Dar: Maandamano ya ACT Wazalendo kuelekea Ikulu kushinikiza waliotajwa wizi kwenye ripoti ya CAG kuchukuliwa hatua

Dar: Maandamano ya ACT Wazalendo kuelekea Ikulu kushinikiza waliotajwa wizi kwenye ripoti ya CAG kuchukuliwa hatua

Mkuu Kwanza elewa Upinzani wa Tz wa hovyo na viongozi wake hawaaminiki ,,toka nilijue hili sitokuja kupiga kura na Wala mwanafamilia yangu hatathubutuu. Wazazi wangu nilishawapora kadi za mpiga kura toka 2010.

Kuwa na kiongozi asiyekuwa na dira Wala msimamo wa anachokisimamia ni upumbavu

Acha uongo, tangu lini upinzani wameongoza nchi hii. Mna hasira na upinzani walioko nje lakini CCM inayowaibia kila siku mnailamba matakao na kuisujudia. Ondoa unafiki wako hapa.
 
ACT kinapambana sana kuwa chama kikuu cha upinzani. Wakiendelea hivi chini ya miaka mitatu ijayo watakuwa wameshaipiku CHADEMA hasa hii ya sasa.

Maandamano yana nia nzuri sana sema mwamko wa Watanzania ndiyo zero....

View attachment 2591675

Hakiwezi kuipiku CHADEMA hata siku moja. CHADEMA imevuja jasho na damu kufika ilipofika leo. ACT Ni chama Cha Fursa.
 
Kupitia thread hii ndipo utajifunza udhaifu wa wanasiasa wa upinzani Tanzania.
ACT wataanza kushambuliwa na wafuasi na shabiki wa vyama vingine vya upinzani kuhusu haya maandamano kuliko watakavyo shambuliwa na wafuasi wa chama tawala (CCM).

Hiyo yote ni kuwakatisha tamaa wasifanikiwe kupata umaarufu kuliko wao. Kwao bora CCM iendelee kukaa madarakani na kuvurunda vitu kuliko wenzao wawe juu yao kisiasa.

Kwa mshangao kesi kama hii hadi watu maarufu na wajuaji wakubwa wa JF utawakuta wanashangilia kukwamishana wapinzani.

Ufuasi wa vyama kwa msingi wa ukabila, udini na ukanda husababisha tatizo hili.

Hawashambuliwi na CCM maana ni tawi lao. CHADEMA waliitisha UKUTA jeshi la polisi nchi nzima likaingia mazoezini. Mpaka jeshi la JWTZ likajiingiza kwenye mazoezi.
 
Kwa hili nampongeza sana Zitto kwa katika wote at least yeye na chama chake wameonekana kuwa serious kidogo hasa kutokana nareport ya CAG!

Hongera Zitto

Lakini pamoja na juhudi hizi sioni kabisa hao wezi wakichukuliwa hatua kwakuwa mchukua hatua anawaogopa sana hao wezi….kiufupi Samia anawaogopa hao mnao waita wezi

Haya maandamano ya ACT wangefanya Dodoma ingeleta impact.
 
Hili ndilo tatizo kubwa zaidi Tanzania kuliko hata ufisadi...Ingetakiwa woote tuandamane hayo ya kuangalia nan kaandaa maandamano ni ya baadae...Nnaamini tungeleta mshtuko mkubwa Serikalini lakin kwa kujigawa huku ndo tushapoteza kabiiiisaaaaa

ACT hayuko serious ni Kama anafanya utani. Maandamano gani yanapokelewa na Rais ikulu?. Jiulize na wewe.
 
Kwa jinsi watanzania tulivyo, hapo uko kitandani umejifunika na duvet, unaandamana Kwa simu[emoji1787][emoji1787]
Watanzania labda tutaandamana siku mafuriko yakiingia kwenye nyumba zetu, manake tutakuwa hatuna Kwa kujificha.

Acha kutumia neno watanzani sema “kuna Watanzania wengine”
Kujiropokea na kutupa uchoro usio na mbele wala nyuma [emoji2959]
Idiot!
 
Back
Top Bottom