Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

ni wazungu alafu ni wageni pia.. je wahalifu hawa wamewezaji kuingia nchini na kufanikiwa kufanya uovu... sijawahi kusikia dunianii..
tujikumbushe waliolipua ubalozi wa USA TANZANIA walikuwa wageni au wazawa?
 
Ujanielewa kabisa namanisha saa zingine polisi wanafanyaga makusudi kutoa misleading information ili anayetafutwa ajue polisi wamepotea muulekeo kumbe ni mtego.
 
Amen
 
ni wazungu alafu ni wageni pia.. je wahalifu hawa wamewezaji kuingia nchini na kufanikiwa kufanya uovu... sijawahi kusikia dunianii..
tujikumbushe waliolipua ubalozi wa USA TANZANIA walikuwa wageni au wazawa?
Wageni toka Belgium waliingia France na kufanya uhalifu lile tukio la kighaidi.

Wewe kama haujapata kusikia haimaaniahi haijawahi kutokea duniani.

Usisahau Black September, tukio la ughaidi Ujerumani wakati wa michezo ya olympic.
Usisahau tukio la Westgate Kenya walikuwepo wageni na mmojawapo ni kijana wa kitanzania.

Wakati mwingine ni busara kunyamaza kuliko kuongea.
 
Unapomuachia Bashite ajifanye msemaji wa Jeshi, tegemea lolote kuchomoka kutoka kinywani mwake.
 
Mambo mengine yanatakiwa kuwa siri hadi hapo yanapothibitishwa kuwa na ukweli. Kwa mfano wahusika wakivaa vinyago vyenye sura ya watu weupe tayari taarifa zitakazotolewa zinakuwa si sahihi na pia zitafanya wapelelezi wapoteze muda kwa kujikita kutafuta watu weupe. Ni vyema tu wakatoa taarifa kuwa wahusika ni "watu wasiojulikana" hadi hapo watakapojulikana ndio taarifa rasmi itolewe.
 

Yes ilipaswa Kuwa hivyo lakin unashangaa Afisa wa Usalama anasimama na kuzungumza taarifa Za kiitelijensia Kama vile yupo Morning call na wenzie kutathmini hatua Za kipelelezi
 
Sitaki kuwa mnafki jumba bovu kuniangukia Mo kama akitoka salama ataacha hizi jokes zake no way
 

Attachments

  • issamichuzi___BoyO6Dpl9ty___.jpeg
    88.2 KB · Views: 37
  • issamichuzi___BoyO6Dpl9ty___.jpeg
    88.2 KB · Views: 32
Umeishia darasa la ngapi mkuu..?? Maana mchango wako hapa ni wa kama wa mtu wa darasa la tatu B...
Hii the so called CCM mpya itazidi kuwafanya vijana kuwa mazezeta. Wanajaribu kurejesha propoganda zilizopitwa na wakati za enzi za ujamaa. Sasa unasikia hata viongozi wao wanatamka majukwaani 'mabepari' (watakiona kijinga cha moto), mabeberu, nk. Hizi propoganda zilikuwa na maana wakati wa vita baridi za kiitikadi kati ya ubepari vs usoshalisti. Lakini dunia imebadilika na kila mmoja (ikiwa ni pamoja na Tanzania, China, Urusi, nk) amekumbatia itikadi ya soko huria. Sasa propoganda za enzi za ujamaa hazina mashiko katika zama hizi za soko huria.. Ni kuapotosha vijana. Wanabakia kuimba vitu visivyokuwepo!!
 
Waziri wa mambo ya ndani Mh Kangi Lugola ni kama amepugwa ganzi vile. Hajasikika kokote, kwa kulaani na kuonesha mkakati wa kumpata Tajiri Mo.

Kama tujuavyo kwa kila tukio Nchini, lazima waziri huyu atoke hadharani na kusema chochote.

Je Waziri amejiepusha na huu mchezo mchafu?
Au Hataki kushiriki kwenye ishu ya kitoto?
Au sio level yake kusemea hili?
 
Na anavyopenda ujiko, inashangaza kuwa kimya mpaka sasa. Au naye kaminywa na mwana wa mfalme jiwe?
 
Bosi wake - Mkuu wa mkoa ameshatoa tamko, sasa unafikiri atasema nini zaidi?
 
Bosi wake - Mkuu wa mkoa ameshatoa tamko, sasa unafikiri atasema nini zaidi?
'Kama huna taarifa kamili kaa kimya'.......Albert Bashite. Lugola ametii bila shuruti ndo maana yupo kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…