Dar: Kuna Tatizo la watu Homa na Mafua, Wizara ya Afya ipo kimyaa..

Kwakweli ata mimi leo nipo hovyo ila homa sina napigwa na joto kali,kichwa kinaniuma sana na viungo vinauma sana
aisee ni hatari,mi leo ndio nimepata nafuu kidogo, yaan joto la mwili lilikuwa juu mnoo, kichwa kinauma Hadi nilihisi labda nimerogwa, viungo vinauma Ni balaa, halafu siwanasemaga sisi wenye damu group O ni ngumu kupata hivi vimalazi vidogo dogo,

Hila hii huenda Ni Corona mpya,

Kwa Hali niliyokuwanayo siku tatu nyuma, Kama ndio ingekuwa mtu mwenye ngoma ,aisee Ni msiba
 
Mara ngapi mumeambiwa mchukue tahadhari mnakaidi na kudharau?

Wakati fulani Waziri alienda hadi kituo cha daladala na sokoni akakuta watu hawana barakoa wala hawana sanitaiza au maji na mbaya zaidi hawajachanja.

Sasa kuleni jeuri yenu.
 
Ndugu unaishi wapi? Mbona wizara umeshatoa maelezo Leo na kwenye gazeti la mwananchi wametoa ufafanuzi almost page nzima????
 
Mnaozungumzia chanjo zikitoka zile life time kama za surua sijui ndui mnijulishe nikachome

Binafsi kuumwa mafua ni kawaida kwangu haswa kama nitatumia pafyumu yenye harufu kali, nikivuta moshi wa sigara/nikikaa karibu na mvutaji, vumbi, shuka chafu( hapa nimejikuta nikiwa na shuka nyingi kama nguo za kuvaa ), baridi au nikinywa maji ya baridi sana yanayoumiza koo


Huwa napona ndani ya siku tatu

Narudia tena, ZIKITOKA CHANJO PERMANENT MNIJULISHE NIKACHOME, SIO KILA SIKU KINATOKA KIRUSI KIPYA NA KUTAKIWA KWENDA KUCHOMA TENA CHANJO MWILI SI UTAKUA NA VITOBO VITOBO VYA SINDANO KAMA CHEKECHE LA MASHINE YA KUSAGA NAFAKA
 
Hata mimi sijachoma na siumwi hicho kilichoandikwa na nipo Dar, kutwa nzima nashinda kariakoo kwenye msongamano wa watu narudi home saa tatu au nne usiku
Hongera mkuu
 
Acha uchochezi.

Kwanza ingekuwa ni covid macron kila mji dar ingekuwa na msiba.

Haya ni mabadiliko ya hali ya hewa. Tumepigwa Jua muda mrefu ghafla mvua kubwa lazima makoo yayumbe.
Mimi niko safarini lakini naona homa ya Dar imenifata hadi huku Tanga
 
Acha uchochezi.

Kwanza ingekuwa ni covid macron kila mji dar ingekuwa na msiba.

Haya ni mabadiliko ya hali ya hewa. Tumepigwa Jua muda mrefu ghafla mvua kubwa lazima makoo yayumbe.
ndivyo ninavyofikiria hata mimi, leo siku ya pili nasikilizia hali ikifika siku ya nne bado sijakaa sawa nitalazimika kutembelea kilingeni!!
 
Mwenyewe nilisafiri kutoka mwanza kuja shinyanga imenikuta huku homa sio homa, kichwa kinauma kwa mbali, mafua na viungo vinauma sanasana shingo. Nlidhani labda kwasababu ya gesti kuacha ac wazi.. kumbe hii ishu inaweza kua mambo mengine
 
Mimi nlikuwa naumwa kichwa sana natoka jasho then mwili unatetemeka hadi goose bumps ,ni kama ni sensor za mwili zilikata mawasiliano yan ilikua balaa, nikajihisi nimepata ngoma aisee, nilipanic saana kwasababu sio homa ambayo nimewahi ipata it's something new
 
Ndugu unaishi wapi? Mbona wizara umeshatoa maelezo Leo na kwenye gazeti la mwananchi wametoa ufafanuzi almost page nzima????
Sio wote tunasoma magazeti. Ishu burning kama hii sio ya kuandika kwenye magazeti tuu na kutulia. Enzi za mwenda zake mambo hayakuwa bubu hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…