosi,mauaji Arusha, ulimboka, kibamba haya yalitokea China. Bora uwe MCHAWI KULIKO MNAFKI.
 

Mkuu unaposema dira ya CCM tayari kwangu naona ni makosa, maana wakija CDM au CUF nao watakuja na dira zao and what about dira ya CCM binafsi nafikiri tuache kuwaza hizi dira za vyama. Mpango wote wa maendeleo mkubwa unaodetermine future ya nchi uwe ni dira ya nchi ili tukiongozwa na CCM/CUF/CDM waufuate na lazima itambulike kwa vyombo vyetu vyote ikiwemo TISS na JWTZ ili mtu akiweka yakwake hao wasimame upande wa Raia/Wananchi.

Mfano tunahitaji 2030 tuwe na 10000MW za umeme, mikakati na njia za kuifikia hiyo 10000MW ibaki kuwa dira ya nchi na sio dira ya chama na lazima wataalamu wawe wamekaa na kuamua hilo na sio makada wa chama fulani kwa kujifurahisha. Mradi kama wa Airport uwe kwenye dira ya nchi baada ya wataalamu kukaa na kuonyesha mahitaji kitaalamu. Pia vyama na viambiwe Dira ya nchi ni nini na dira ya chama ni nini. Binafsi kazi ya chama ibaki kuwa juhudi za kuanganisha watu na kutafuta fedha za kutufikisha huko, chama kikishindwa kutufikisha sehemu fulani baada ya miaka mitano hasa kwenye zile dira ambazo ni short term tunakihukumu kwenye box la kura..
 
Niko na Chadema hapa tunasikiliza hotuba ya mheshimiwa wamenuna kwelikweli naona hawajapenda haya mafanikio wamebaki wakisema siyo flyover ila ni daraja ilimradi ni kuponda tu yaani wananongwa kwelikweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…