Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

Mambosasa: Polisi tumesitisha kumuita Tundu Lissu, tunamtaka aendelee na Kampeni zake

Baada ya mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, kukataa kuitikia wito uliotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, uliotolewa jana ukimtaka aripoti kituo cha Polisi Kilimanjaro.

Lissu kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa ataendelea na ratiba zake ikiwemo kikao cha mabalozi kinachofanyika leo.

“Wito wa polisi sio barua ya kirafiki ni amri kisheria, wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama, huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria, nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho” ameandika Lissu kupitia kaunti yake ya Twitter.

Kwa mujibu ya barua iliyotumwa kwa Mwenyekiti wake wa Chama, Freeman Mbowe, Lissu alitakiwa kuripoti polisi 02/10/2020 kwa ajili ya mahojiano kufuatia kauli na matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa kwenye mikutano yake ya kampeni dhidi ya maafisa wa polisi.
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

View attachment 1587836
Video ya maelezo ya kamanda wa kanda maalum Lazaro Mambosasa akithibitisha kusitisha wito wa kumtaka Tundu Lissu kuripoti kwa jeshi hilo kanda ya Dar es Salaam
View attachment 1587905

Saf sanaaa jiwe apo atalalamika sanaa
 
Kwa mokorokoro niliyoyaona kwenye hii issue ya Lissu ni hatuna jeshi la polisi ambalo linaweza kumfanya kitu chochote Lissu

1.Lissu amefanya kosa Moshi akaandikiwa barua kuwa aripoti Dar.Hakuna sheria ya namna hiyo

2.Aliefanya kosa ni Lissu ila barua ikaandikwa kwa chadema

3.Barua ilikuwa na kiwango cha chekechea("chana cha democrasia")View attachment 1587961View attachment 1587962View attachment 1587963

kimsingi jeshi la polisi halina mamlaka ya kumfanya mtu kitu chochote,sio kwa sababu huyo ni lissu.

kitendo cha jeshi la polisi kukuita halafu ukachukulia kwanini uitwe hii ni kutokujiamini au uoga.

lissu ni mjuvi wa sheria,ilipaswa aende halafu akawathibitishie kwamba wao ni vilaza hawana la kumfanya.akatumia sheria kufanya uhuni wa watoto watukutu wanaosoma.
 
Mambosasa: Polisi tumesitisha kumuita Tundu Lissu, tunamtaka aendelee na Kampeni zake

Baada ya mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, kukataa kuitikia wito uliotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, uliotolewa jana ukimtaka aripoti kituo cha Polisi Kilimanjaro.

Lissu kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa ataendelea na ratiba zake ikiwemo kikao cha mabalozi kinachofanyika leo.

“Wito wa polisi sio barua ya kirafiki ni amri kisheria, wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama, huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria, nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho” ameandika Lissu kupitia kaunti yake ya Twitter.

Kwa mujibu ya barua iliyotumwa kwa Mwenyekiti wake wa Chama, Freeman Mbowe, Lissu alitakiwa kuripoti polisi 02/10/2020 kwa ajili ya mahojiano kufuatia kauli na matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa kwenye mikutano yake ya kampeni dhidi ya maafisa wa polisi.
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

View attachment 1587836
Video ya maelezo ya kamanda wa kanda maalum Lazaro Mambosasa akithibitisha kusitisha wito wa kumtaka Tundu Lissu kuripoti kwa jeshi hilo kanda ya Dar es Salaam
View attachment 1587905

Sijaona dunia hii kama kuna MTU anaweza mshinda lissu kwenye sheria never never twende na lissu
 
Ujanja uko kwenye box la kura ndugu!

Na binafsi nlishauri hawa polisi waachane na Lisu afanye chochote anachotaka maana pia ni tiba kwake kwa yaliyomsibu.

Wakati mwingine Lisu anapata point za bure kwa mihemuko ya polisi tu.

Mtu inajulikana hawezi kushinda, yanini kuhangaika nae?
Umegeuka mshauri tena? Si hapo juu umekana hii barua ukaiona feki. Kwanini usingeshauri jana?

Na utazidi kuchanganyikiwa tu mpka kufikia oct 28!!
 
Maguli anapaswa kuwa makini na Polisi pamoja na Tume kwenye uchaguzi huu. Wote hawa wanaweza kumaliza umaarufu wake kabisa na akajikuta anashindwa uchaguzi

Tunisia mmachinga mmoja aliamua kujichoma moto hadharani baada ya kunyanyaswa na polisi nchi nzima ikachafuka na Rais akang'olewa. Naona dalili za mfuasi au wafuasi wa CHADEMA kufanya tukio la aina hii kama polisi watajaribu kumnyanyasa Lissu wakati huu wa kampeni.

Rais Magufuli aelewe hujuma sio kugomea amri tu, inaweza kuwa kuitekeleza amri vibaya na kimakosa ili kuleta tafrani. House girl mmoja alikuwa akilaumiwa kuwa chakula hakina chumvi wala mafuta na bosi wake mnyanyasaji watoto wa bosi hawakupenda manyanyaso yale.

Kesho yake mtoto mpendwa wa bosi akaambiwa apike alichofanya akajaza mafuta na chumvi kwenye chakula kama namna ya kumtetea na kuonyesha hisia zake dhidi ya unyanyasaji wa house girl.

Sasa juzi tume wametoa wito kwa Tundu Lissu unaoonyesha dhahiri upendeleo na Lissu akaugomea wito ule. Hakuna kilichotokea. Polisi wametoa wito kwa Lissu jana na Lissu amegoma polisi wamefuta wito wenyewe. Sasa wananchi waliokuwa waoga wanaondoa hofu maelfu kwa maelfu. Hawa wanaotoa wito usioeleweka je wanatumwa au wanajituma? Je hawakuona mapungufu katika wito wao? Au wanatekeleza vibaya maelekezo ili kumhujumu mtoa maelekezo?

