Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

Mwamba kutoka kanda ya Kati,

Twende tumechelewa sana , muda ni mchache.

Huku NEC CCM, Huku Polisi CCM, Huku IGP Sirro,Huku Mambo leo ,Huku Nyahoza ,Kule Pole pole ili mradi ni matamko tu yasiyo na Kichwa wala Miguu.

Ngoma inogire,Twende Mwamba muda ni mchache.
 
Mkuu huwa naheshimu sana michango yako. Tatizo mnaegemea upande mmoja kuwalaumu watanzania kuwa ni waoga. Upande wa pili ni aina ya wagombea mnaowaleta. Kuna tatizo kubwa kwa Mgombea wa CHADEMA, kutokana na Lissu kupigwa risasi, zile hasira Kuna watu amewahusisha na wapo front kwenye kuusaka uraisi ambao ni tishio kwa ustawi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Tatizo linaanzia njia alizojaribu kutumia Lissu kuusaka uraisi haziwezi kufanya kazi nchi hii(nakuhakikishia). Hii sio Malawi,Zambia au Mali hii ni Tanzania. Na wengi mna underestimate system ya Tanzania. Sio ya mchezo mchezo kiongozi.
 
Kuna kipindi watu tumeshauri hapa..kwa wema tu kwamba Tundu Antipasy Lissu..kabla hajasmama kumwita aidha kumhoji ama kumshitaki ama kumuuliza maswali lazma ukae chini utafakar. Huyu ni mgombea anaijua anachosmamia...Katika jambo ambalo Polisi wamekwepa mtego mkubwa wa kudharilika ni huu. Maana Wangepata tabu kumhoji...mana "system ya answer by Question "ingewatoa kwenye line...wangemwongezea umaarufu mkubwa mwishowe wangejikuta wanalaumiwa na HP mwenezi. Hongera polisi kwa kulitafakar hili . mjue tu wagombea wote wakishinda ni Tanzania itakua imeshinda..tendeni haki Bila upendeleo Tafadhar sana!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Hata kina mange walikuwa Hivi,,



Leo hii wako wapi?
 
Kama kweli ka withdraw, huyo ndiye Siro halisi wa Mwanza enzi hizo. Huwa anazo busara, basi tu CCM hubemenda raia wema.

lissu anapaswa ajue sio kila mtu ni wa kumuona mjinga.

lazima atumie watu humu humu ndani ya serikali kuwaonyesha ccm kwamba hana tatizo na watu ambao wanajitambua.

kitendo cha kuita askari wajinga halafu wako nyuma yako wengine na unadai ni watu miongoni mwa unao waomba kura,hii nayo ni bangi.
 
Mkuu
Nakumbuka Hosni Mubarak na Elbashir walikuwa na wapambe wao kama ww, ila sasa hivi wapambe wao wote wana vusukari maana hawaamini wanachokiona.
Mkuu hii sio Misri wala Tunisia, hii ni Tanzania. Bado siku 25 tu.
 
Hahahaha wanajitekenya na kucheka kwenyewe
 
Bado polisi inabidi wa angaliwe kwa macho 4 maana hawaja wahi kuwa waungwana ata siku moja
 
Kajinyonge!
 
bro shetani akikusemesha"tumsifu yesu kristo"
kemea kwa ukali.

usishangilie kwamba sasa ameokoka.
Kwa mokorokoro niliyoyaona kwenye hii issue ya Lissu ni hatuna jeshi la polisi ambalo linaweza kumfanya kitu Lissu:

1.Lissu amefanya kosa Moshi akaandikiwa barua kuwa aripoti Dar.Hakuna sheria ya namna hiyo

2.Aliefanya kosa ni Lissu ila barua ikaandikwa kwa chadema

3.Barua ilikuwa na kiwango cha chekechea("chana cha democrasia")

Ni vyema jeshi la polisi likaguliwe vyeti kuanzia IGP
 
Wamekubali kuwa sisi ni juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…