Dar: Mauaji Lemax Bar Sinza kwa Remmy. Kabla ya kujiua, Alex Korosso alimpiga risasi Gift Mushi

Dar: Mauaji Lemax Bar Sinza kwa Remmy. Kabla ya kujiua, Alex Korosso alimpiga risasi Gift Mushi

Du kwahiyo alikuwa ni Afisa usalama lakini hapo mtaani alikuwa anazuga kama mziba pancha? Au kulikuwa na afsa usalama mwingine ambaye baada ya milio ya risasi na yeye akakimbia.
Ukimskiliza kamanda wa polisi wa kinondoni anakuambia afsa usalama mmoja alimuambia acha hiyo sio sawa,,..
Wananchi walokua eneo la tukionwanakuambia bwana gift mziba pancha ndo aliku anamsisitiza aache hiyo kitu,,..
Na alopigwa risasi na kufariki ni bwana gift..
So hapo inabd ujiongeze tu..
Jamaa inabd afe akienda kama mziba pancha..
 
Dogo alikua famous aisee...alikua anapenda attention

Mostly alikua very very good guy,anapenda company sana,very good dude

Without him my childhood isingekua poa...official name yake shule ilikua Abdi Hussein

Ukigeuka ni Alex Buretta,ikafika times anatumia Alex Games,ikawa Alex James,ikaja Alex James Korosso,nasikia ukubwani Dar wanamuita Simba

I remember him sana,yeye ndio alitufundisha ku-surf internet,kufungua email,kudownload mp3 miziki,ku-burn CDs,etc..hiyo ni 1990's ujue

Yeye ndio kwa mara ya kwanza akiwa primary hiyo ni 1996 huko ana video game console ya Nintendo..watu tulishangaa katolea wapi

In the 90's hakuna cassette ya movie yeyote,au rapper yeyote wa America umwambie akuletee ashindwe..imagine ni 1997 kushuka chini Moshi mjini cafe ni moja na mji umejaa tope wote

Magazine gani kutoka America iwe Source,Slam,etc Abdi Hussein hana na tena ni mapya?

Hapa naongelea mtu alikua 12-13-14-15-16 years old!

That little nigga was legendary aisee
Amezaliwa mwaka gani?
 
Kwahiyo

Unaamini hatuna akili sasa za kuweza kua huru kutumia haki yetu ya kujilinda?

Wewe ndio unaamini hivyo?

Yaani kwa lugha ingine,sasa hivi sisi IQ zetu ni ndogo sana kuweza kutumia hii freedom yetu ya kujilinda tuikabidhi serikali ikae nayo ije itupe miaka 20 ijayo tutakua na IQ kubwa?

Ndio hivyo unavyomaanisha?

Kwanini kuna maovu kwenye jamii?Swali uliulizwa shule hili,ulijibuje ukapata division I?

Jibu ni hili : mfumo wa haki wa nchi ni mbaya hivyo kila mtu anatumia anachoweza kujipa haki ya kuonewa.....

Kama hoja yako ni hiyo bado ni hovyo sababu kama ishu ni bastola bado kuna panga,shoka,sumu,etc mtu akitaka kuua mtu anaua tu!

Kwanini usihalalishe hii haki,ukawapa silaha unayoweza ipima ukajua imepigwa na nani na wakati gani kuliko silaha zisizo rasmi kama sime na mapanga hujui hata umiliki wake?

Na pia hii haki kuipa serikali ni hovyo maana wanaoendesha serikali ni watu wenye IQ kama wewe na wao wanaweza tumia haki hiyo kukuua wewe bila sababu na wewe huna njia ya kujitetea

Hizi lawama za bunduki ni nyege tu zimewajaa sababu ni kifaa very modern na status symbol zaidi ya shoka,panga,sime,sumu,etc

Mimi naamini hii haki kila mwanadamu akae nayo yeye kuipa serikali hii haki akushikie ndio kuwapa wanasiasa vichaa waje wakuue usiku bila wewe kujitetea popote
Umezunguka sana mkuu jibu ni jepesi tu sisi ni bado bado sana kupewa freedom ya aina hiyo tutamalizana,,..
Tuende t ivi ivi..
 
