DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Huwa tunapoteza sana talents kwa sababu ya roho mbaya tulizonazo.

Mbwana Samatta asingekuwa na utulivu kichwani asingefika alipofika kirahisi tu. Angekatishwa tamaa na uswahili wetu.

Wale wachezaji wa Ufaransa wenye asili ya Afrika waliobeba kombe la dunia kule Moscow, wasingekuwa na msaada wowote ule kama wangekuwa wanachezea mataifa ya Baba zao.

Tuna matatizo sana sisi watu weusi, hakuna jema ambalo linaweza kufanyika na tukakiri kwamba hili jambo ni jema, sana sana tutakiri kinafiki yaani usoni tu na sio moyoni.
 
Kwa hiyo Bashite hata akimchapa kofi Mteule wa rais hadharani hatamtumbua?

Kuna watu wanarisk maisha yao kupambana na ujambazi na magenge hatari au kuiweka nchi salama lakini wanakuwa na nidhamu. Kazi zao siyo kinga ya kufanya upuuzi kwa hoja kuwa mamlaka za juu yao zitawavumilia!

Bashite kama anapendwa sana basi apangiwe kazi nyingine, kama anampenda sana apewe jimbo akagombee, kisha atangazwe na Mkurugenzi, baada ya hapo amtoe Kasimu amuweke yeye!. Naamini kwa cheo kama cha Kasimu atakuwa na ulinzi mzuri zaidi au vipi?
Huna habari ndiko aelekeapo

Jimbo la Ukonga linamngoja 2020



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya lile sakata la makontena kati ya mkuu wa mkoa wa Dar na waziri wa fedha,wananchi kila kona walisema,na wakatabiri Makonda kufutwa kazi lakini mpaka dakika hii bado hajafutwa kazi na anaendelea kuwa mkuu wa mkoa

Siku za hivi karibuni Makonda amelaumiwa na Rais hadharani kuwa mkoa wake umeshuka kimapato na madiwani wanalipana posho mara mbili hata hivyo Rais hakuona sababu za kumuondoa nafasi hiyo kwa kosa tajwa

Wangekuwa watendaji au viongozi wengine wamefanya makosa mfululizo wangekuwa wameisha tumbuliwa zamani na wananchi wangekuwa wamesahau lakini kwa Makonda ni tofauti ,kumbuka kisa cha DED Bukoba ,kusahau kiasi cha fedha tu akatumbuliwa sembuse Makonda anapambana na serikali yake mwenyewe lakini hatumbuliwi

Sababu hizi hapa

Ishu ya Makonda kupambana na madawa ya kulevya ilimfanya awe na maadui kila kona na hata kuongezewa ulinzi na serikali

Inafahamika duniani ukishaingia katika harakati za kupambana na madawa ya kulevya basi maisha yako huwa yapo hatarini hivyo Rais anaona dhahiri kuwa akimfuta Makonda kazi basi atakuwa amewapa tiketi ya kuuawa kwa Makonda

Sio siri tena Makonda ana maadui kila kona baada ya sakata la madawa hivyo Rais anamhurumia sana

Ni swali la kujiuliza baada ya Magufuli kumaliza muda wake na Rais mwingine akaingia madarakani na asipomteua makonda kuendelea kuwa mkuu wa kitengo fulani ili aendelee kulindwa je,atakimbia nchi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kudanganya watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi wamezoea kutulisha matango pori mchana kweupe na sie hatuna neno kabisa, tukishavimbiwa masikini wanatupa dawa ya maumivu.. Naipenda nchi yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebu tujiulize thamani ya mchango wake kwa mkoa wa Dsm, unalingana na udhaifu wa makontena aliyoleta? Inawezekana hatupati muda wakuona uzuri wake, tunajikita zaidi kwenye udhaifu wa ufanyaji wake kazi, ebu jamani kama wanadamu tunamakosa mengi kila mtu anayakwake lakini pia tujipe nafasi ya kupima mabaya na mazuri yake, kila mtu ana mapungufu. Jambo la makontena nilakiutawala zaidi watumishi Wa umma njia wanayotumia kulumbana siyo sahihi Makonda ni mkuu wa mkoa kumbuka yenye ndiyo mlinzi wa Bandari anamadaraka kuliko waziri ki mkoa bandari ni tasisi iliyochini ya ulinzi wake alikuwa nanafasi yakumaliza hayamambo ofisini kwake hata kwa kumwita waziri wakamaliza bila maneno, Haya mambo hatuna budi kuwakumbusha watendaji wetu kushirikiana katika kufanya maamuzi.
 
