Dar: Kuna Tatizo la watu Homa na Mafua, Wizara ya Afya ipo kimyaa..

Dar: Kuna Tatizo la watu Homa na Mafua, Wizara ya Afya ipo kimyaa..

byakunu

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
583
Reaction score
1,318
Takribani kwa muda wa wiki moja tangu tarehe 10 Desemba 2021, kumekuwa na wimbi kubwa sana la watu wakaazi wa Dar es Salaam, wamekumbwa na hali ya homa sambamba na kupata mafua na kikohozi,

kila mtu analalamika kwa namna yake, Mimi juzi nimekumbwa na hii homa nikahisi nina malaria ila ni kwamba kila ninae kutana nae analalamika kikohozi na mafua. Waziri wa Afya upo? mbona haukuoni? mbona hatukusikii?
 
Piga chanjo mkuu...maradhi mengine Kama haya, kinga za mwili zenye utayari zitapambana nayo.
 
Nilikotoka watu kibao tunaumwa tena wengine wakienda pima hawakutwi na ugonjwa. Mama alikuwa anaumwa ila yeye kakutwa na malaria. Kila mtu analalamika kivyake mimi mwenyewe niko hapa nipate dawa maana usiku hali inakuwa tete
IMG_20211216_155408.jpg
 
Acha uchochezi.

Kwanza ingekuwa ni covid macron kila mji dar ingekuwa na msiba.

Haya ni mabadiliko ya hali ya hewa. Tumepigwa Jua muda mrefu ghafla mvua kubwa lazima makoo yayumbe.
kuna uchochezi wowote umeuona hapo? kwahiyo tukiumwa homa watu kumi tukaushe tusiseme
?
 
Kusema kila mtu Dar anaumwa mafua ni Uongo sema baadhi huko kwenu

Umewapima saa ngapi watu wote Dar kuwa wanaumwa mafua? Mleta mada muongo wa kutupwa
kwenye uzi wangu "kila mtu" ndo ina ukakasi ni kweli, mniwie radhi. Ila haiondoi uhalali wa content kufanyiwa utafiti. Asilimia kubwa ya watu nilio kutana nao wote wana same case, same scenario.
 
Hahahaaaa. Mkopo wa korona mmechukua halafu mkaujengea madarasa kutafuta sifa kwa wananchi. Sijui mtawaambia nini mabwana zenu..
 
Back
Top Bottom