Huyo jamaa ni mpenda masifa, wapend sifa always wanaishiaga pabaya tu
Nlikuwaga na jamaa mmja naye alikuwa na chamoto 9mm alipoipata basi ilikuwa shida
Ilikuwa ukikaa naye kdg kaitoa,Mara anakupiga nayo began
Nkamuonya kuwa silaha hii haikufai,kna siku tulikuwa tunapiga mitungi msasani chivas pale
Jamaa si akaipiga juu pemben kulikuwa na bar
Twiga bar ile ilikuwa inajaza wazeee sana
Ah wakaja wakamuokota
Wakampeleka obay,wakati ule obay alikuwa smdy kalinga nlimwambia kalinga huyu jamaa yang mnyanganyeni na msimrudishie
Jamaa mpaka leo hana
Jamaa alikuwa na tabia kama Alex tu

Ova
 
𝐀𝐥𝐞𝐱 𝐚𝐥𝐢𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐩𝐞𝐬𝐚 𝐚𝐢𝐬𝐞𝐞

𝐚𝐜𝐜𝐨𝐮𝐧𝐭 𝐲𝐚𝐤𝐞 𝐲𝐚 𝐢𝐧𝐬𝐭𝐚 𝐢𝐦𝐞𝐣𝐚𝐚 𝐩𝐢𝐜𝐡𝐚 𝐳𝐚 𝐛𝐚𝐭𝐚 𝐛𝐚𝐭𝐚𝐧𝐢. 𝐁𝐨𝐧𝐠𝐨 𝐦𝐩𝐚𝐤𝐚 𝐮𝐥𝐚𝐲𝐚

𝐫𝐢𝐩 𝐛𝐫𝐨

View attachment 1860039
Bora limekufa tu
 
Watu wawili wamefariki Dunia jioni hii Saa 11...baada ya Jamaa anayejishughulisha na Biashara ya Madawa ya Binadamu Alex Koroso kumpiga risasi Jamaa ambaye jina lake halijajulikana lakini anasadikika ni Mziba Pancha wa Maeneo hayo na kisha yeye kujiua kwa kujipiga Risasi kwenye shingo na Kufumua Ubongo wake.

Habari zaidi zitawajia

MUENDELEZO...
===

Watu wawili wamefariki Dunia katika baa ya Lemax iliyopo Sinza kwa Remmy mkoani Dar es Salaam. Baada ya mtu aliyekuwa amelewa kumpiga risasi na kumuua mtu aliyekuwa akimuonya mlevi huyo kuacha kitendo cha kuonesha hadharani silaha aina ya bastola ambapo mlevi huyo akamuua kumuua aliyekuwa akimuonya na kisha kufyatua risasi hewani kabla ya kujiua.

TAZAMA MASHUHUDA WAKIELEZA TUKIO HILI HAPA CHINI: (Video Credit ITV)

View attachment 1857511
Mashuhuda wameeleza kuwa Gift Mushi aliyepigwa risasi jana alikumbwa na tukio hilo, baada ya kumshauri Alex Korosso aache tabia ya kuwatishia watu kuwapiga risasi wakati wakipata kinywaji.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana Julai 17,2021 katika baa ya New Lemax iliyopo maeneo ya Sinza kwa Remmy

Mashuhuda wamesema siku ya tukio Korosso alifika kwenye baa hiyo aliyezoea kunywa akiwatisha wenzake na kwamba anatamani kuua mtu.

"Gift Mushi alipigwa risasi moja ya mguu, mbili za tumboni baada ya kumuona anaendelea kuangaika chini alienda kummalizia kwa kumpiga risasi tatu kichwani na baadaye kurudi kwenye kiti alichokaa kujimalizia mwenyewe kwa kujipiga risasi moja kichwani," amesema Karim Hussen.

"Alikuja toka asubuhi akiwa na gari yake ambayo alimpa ufunguo aitengeneze huku mwenyewe akiwa anaendelea kunywa na kuwatisha wenzake muda wote na baadae Gift Mushi ambaye ni marehemu akamfuata kumshauri aache kuwatisha wenzake wakati wakinywa."

"Baadaye kuna jamaa mmoja alikuwa anakunywa naye silijui jina lake akamuambia kwamba kuwa yeye ni usalama wa taifa na kumuonesha kitambulisho baadae alitulia na kuanza kuomba msamaha, alikaa kimya kwa muda akawa anajishauri ghafla alitoka kwenye kiti alichokaa na kwenda hadi kwa DJ kumuambia azime muziki nako alikataliwa" amesema Lema.

Lema amesema "Kossoro baada ya kukataliwa kuzima muziki alianza kuongea kwa sauti kubwa na kusema watu katika baa wanajifanya usalama na kuchomoa bunduki yake kuanza kupiga risasi juu baadae Gift Mushi alipomfuata kumshauri alipigwa risasi ya mguu kabla ya hajakaa sawa alipigwa risasi mbili za tumboni na akuanguka chini na watu wengine walikuwa wanakunywa walianza kukimbia," amesema.

