DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Sasa Makonda anamiliki shule?!..mpaka aagize Madawati.
KWANI AKIVYOTANGAZA WTUMIA MADAWA YA KULEVYA ALIKUA POLISI. Wakati wenye kaz yao wapo wanaijua fika kwa nini asiwatumie hao au KUTAKA MISIFA TU
 
Kwenye majina yake ni pa kuchunguza, anaweza hasiwe na nia mbaya, ila kutaka sifa ionekane ni makonda kafanya
Sheria huwa haina kitu kinachoitwa 'nia nzuri, vinginevyo watu wangeiba na kusema nia ilikuwa kuwasomesha watoto
 
KWANI AKIVYOTANGAZA WTUMIA MADAWA YA KULEVYA ALIKUA POLISI. Wakati wenye kaz yao wapo wanaijua fika kwa nini asiwatumie hao au KUTAKA MISIFA TU
Ndio kapelekea kuudws kwa taasisi ya kupambana na madawa haramu ya kulevya.
 
Anyway Makonda is here to stay,mtake msitake chuki za wanabavicha dhidi mkuu wa mkoa wa Dar hazitofanya chochote mimi nataka apewe wizara ya mambo ya ndani kabisa ili awanyooshe vizuri.
 
Ndio kapelekea kuudws kwa taasisi ya kupambana na madawa haramu ya kulevya.
Mshauri kaka yako kwenye ksaidia jamii asitangulize jina MBELE ni hatarii kisiasa mana fursa hii kila mtu anaiwinda. We utabaki kulaan wenzio wakifaidika na MUNGU HATIMIZ/Ihazingatii LAANA ZA KIJINGA
 
Anyway Makonda is here to stay,mtake msitake chuki za wanabavicha dhidi mkuu wa mkoa wa Dar hazitofanya chochote mimi nataka apewe wizara ya mambo ya ndani kabisa ili awanyooshe vizuri.
KHEE.. bav wameingiaje hapa! huku huko. tena punguzen kuomba omba post kaka yako tulivyopokea Dreamliner akaomba LIVE post ya polepole masikini bila aibu hadharan. Nahisi kuna dawa yenu inachemka
 
Dah huu mjadara wa RC makonda na mh mpango mbona siulewi kabisa , aliyemteua rc makonda kuwa Rc ni nani ?? Na aliyemteua Dr mpango kuwa wazir wa fedha nani???! Kama aliyewateuwa ni MTU mmoja basi huyo ndo kusema hivyo vifaa visamehewe au vitozwe kodi , ikiwa Rc makonda anawalaumu anaowaita " wanamkwamisha " na Dr mpango pia anamlaumu RC makonda kwa vijembe basi warudi kwa aliyewateuwa tu hizi movie za kama kuna mwajiri wa makonda tofauti na mwajir wa Dr mpango basi acha movie iendeleee tu ???

Sent using Jamii Forums mobile app
MWIGULU alishindwa kumshughulikia huyu wacha huyu amnyooshe hata raia anafurahi ndio maana kauchuna. dogo ametoka nje ya line sio wa kubebwa kila wakat
 
Anyway Makonda is here to stay,mtake msitake chuki za wanabavicha dhidi mkuu wa mkoa wa Dar hazitofanya chochote mimi nataka apewe wizara ya mambo ya ndani kabisa ili awanyooshe vizuri.
Ni vizuri akalipe kodi. Nawe utaonyesha busara kama utasaidia kumshauri Prince Makonda aachane lugha za kitoto kwenye maswala ya msingi. Kuna kesho na keshokutwa Mfalme Jiwe hatokuwa kwenye kiti cha enzi. Kama aliishazoea dharau basi anahitaji msaada wa kisaikolojia haraka, kwani itakuja kuwa taabu sana hasa baada ya wapambe wasiyokauka miguuni, nao watakapo mkimbia. Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania tusichambue mambo kwa hisia, hasa hili la makonteina ya Makonda. Kwanza kabisa, sheria ni sheria. Je Watanzania tunakumbuka TFF walivyopata shida kupewa msamaha wa kodi kwa ajili ya majani ya uwanja WA TAIFA? Na hayo majani yaliagizwa na serikali kwa jina la taasisi ya serikali. Sasa sembuse Makonda kuagiza vitu kwa jina lake!

