Wanazingua tu ni movi wanatufanyia ili serikali ionekane inatenda haki kwa watu wote lkini in fact hayo makontena hayatanunuliwa na atakayenunua ni mtu maalum aliyepangwa kwa kiini macho tu.
Kamani movie, ni ujinga zaidi.
Nikama mama na baba watengeneze ugomvi wa uongo, wawaoneshe watoto wanapigana kwa sababu wanawapenda watoto.
Ile heshimainayovunjwa kwa haowazazi kuwaonesha watoto wanapigana itakuwa na madhara makubwa kulikofaida itakayoletwa kuonesha wazazi wanapigana kwa sababu wanawapenda watoto.
Wazazi hata wakipigana, wanatakiwa wapigane chumbani huko, watoto wasiwaone wanavyopigana.
Viongozi ni watu, watakuwa na tofauti, watalumbana, hilo halinamjadala.
Ila, viongozi bora watawezakulumbana kwenye vikao, behind closed doors, wakija ku present vitu kwa watu, wanakuwa washamaliza tofauti zao, au hata kama zipoi, haziwi exposed kwenye public.
Uongozi ni kazi ya imani. Imani ya wananchi kuwamini hawa viongozikwamba wanaweza kazi ya kuongoza watiu.
Viongozi kulumbana lumbana kijinga,kunatupa picha wananchi kwamba "kumbe hawa hata wao kwa wao wenyewe waliokaribu katika uongozi hawawezi kusikilizana, wataweza vipi kutuongoza sisi tulio mbali na uongozi?"