Amesema wakati huo Gift Mushi alikuwa chini anahangaika baadae alimfuata tena kumpiga risasi tatu kumalizia kumuua na baadae alitoka nje ya baa na kwenda kwenye gari yake kufungua mlango alikuta umefungwa.

Husseni anaeleza "baada ya kuona mlango haufunguki alirudi tena kwenye baa na kukaa kwenye siti yake kisha kujipiga risasi ya kichwa na baadae sisi tulijitokeza,"

Husseni amesema siku hiyo Gift Mushi hakulewa isipokuwa Alex Korosso alikuwa amekuwa na tabia ya kuwatisha watu kwenye baa hii toka miezi miwili alipoanza kumiliki silaha hiyo yenye magazini 16," amesema.


Credit:Mwananchi
Magazine 16
 
Kuna siku nilienda kutoa pesa kwenye ATM pale city, sasa kuna jamaa alikuwa ndani anatoa.......nikasema ngoja nisubiri atoke na mimi niingie pale maana sikuwa na uhakika kama machine nyingine zinatoa. Jamaa si akanipandishia kwamba mimi ni mtu mbaya hadi tukajibizana pale. Ni kweli unavyosema kuna watu walishavurugwa ni vizuri kuwa makini...
Umekaa kijambalika NN mzee baba?
 
Kuna member alituhaidi kutuletea siri za hiyo bar
 
Ndomana marekani mpaka leo mambo ya silaha yanawatesa,maana mpama wendawazim wanamiliki

Ova
Kuna matukio mengi sana yanatokea mitaani kwetu yakipumbavu tu wat wanapasuana na vyupa,wanavunjana miguu,
Mtu anakula kipigo ad anachakaa jambo la kijinga tu..
Unavuta picha hawa watu wangekua wanamiliki silaha za moto,,..
Huyu mtu angekua na silaha kiunoni..
Mungu atuepushie mbali ivo vitu,,..
Asije kutokea kiongozi yeyote akafkiria huo upumbavu aisee tutaisha..
 
In my opinion one of the factor inafanya aman nchi hii bado ipo ipo ni hili jambo la kuzuia silaha za moto wat kuzimiliki kiholela,,
Tukipotea t apa tutajuta milele ..
Historia yetu itabadilika kuanzia hapo,na tutaweka rangi nyekundu kwenye bendera yetu.
Tutaenda kua burundi na congo nyingne,,
Na mungu anatupenda sana watanzania tukio kama hili linatukumbusha tujitazame upya kwenye hili eneo.
Ikiwezekana papigwe pini kbsa lazma uwe na X factor kumilikishwa silaha..
 
Kufa au kupoteza maisha kizembe na kwa vitu vidogo namna hiyo ni uchungu na hasara kwa wazazi na ndugu labda ambao ndio walikuwa wanakutegemea.

Sijui ila nadhani ni vizuri kwa mamlaka husika kuangalia record ya mtu kabla ya kumkabidhi silaha.

Pia nadhani hii inachangiwa na ushawishi wa movies kama John Wick.
 
Kuna matukio mengi sana yanatokea mitaani kwetu yakipumbavu tu wat wanapasuana na vyupa,wanavunjana miguu,
Mtu anakula kipigo ad anachakaa jambo la kijinga tu..
Unavuta picha hawa watu wangekua wanamiliki silaha za moto,,..
Huyu mtu angekua na silaha kiunoni..
Mungu atuepushie mbali ivo vitu,,..
Asije kutokea kiongozi yeyote akafkiria huo upumbavu aisee tutaisha..
Watu wangeuanaa sana
Silaha aka manati ya kizungu hayafai

Ova
 
Kufa au kupoteza maisha kizembe na kwa vitu vidogo namna hiyo ni uchungu na hasara kwa wazazi na ndugu labda ambao ndio walikuwa wanakutegemea.

Sijui ila nadhani ni vizuri kwa mamlaka husika kuangalia record ya mtu kabla ya kumkabidhi silaha.

Pia nadhani hii inachangiwa na ushawishi wa movies kama John Wick
Kifo hakikosi sababu
Na watu wengi naona hawajui
Chanzo cha hasira ukichaa kumpanda jamaa
Pale ila target yake kubwa ilikuwa mmiliki
Wa bar ile,alikuwa ana mmind mmiliki
Hayo mengine naona yalikuja baada ya jamaa
Kulewa sana hadi kufanya mambo ambayo hayakutarajiwa

Ova
 
Back
Top Bottom