Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Siwezi kwenda kupanga wakati nyumba ya wazazi ipo apo nitaendelea kukaa huku najipanga nawasaidia na wazazi nikitoka apo naenda ktl kibanda changu
 
Unajua bro inategemea unajiwekaje hapo nyumbani.
Ukiwa kijana wa hovyo,dira hauna,direction ya maisha hauna hata mawazo chanya ya kimaisha hauna pia hata kupambana haupambani wazee wakifungua mlango wanaweza ona beberu kalala kitandani kumbe kijana wao Moses.
Ila ukiwa una malengo yako na unayatimiza na pia unai handle familia pale inapohitajika kwa familia zetu hizi waonekana mtu wa umuhimu ni ngumu wao kukuruhusu utoke home.
Mimi mpaka naoa nimeoa niko nyumbani.
kama wazazi wako wako happy kukaa nyumbani sawa, familia zetu hizi wazazi wakikuona unakaa kwao wanaanza kukusimanga na kukunyanyasa, inabidi uhame tu kwa lazima
 
Habari zenu,

Mjanja M1 nimeona maeneo mengi Dar vijana wenye umri mkubwa miaka 30 na kuendelea wakiishi kwa wazazi wao na wengine kuzalia makwao.

Kautafiti kangu kamegundua zaidi kuwa kuna wanaume waliooa pia ambao wanaishi na wake zao kwenye nyumba za wazazi wao.

Vijana wengi wa Dar wameshakata tamaa ya kujenga makazi yao binafsi, wengi wanategemea cha wazazi eg. Nyumba, Magari n.k

Utafiti wangu pia umegundua kuwa kuna vijana wanaojitegemea lakini maisha yao hayapo vizuri kwani kesho yao imekuwa ngumu kueleweka, na mara nyingi utakuta kijana anaishi kwenye nyumba za kupanga na bado kodi ya pango inamsumbua kulipia.

Vijana hawa wenye umri mkubwa hawana future iliyobora maana kuna uwezekano kwenye uzee wao wakawa wanaishi maisha ya tabu kwa kukosa makazi yao binafsi.

USHAURI - NAOMBA SERIKALI IONGEZE NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA, NA PIA IONDOE VIKWAZO VINGI KWA WANAOFANYA BIASHARA.

NB. HUU NI UTAFITI WANGU KAMA MJANJA M1, KAMA UTAUPINGA BASI UTAKUWA SAHIHI PIA.

Written by Mjanja M1.
''USHAURI - NAOMBA SERIKALI IONGEZE NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA, NA PIA IONDOE VIKWAZO VINGI KWA WANAOFANYA BIASHARA.''
Ushauri uliotoa ni ushauri wa ''typically Tanzanian mindset''. i.e ufinyu wa kujua tatizo letu na suluhisho lake.
 
Milion nane ni bei ya kiwanja huku kijijini kwetu,
Hiko kiwanja kina ukubwa gani?
Maana hiko cha mil 8 ni cha futi 10 kwa 15.Tena rural area huko kama unaelekea Kisarawe 2 ama Pemba mnazi.
Aya hicho cha mil 8 kijijini kwenu heka ngapi na eneo la urban ama rural?
 
Habari zenu,

Mjanja M1 nimeona maeneo mengi Dar vijana wenye umri mkubwa miaka 30 na kuendelea wakiishi kwa wazazi wao na wengine kuzalia makwao.

Kautafiti kangu kamegundua zaidi kuwa kuna wanaume waliooa pia ambao wanaishi na wake zao kwenye nyumba za wazazi wao.

Vijana wengi wa Dar wameshakata tamaa ya kujenga makazi yao binafsi, wengi wanategemea cha wazazi eg. Nyumba, Magari n.k

Utafiti wangu pia umegundua kuwa kuna vijana wanaojitegemea lakini maisha yao hayapo vizuri kwani kesho yao imekuwa ngumu kueleweka, na mara nyingi utakuta kijana anaishi kwenye nyumba za kupanga na bado kodi ya pango inamsumbua kulipia.

Vijana hawa wenye umri mkubwa hawana future iliyobora maana kuna uwezekano kwenye uzee wao wakawa wanaishi maisha ya tabu kwa kukosa makazi yao binafsi.

USHAURI - NAOMBA SERIKALI IONGEZE NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA, NA PIA IONDOE VIKWAZO VINGI KWA WANAOFANYA BIASHARA.

NB. HUU NI UTAFITI WANGU KAMA MJANJA M1, KAMA UTAUPINGA BASI UTAKUWA SAHIHI PIA.

Written by Mjanja M1.
Sio Dar tu ni Tanzania ukiacha kwa wamasai na kule wanakojenga nyumba za tembe
 
Back
Top Bottom