Wengi sasa tunajua kuwa kuna sakata la makontena 20 yanayoshikiliwa na TRA yakidaiwa kuingizwa nchini kwa jina binafsi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Mnada wa makontena hayo, kwa mujibu wa gazeti la leo la Mtanzania, umepangwa kufanyika tena mnamo Septemba 1 mwaka huu yaani Jumamosi ijayo.
Kwa mujibu wa maelezo ya upande wa Makonda yaliyoripotiwa, inadaiwa kuwa makontena hayo 20 yana samani za shule za mkoa wa Dar es Salaam zilizochangwa na kuingizwa nchini na watanzania wema waishio nje ya nchi almaarufu kama Diaspora. Taarifa zinadai kuwa wanaDiaspora hao walichanga na kuleta samani hizo ili kuunga mkono juhudi za Rais na Mkuu huyo wa mkoa wa Dar za kuboresha elimu.
Iko wazi kuwa
JamiiForums ni mtandao wa kijamii wenye wanachama kila kona ya dunia hii. Kuanzia watanzania hadi wale wasio watanzania wamekuwa wanachama wa mtandao huu. Katika kusema hivyo, wapo wana-JF ambao ni wanaDiaspora mfano mtani wangu
Nyani Ngabu anayesemekana kuwepo nchini Marekani. Ndiyo maana nimeona vyema kuwauliza wanaDiaspora kokote walipo, kama 'wachangiaji' wa makontena 20 yanayohusika maswali yafuatayo ya lazima.
Mosi, ni kweli kuwa wanaDiaspora ndio waliochanga na kufanikisha kuletwa kwa makontena yaliyo mikononi mwa TRA? Pili, makontena hayo yamebeba bidhaa gani hasa? Tatu, mlengwa wa makontena hayo na bidhaa zake ni nani? Nne, kwanini yaliingizwa nchini kwa jina binafsi la Paul Makonda na si Ofisi ya Mkuu wa Mkoa au Wizara au Taasisi yoyote ya kiserikali? Na tano, watumaji mliambiwaje kuhusu kodi ya bidhaa hizo ili ziweze kutoka mikononi mwa TRA?