Sababu ingine ni kwamba; Mkuu wa Mkoa wa Dar ndio Mlinzi wa Mali za Rais aliyeko Madarakani.
 
Huwa tunapoteza sana talents kwa sababu ya roho mbaya tulizonazo.

Mbwana Samatta asingekuwa na utulivu kichwani asingefika alipofika kirahisi tu. Angekatishwa tamaa na uswahili wetu.

Wale wachezaji wa Ufaransa wenye asili ya Afrika waliobeba kombe la dunia kule Moscow, wasingekuwa na msaada wowote ule kama wangekuwa wanachezea mataifa ya Baba zao.

Tuna matatizo sana sisi watu weusi, hakuna jema ambalo linaweza kufanyika na tukakiri kwamba hili jambo ni jema, sana sana tutakiri kinafiki yaani usoni tu na sio moyoni.
Kweli kabisa hujakosea mkuu. Nchi za kiafrika zina viongozi wahovyo sana ndiyo maana waafrika wakienda nchi nyingine hufanikiwa sana. Tena waafrika wanaona radhi kuwa zimamoto huko Ufaransa kuliko mwanajeshi Afrika...Afrika ina ombwe kubwa sana la uongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini kibaya zaidi ambacho watu hawakioni ni kwamba, hizi laana na lawama anazozirusha kwa serikali inaleta picha kwamba haifuati wala kuheshimu taratibu.

Ni kandamizi na ya kibabe. Hivi kweli wahusika wa Forodha, TPA na mawaziri wameshindwa kabisa kuelewa kwamba hivyo vitu vinaenda kusaidia watoto? Hiyo ndio picha tunayoipata kwamba anaonewa, lakini Je, ni kweli anaonewa?
Mkuu umezisoma hoja za Dr. Mpango katika barua aliyomjijibu Mh. Paul Makonda juu ya ombi lake la kutaka kupewa msamaha wa kodi wa mzigo huo?

Je katika barua hiyo umeusoma vizuri ushauri alioutoa Dr. Mpango kwa Mh. Makonda ili Mzigo huo apate Tax execemption?

Je kwa nini Mh. Makonda hakufata ushauri huo aliopewa toka May mapaka leo.

Sheria ni sheria tu. Kama tunashindwa kusimamia sheria ndogo kama hizi tulizojiwekea, vipi sheria katika maswala makubwa?
 
Hivi sasa sakata la makontena ya Makonda limefikia patamu, baada ya Musiba kutamka wazi kuwa angekuwa na mamlaka yeye angeyachukua jumla na siyo kuyapiga mnada!

Amempongeza waziri wa fedha Dr Mpango kwa kusimamia sheria na kubainisha kuwa nchi ina mihimili mitatu na inafanya kazi bila kuingiliwa!

Hivyo amemtaka Makonda kulipa kodi ya hayo makontena, ambapo inaelezwa kuwa makontena hayo yamebeba samani za ofisi za shule lakini kwa nyepesi nyepesi ni kuwa kilichopo ndani ni samani za hotel na viti na meza chache za ofisi zilizowekwa kama geresha tu.

Amesema makontena hayo ni zaidi ya 800...!

Ngoja huu mtanange tuuone Musiba Vs Makonda.


huyu naye utadhani ni naibu waziri wa mkulu yaan yeye ni kukurupuka tu kutafuta kiki,nahc bado ana uhayawani wa utototni mwake hajapona vzr,kizuri pamoja na uropokaji wake serikali inamchekea tu na kufurahia ila haya yangefanywa na mtu anayehisiwa ni mpinzani hadi sasa angekuwa ndani na kesi zaidi ya 500 hii inatusadikisha kujua kuwa ni mtu mwehu ndani ya system na hata anayosena kaandikiwa na analipwa kutokana na hayo,wafadhili wake ni serikali yenyewe,huyu ndio kiongozi wa propaganda wa CCM kwa sasa
 
Back
Top Bottom