Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Hawa vijana muwaonee huruma wana stress sana wengi hawapendi kubaki kwao wanalazimika

Kuna vijana tangu wamalize vyuo hawana mishe za maana hivyo hata kwenda kupanga anaona kodi zitamtesa na akizingatia kwao kuna vyumba/chumba

Wengi unakuta walisoma seko mpaka chuo ila hawana ujuzi wowote wa VETA wanategemea magamba yao ya vyuo. Mitaji ya biashara hawana familia maisha ya kuungaunga.

Wengine wamejiongeza kuwa boda au winga K/koo, udalali n.k

Wanaumia sana wanapoona wenzao waliosoma nao wakiwa wana mishe. Wao wakiamka asuhuhi hawajui waende wapi

Tusiwaseme sana vijana wa Dar ila wanachopitia Mungu mwenyewe anajua
hayo mengine yanaeleweka ila kuzalia nyumbani ni tatizo
 
hayo mengine yanaeleweka ila kuzalia nyumbani ni tatizo
Hili suala la kuzalia nyumbani ni pana kidogo

Utakuta kijana wazazi wake wanempa chumba cha uani aendelee na maisha yake ajipange mdogomdogo. Wengine wanaamua kuvuta kabisa wanawake wa kufanya nao maisha na kuwazalisha hapohapo kwao. Au anamtia mimba binti wa watu inabidi aanze kuishi naye hapohapo

Wengine ndio hivyo katia mimba binti wa watu ambaye naye maisha yao choka mbaya. Bibi upande wa baba anaamua kuishi na mjukuu wake na kijana naye humohumo katika visa fulani hadi mama ya mtoto naye anaishi hapohapo

Kuna life fulani Dar unaweza kusema ni kama watu wanaigiza kumbe ndo maisha halisi yanaenda hivyo
 
Habari zenu,

Mjanja M1 nimeona maeneo mengi Dar vijana wenye umri mkubwa miaka 30 na kuendelea wakiishi kwa wazazi wao na wengine kuzalia makwao.

Kautafiti kangu kamegundua zaidi kuwa kuna wanaume waliooa pia ambao wanaishi na wake zao kwenye nyumba za wazazi wao.

Vijana wengi wa Dar wameshakata tamaa ya kujenga makazi yao binafsi, wengi wanategemea cha wazazi eg. Nyumba, Magari n.k

Utafiti wangu pia umegundua kuwa kuna vijana wanaojitegemea lakini maisha yao hayapo vizuri kwani kesho yao imekuwa ngumu kueleweka, na mara nyingi utakuta kijana anaishi kwenye nyumba za kupanga na bado kodi ya pango inamsumbua kulipia.

Vijana hawa wenye umri mkubwa hawana future iliyobora maana kuna uwezekano kwenye uzee wao wakawa wanaishi maisha ya tabu kwa kukosa makazi yao binafsi.

USHAURI - NAOMBA SERIKALI IONGEZE NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA, NA PIA IONDOE VIKWAZO VINGI KWA WANAOFANYA BIASHARA.

NB. HUU NI UTAFITI WANGU KAMA MJANJA M1, KAMA UTAUPINGA BASI UTAKUWA SAHIHI PIA.

Written by Mjanja M1.
Kwani ilani ya CCM inasemaje kuhusu hili suala mtambuka
 
Vjana

Vijana wengi wazawa wa dar wanawaza kuzamia tu bondeni kwa madiba😀😀😀😀
 
Kweli ndivyo ilivyo, ila hii inachangiwa na kitu kimoja....
Vijana wa mikoani wamezoea hustle na kuna umri ukifika wao husema wanaenda kutafuta maisha hivyo huamia mikoa na kujikuta wanaondoka nyumbani rasmi, Kwa Dar iko tofauti unatokaje Dar unaenda kutafuta maisha mkoani?
Kumbe kama huwezi tafuta maisha Mkoani Toka kwenu tafuta hapo hapo.

Mnakutana na Akina baba legelege na malofa,kukutimua?
 
Back
Top Bottom