DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Dr mpango huna ubavu wa kupambana na mtoto wa malaika........
Nasema utapataaa taaaabuuu sanaaa dr mpango
 
Anaweza onesha mapenzi ya kweli kwa bashite na aka mfire mpango kwa kumtaftia sababu hata ambayo si sababu.

Mfano, unaamini magulu alitumbuliwa eti kwa sababu haendi misibani na hatoi salam za pole?

Si ndii huo unafiki wenyewe tunaosema? Huyu ni msema kweli kama anavyojiita mwenyewe, sasa hapa kuna uvunjaji wa sheria na aliyevunja sheria bado anatoa vitisho, je anayetishiwa atalindwa au ndio safar inamngoja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasubiri Mkuu aongee,ninaamini mmoja kati ya hawa wawili lazima apewe madongo ya kutosha
 
Dk Mpango angeonesha njia kwa kununua angalau kontena moja kuthibitisha kwamba yeye haogopi vitisho vya kulaaniwa yeye na uzao wake.
Mwisho wa siku hizo fanicha zitaozea hapo bandarini wakose wote!
Zikiozea hapo basi ni kuwa watu hawaoni umuhimu wa kununua na siyo kuogopa laana. Mtu yeyote anayetaka kununua na akawa anaogopa laana namba ani PM mimi nimsaidie kununua bila hofu yoyote ili mradi fedha ziwe zake.
 
Na hili halipo sawa hata kidogo! Nilitarajia awe ameshaiacha ofisi ya umma mara moja kwani yeye ndiye msimamizi na mhimizaji mkuu wa watu kulipa kodi katika mkoa wake! Na hii ya yeye kutaka asamehewe ndiyo iliyoishusha mkoa wake katika makusanyo ya kodi hadi kuzidiwa na Dodoma! Sasa wananchi anaowaongoza na kuwahimiza kulipa kodi si nao watataka msamaha na kukimbilia madhabahuni kuomba Mungu awalaani wanaonunua mizigo yao waliyoshindwa kuilipia? Mteuzi amtungue tu kwani siyo mfano mwema kwa anaowaongoza na kavunja sheria kwa nafasi yake! Nitazidi kushangaa akiachwa kwenye nafasi hiyo!
Na mimi basi nipunguziwe kodi ninayolipa kila mwezi au niende madhabahuni!
 
Lakini mwenzenu au sijaelewa vizuri: makontena yameingia nchini kutoka diaspora wa Marekani ....huu si ndio ule msaada kwa ajili ya shule zetu kutoka kwa ndugu zetu wa nje? Sheria inataka kodi hata kwenye misaada ya kijamii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo ni moto. Twendeni kuchukua vitu kwa bei Rahisi
 
Back
Top Bottom