Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Ulilolisema ni sahihi kabisa, 80% ya marafiki zangu, majirani zangu I mean age mates wangu wanaishi majumbani kwao. Home Kijitonyama washkaji wengi wanafanya kazi lakini hawajatoka kwenye nyumba za wazazi. Ila nilichogundua ni pamoja na kuwepo kwa space, na wengine wanaambiwa na wazazi wao wenyewe kwanini unataka kupanga wakati vyumba nyumbani vipo?
Hii ilinitokea hata mimi kabla sijahamishiwa kikazi mkoani, mama haukutaka nikapange kabisa maana madogo wote wapo mikoani kikazi.
 
Hawa vijana muwaonee huruma wana stress sana wengi hawapendi kubaki kwao wanalazimika

Kuna vijana tangu wamalize vyuo hawana mishe za maana hivyo hata kwenda kupanga anaona kodi zitamtesa na akizingatia kwao kuna vyumba/chumba

Wengi unakuta walisoma seko mpaka chuo ila hawana ujuzi wowote wa VETA wanategemea magamba yao ya vyuo. Mitaji ya biashara hawana familia maisha ya kuungaunga.

Wengine wamejiongeza kuwa boda au winga K/koo, udalali n.k

Wanaumia sana wanapoona wenzao waliosoma nao wakiwa wana mishe. Wao wakiamka asuhuhi hawajui waende wapi

Tusiwaseme sana vijana wa Dar ila wanachopitia Mungu mwenyewe anajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…