Kuna video ya msafara wa mgombea mwenza Salum Mwalim ukipigwa mabomu. Video imerekodiwa toka ndani ya gari la polisi na unawasikia askari wakibishana kuwa kwanini unawaelekezea watu bomu? Huenda aliyekuwa anawaelekezea wananchi bomu alitaka litokee kama lile la Mwandishi Mwangosi kule Nyololo ili mambo yaharibike.

Magufuli anaweza kushinda kwa kishindo asipotumia nguvu. Watanzania kwa asili yao hawampendi mtu mbabe. Ukiwa mbabe jamii ya Watanzania inakutenga
 
lissu anapaswa ajue sio kila mtu ni wa kumuona mjinga.

lazima atumie watu humu humu ndani ya serikali kuwaonyesha ccm kwamba hana tatizo na watu ambao wanajitambua.

kitendo cha kuita askari wajinga halafu wako nyuma yako wengine na unadai ni watu miongoni mwa unao waomba kura,hii nayo ni bangi.
Kwenda zako huko
 
kimsingi jeshi la polisi halina mamlaka ya kumfanya mtu kitu chochote,sio kwa sababu huyo ni lissu.

kitendo cha jeshi la polisi kukuita halafu ukachukulia kwanini uitwe hii ni kutokujiamini au uoga.

lissu ni mjuvi wa sheria,ilipaswa aende halafu akawathibitishie kwamba wao ni vilaza hawana la kumfanya.akatumia sheria kufanya uhuni wa watoto watukutu wanaosoma.
Kwa nini mtu akuite kinyume na sheria uende wakati ratiba ya kampeni ni very tight na shughuli ni nyingi?!Kwani ukitaka kuonyesha kuwa mtu ni kilaza lazima uende alipo physically?
 
Magu urais ni wake hawezi kuhamgaikia kupoteza rasimali za bure!

Acha Lisu akomae ili angalau aje apate 20%

Sasa kama ndivyo si angetulia tu kule Ikulu aendelee kula wale Bata Mzinga apmoja na kiharufu flan amaizing cha Feri ili ausubirie huo Ushindi !?
 
Hilo kanusho au ubatilishaji wa maamuzi ulipaswa utolewe na IGP Siro mwenyewe ingependeza.

Kufokeana sio kuzuri, kuna mgombea anatufokea sana lakini haguswi.

Lisu hata akipiga chafya anatakiwa alipoti polisi.
 
Hahahaha wanajitekenya na kucheka kwenyewe
[emoji1782][emoji1782][emoji1782]
JamiiForums-931025076.jpg
 
Isije ikawa ni fake. Maana amri katoa Sirro usitishaji atamke Mambosasa. Hii imekaaje?

Itakuwa ni fake

Kwasababu Siro angeona amejidhalilisha mwenyewe kwa kutoa amri kwa mbwembwe halafu atoke tena hadharani ale maneno yake. Ndio maana amemtuma mtu mwingine aseme kuficha aibu yake.
 
Polisi mmeonesha weledi wa hali ya juu...hatutaki mtu alete visingizio,uchaguzi huu Lisu ndio atajua CCM ndio Dingi wa siasa za nchi hii.

JPM ANATOSHA
CCM USHINDI NI JADI

Mmeishiwa na kubaki na vimaneno maneno hivi hivi kila wkaati.
 
Mkuu huwa naheshimu sana michango yako. Tatizo mnaegemea upande mmoja kuwalaumu watanzania kuwa ni waoga. Upande wa pili ni aina ya wagombea mnaowaleta. Kuna tatizo kubwa kwa Mgombea wa CHADEMA, kutokana na Lissu kupigwa risasi, zile hasira Kuna watu amewahusisha na wapo front kwenye kuusaka uraisi ambao ni tishio kwa ustawi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Tatizo linaanzia njia alizojaribu kutumia Lissu kuusaka uraisi haziwezi kufanya kazi nchi hii(nakuhakikishia). Hii sio Malawi,Zambia au Mali hii ni Tanzania. Na wengi mna underestimate system ya Tanzania. Sio ya mchezo mchezo kiongozi.

Imebidi nicheke sana, kuwa naegemea upande mmoja, hivi ww kwa michango yako uko neutral? Tatizo la wagombea tunaowaleta ni lipi ukiacha lile zee tapeli lililotoka ccm uchaguzi uliopita?

Au unataka mgombea wa CDM afurahishe na kukidhi matakwa ya hilo kundi unaloliita system? Mtu yoyote anapotaka kuuwawa ni lazima atakuwa na chuki, na hao anaowahusisha ndio hao hao. Tuna akili zetu timamu za kuweza kuutambua ukweli.

Hakuna mtu yoyote anaye underestimate system ya Tanzania, ila hiyo system unayoisema inaonekana ni kikundi cha wala nchi fulani ambao wana maslahi binafsi na ccm. Usitegemee sisi wapinzani tutakuwa na muda wa kumpitisha mgombea anayekubalika na kikundi cha watu wanaojiita system.

Tufupishe maneno, tunataka mshindi wa halali na sio anayetakiwa na hiyo uiitayo system, kinyume na hapo kutatokea msuguano usio wa lazima ambao utagharimu taifa letu.

CCM sio chama cha kizazi hiki, hiyo system inapaswa kusoma alama za nyakati. Tumeomba tume huru ya uchaguzi, hiyo system iko kimya, acha tutumie njia nyingine maana ni nadra watawala wa kiafrika kukubali mabadiliko bila misuguano.
 
Back
Top Bottom