Dar: Mahakama kuu yatupilia mbali kesi ya Halima Mdee na Wabunge wenzake 18. Sasa kupoteza Ubunge

Haya Maamuzi pia yamesababisha CCM ikubali Maridhiano maana Bungeni hakutakuwa na Wabunge wa upinzani.
 
Shida yote hii inaletwa na katiba mbovu tuliyonayo inayompa rais mamlaka makubwa kupindukia na ndio iliyopelekea Magufuli kuhujumu uchaguzi na kuwachagulia Chadema wabunge hao feki.

Bila kupata katiba mpya hakuna sababu ya watu wenye akili zao kupoteza muda kwenda kupiga kura kwenye uchaguzi feki.
 
Wanarekebisha maombi yao halafu wanayarejesha tena.

Ngoma bado mbichi.
 
Haki huinua taifa, waje kitaa huku tupambane maana mambo ya janjajanja Mama Samia kashakataa
 
Kwangu mimi hizi ni habari za Ngoswe, ngoja nimuachie Ngoswe mambo yake, washinde wasishinde I don’t give a damn.
 


Mdee ametuangusha sana sisi wapare. Sisi. Sio watu wa kungangania vitu kwa sababu ya pesa . Angeweza kufungua law firm yake, consulting company yake au kufanya kwenye kampuni nyingine za kimataifa badala ya kutegemea posho ndogo za wabunge na kugushi vitu! Aibu sana. Mbowe alimwambia haya. Sasa wakati mwingine hawa watoto wa walimu wanakuwa nao slow sana🤔
 
Pascal Mayalla usiishie tu "kulike". Nakuona una "like" kila comment ya uzi huu, huna uchoyo kabisa. Lakini tunaomba toa neno tafadhali mtaalamu wa sheria ili nasi tujifunze.
Hahahaaa.... Mwanasheria wa mchongo kapigwa katafunua na vioja vyake cya kimchongo. Kuna Mayalla mwanasheria wa mtandaoni HALAFU Kuna mawakili wasomi mahakamani akina Kibatala, Mtobesya Malya no

Alijitutumua kweli buku , akajitoa fahamu leo kaishia ku-like tu.

Atashauri Nini? Kwani yeye anashauriwa na Nani?

Anyways tumsikilize Mayala Labda atapindua hukumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…