Dar: Flyover ya Mfugale yazinduliwa. Chang'ombe na Gerezani kujengwa flyover, Barabara njia 8 kujengwa Kimara hadi Kibaha

Dar: Flyover ya Mfugale yazinduliwa. Chang'ombe na Gerezani kujengwa flyover, Barabara njia 8 kujengwa Kimara hadi Kibaha

Wengi tulikuwepo pale TAZARA leo katika ufunguzi wa Flyover, daraja lilopewa jina la Eng Patrick Kipilimba Mfugale.

Pamoja na utani mwingi wa Rais, lakini ametuonyesha upande wa shilingi ambao watendaji wengi wa serikali wanapitia lakini umma hauuoni.
Kati ya sifa alizo mwagiwa Eng Mfugale:
1. Amebuni na kusimamia madaraja mengi nchini

2.Ni mwadilifu na amewahi kusimamishwa kazi kwa kutetea ukweli na akavumilia manyanyaso ya bosi wake. Mwenzake ambaye hakuweza kuvumilia alijipiga risasi.
3. Ni mchapa kazi, alisanifu (draft) daraja la Umoja linalounganisha Tz na Msumbiji ndani ya siku tatu.
(Na bado siku ya ufunguzi daraja hilo wala hakutajwa hadi Waziri wakati huo J Magufuli alipomtaja hadharani kwa marabya kwanza)

4. Akiwa Mkuu wa TANROADS kasimamia ujenzi wa maelfunya kilometa zikiwemo 9,000 kiwango cha lami.

Hapo nilipokuwa nimekaa, wananchi walianza kutikisa vichwa na wengine kujisemea, kuwa kweli Tanzania tuna watu wanafanya kazi kwa moyo.


Kwa upande wa wahandisi namshukuru mh. Magufuli kwa kumuinua Eng Patrick Mfugale na kuitambua fani ya Uhandisi.
Fani ya Uhandisi ikitumika vyema na kwa uadilifu kama alivyo fanya Eng Patrick Mfugale, basi nchi itapata maendelto chanya.
Hakika kamtendea haki,wengi tulikua hatumfahamu kiundani
 
Una uhakika kama mimi napata tabu,pumbavu kabisa wewe.
Hujui wanachofanyiwa watumishi wa umma.
Tatizo linalowakabili nyinyi watumishi wa umma ambao mlikosa uadilifu na weledi katika kutumikia Watanzania ni kwamba mlizoea WIZI na kupiga Dili kwa Kuhujumu Mali ya Umma. Mshahara sio tatizo...kwa sababu kuna watumishi wa umma walioishi kwa weledi na kutumikia Taifa kwa nidhamu mbona wanachapa kazi na kuendesha maisha yao bila matusi, kejeli, chuki, ukanda n.k!
Awamu hii Majizi mtapata TABU SANA. Mtalia na kusaga meno kwa kujificha mgongoni kwa Watumishi wa Umma.
 
Mnatapatapa sana. Mradi umeanza kujengwa 2016 na serikali inayoongozwa na jpm.jpm alikua na uwezo wa kupiga chini mipango yote ya jk lkn hana upumbavu ambao mnauonesha humu.Kama kaachana na mradi wa gesi na kaingia wa maji alishindwa nn kuachana na flyover?
Muongo mradi huu umeanza mwaka 2008,wamesema wenyewe wewe unakuja na pambio za kwaya.
 
Na lile kwamba alisimamishwa kazi kwa kutetea uadilifu na kukataa kuingizwa katika kuchota mali ya umma, limewagusa wengi.
Mh Magufuli kasema wazi , alipewa deski na kwa muda mrefu akawa anasoma magazeti tu.
Mkuu story ile inatia simanzi sana,siku zote dunia hii ukiwa muadilifu kuna hatari ya kuishia kupotezwa na manya'ng'au
 
Rais John Magufuli ameagiza kufungwa kamera katika daraja la juu ‘flyover’ la Mfugale lililopo eneo la Tazara lifungwe kamera ili kuwabaini watu watakaokiuka taratibu za usalama barabarani.
Mbali na daraja hilo, pia ameagiza madaraja mengine makubwa yanayojengwa nchini kufungwa kamera.
Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 27, 2018 wakati akizindua daraja hilo.



“Ili hata pale anapokuja mtu amelewa na kusababisha ajali tumjue ni nani hata kama atatelekeza gari lake hapo,” amesema.
“Tutengeneze vitu vizuri vitusaidie na si kutuletea matatizo mengine ambayo yanaweza kuzuilika.”
Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametaka miradi yote ya ujenzi inayosimamiwa na DMDP iwekwe chini ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura).


“Tarura ilipitishwa na Bunge hatuwezi kuwa na chombo kingine kinachojitegemea wakati tulishakubaliana. Hivyo barabara, madaraja, mifereji inayojengwa yote iwe chini ya Tarura,” amesema.


“Na lengo la kufanya hivi ni kutaka kuhakikisha fedha zote zinazoelekezwa katika miradi zinatumika ipasvyo.”
 
Tuache utani camera zilishindwa kubaini watu waliompiga mbunge risasi huko dodoma sembuse kubaini wanaokunya na kukojoa kwenye mitaro,

We are not serious,
Watu wasiojulikana wakiulia hapo kwenye daraja kamera zitafunguliwa kama kawaida
 
Tunaomba vibaka wetu mjiandae kutuibia tufunge majumbani kwetu za Kwa lissu zimetosha
 
Back
Top Bottom