Tunapaswa kuelewa kwamba ikiwa Makonda ataruhusiwa kutoa haya makontaina bila msamaha, yanatoka kama mali za Makonda. Atakuwa na uhuru wa kuyapeleka anakotaka, kuzigawia shule au mtu anaetaka, akisimamia huo ugawaji yeye mwenyewe. Hakutakuwa na udhibiti wowote wa serikali juu ya mali ndani ya makontaina hayo ziligawanywaje. Hilo ni suala la Makonda. Serikali haitakuwa na haki ya kuingilia wala kuweka ukaguzi wa aina yeyote, na wala Makonda hatatakiwa kuyahifadhi makontaina kwenye ghala yeyote ya serikali ili yangizwe kwenye leja ya serikali, kwa sababu ni mali za ya Makonda ambaye amekuwa mkarimu wa kusaidia shule.

Sasa upande wa serikali, ambayo haitakiwi kufanya kazi kwa hisia, suala linakuwa kwamba, unajuaje kama Makonda angewakilisha vifaa vyote kwa ajili ya shule, kama vifaa hivyo havina udhibiti wowote wa serikali kwa kuwa vimeagizwa na MAKONDA kama mtu binafsi?

Angalau basi kama Makonda angekuwa ni taasisi ya NGO basi angetakiwa kujieleza aligawaje zile mali, tena kwa kiasi fulani tu. Lakini kama Makonda hawajibiki kujieleza zile bidhaa za Bilioni 2 aligawa vipi, kama akiruhusiwa kuyachukua makontaina bila kulipia kodi. Kumbuka akiruhusiwa kuyataoa bila kodi, akajigawia sehemu ya mali hizo, huwezi kumshitaki popote pale.

Lakini mtasema ana nia nzuri. Sawa hatukatai, lakini ndio hapo tusiamue mambo kwa hisia. Jiulize, hivi kweli Makonda ni mtakatifu kiasi hicho, vitu vya Tshs bilioni 2 vije kwa jina lake, asishawishike angalau kujiwekea pembeni vitu vya bilioni moja wakati hakuna udhibiti wowote wa serikali wa hivyo vitu? Huyu Makonda akiangusha noti ya Tshs 1000 hataiokota kwa kuwa ameridhika kiasi hicho, kiasi alete bidhaa za Bilioni 2 na asiminye hata kidogo?

Ni wazi serikali inajiuliza, Makonda hapo alipo ana hela kiasi gani asishawishke kunufaika binafsi chini ya kivuli cha "vifaa vya shule" ambavyo havina udhibiti wa serikali? Mie sijawahi kuona Mtanzania mwenye uaminifu kiasi hicho, zaidi ya Nyerere na Sokoine!

Ukiwa waziri, unapopewa taarifa, unatumia na akili zako mwenyewe kujua nini cha kufanya. Kama Makonda ana uchungu na shule, basi atafute namna ya kukabidhi vifaa hivyo kwa serikali ili ndio iwe na jukumu la kuvigawa kwa shule kama mali ya serikali iliyoingizwa kwenye leja ya serikali. Bado lengo lake litakuwa limetimia. Na kwa nini hakufanya hivyo tangu mwanzo? Jiulize kwa nini mwanzoni alikataa katakata kuwa sio yake wala hana habari nayo? Kwa nini alitaka yaingie kimya kimya? Na yangeingia kimya kimya, nani angejua kuwa Makonda kaagiza vitu vya bilioni 2 lakini kagawa vitu vya milioni kumi tu kwa shule mbili au tatu? Sidhani tumefikia hatua ya kuaminiana kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom