Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Bila shaka hili la kujua kuwa watekaji ni wazungu likikuwa na faida kubwa kwa wana usalama. Walikuwa wamepunguziwa kazi ya kudeal na watu wote na kuamua kudeal na wazungu ambao niwatu wachache.

Kusema kuwa watekaji ni wazungu si kunawaalert wajipange zaidi. Na pengine walitumia uzungu wakijua hamna mtu atawahisi sasa wakijua wamejulikana watajipanga zaidi.

kiusalama kulikuwa na faida ya kusema watekaji ni wazungu? kuna weza kuwa na lengo lingine la kusema watekaji ni wazungu? sielewielewi!!!?
ni wazungu alafu ni wageni pia.. je wahalifu hawa wamewezaji kuingia nchini na kufanikiwa kufanya uovu... sijawahi kusikia dunianii..
tujikumbushe waliolipua ubalozi wa USA TANZANIA walikuwa wageni au wazawa?
 
Naomba tuache kabisa kuhusisha serikali na mambo ambayo si kweli.kuna ujambazi na uharamia mkubwa unafanyika nchini kila siku hivi ni kweli serikali ndio inahusika, hapana si kweli.tukio la kutekwa MO ni tukio lililopangwa na watu wabaya sio serikali.Mo ni mfanyabiashara inawezekana kabisa akawa na maadui katika biashara zake,au kuna watu wanataka kumtumia kama njia ya kupata pesa.tukio kama hilo sio la kwanza hapa afrika kwa mfanyabiashara kubwa kama mo kutekwa na waalifu na baadae kudai pesa.Tuache vyombo vya serikali vifanye kazi yao.sisi kama raia tuwape support ili kazi yao ifanikiwe
Ujanielewa kabisa namanisha saa zingine polisi wanafanyaga makusudi kutoa misleading information ili anayetafutwa ajue polisi wamepotea muulekeo kumbe ni mtego.
 
Hii hali tumeilete na kuilea wenyewe Watanzania,nasena hivyo kwa sababu utekaji haukuanza leo na kwa watu wa kaliba ya MO,wanasiasa na "wasiokuwa upande wao" wamehujumiwa sana,wengine wameuawa wengine wamepotezwa lakini hatua hazikuchukuliwa,sasa imefika kwa "mwenzao" wameshtuka,wamesahau kuwa walichopanda sasa kinazaa,watoto wetu wangapi siku za hivi karibuni wamepotea, hakuna anayeonesha kujali hasa,nasikitika kwa hili kumtokea MO,ila naweza kusema ni ishara kuwa Mungu anatuamsha na kutukumbusha kuwa haya siyo maisha,sasa hatua zitachukuliwa kuutokomeza huu uhalifu tuliouasisi na kujiona tuko salama hautatugusa,Mungu twaomba MO huko wanakomshikilia wamuachie bila kumdhuru na bila sharti lolote,kwa jina la Yesu Kristo
Amen
 
ni wazungu alafu ni wageni pia.. je wahalifu hawa wamewezaji kuingia nchini na kufanikiwa kufanya uovu... sijawahi kusikia dunianii..
tujikumbushe waliolipua ubalozi wa USA TANZANIA walikuwa wageni au wazawa?
Wageni toka Belgium waliingia France na kufanya uhalifu lile tukio la kighaidi.

Wewe kama haujapata kusikia haimaaniahi haijawahi kutokea duniani.

Usisahau Black September, tukio la ughaidi Ujerumani wakati wa michezo ya olympic.
Usisahau tukio la Westgate Kenya walikuwepo wageni na mmojawapo ni kijana wa kitanzania.

Wakati mwingine ni busara kunyamaza kuliko kuongea.
 
Unapomuachia Bashite ajifanye msemaji wa Jeshi, tegemea lolote kuchomoka kutoka kinywani mwake.
 
Kuna Makosa kadhaa Vyombo vyetu vya Ulinzi huwa wanafanya wanapo report Matukio

Kutaja udhaifu wa ushahidi uliokusanya ni kosa kubwa Sana Kwa wenye ujuzi kiasi wa Masuala hayo


Kutangaza Kuwa CCTV Camera hazioneshi Vizuri sura Za Watuhumiwa
Hazioneshi Mlango walioingilia n.k maana yake unawafanya wahalifu watuambie udhaifu uliopo kwny collected evidence Na hivyo kujipanga kutokea hapo Na Pia Hata suspect utakaowakamata kuanzia Leo watajua Kwa kiasi gani kuna udhaifu kwny ushahidi mlionao!

Kwa Mfano Kama wahalifu Ni waarabu/ Wahindi Au wachina lakin nyie mme tangaza Kuwa Ni Wazungu maana yake tayari washajua mpo off point hivyo wanaweza kuchomoka kirahisi

Tusiwape Fursa Wanasiasa Kuwa wasemaji wa Masuala haya Kwa Kuwa kuna taarifa zingine Ni muhimu Kwa wakati Fulani but sio for public consumption Kwa wakati huo

Kwenye Shambulio la 7th August, 1998 pallet Ubalozi wa America Ally Hassan Mwinyi Road walipata evidence nyingi Sana Za awali lakin hawaku expose chochote bali tulikuja kujua Baada ya Khalifa Mohamed kukamatwa Bungoni Ilala Na kupelekwa America Na kuja kugundulika Mengi wakati kesi inaendelea


Kuanza kufafanua features Za collected evidence Ni kosa kubwa Sana tunafanya Kwa Kujua Au kutojua

Unapotaja mbinu walizotumia wahalifu hadharan maana yake unatoa Semina Elekezi Kwa wahalifu wengine waige bila ya kutambua
Mambo mengine yanatakiwa kuwa siri hadi hapo yanapothibitishwa kuwa na ukweli. Kwa mfano wahusika wakivaa vinyago vyenye sura ya watu weupe tayari taarifa zitakazotolewa zinakuwa si sahihi na pia zitafanya wapelelezi wapoteze muda kwa kujikita kutafuta watu weupe. Ni vyema tu wakatoa taarifa kuwa wahusika ni "watu wasiojulikana" hadi hapo watakapojulikana ndio taarifa rasmi itolewe.
 
Mambo mengine yanatakiwa kuwa siri hadi hapo yanapothibitishwa kuwa na ukweli. Kwa mfano wahusika wakivaa vinyago vyenye sura ya watu weupe tayari taarifa zitakazotolewa zinakuwa si sahihi na pia zitafanya wapelelezi wapoteze muda kwa kujikita kutafuta watu weupe. Ni vyema tu wakatoa taarifa kuwa wahusika ni "watu wasiojulikana" hadi hapo watakapojulikana ndio taarifa rasmi itolewe.

Yes ilipaswa Kuwa hivyo lakin unashangaa Afisa wa Usalama anasimama na kuzungumza taarifa Za kiitelijensia Kama vile yupo Morning call na wenzie kutathmini hatua Za kipelelezi
 
Sitaki kuwa mnafki jumba bovu kuniangukia Mo kama akitoka salama ataacha hizi jokes zake no way
 

Attachments

  • issamichuzi___BoyO6Dpl9ty___.jpeg
    issamichuzi___BoyO6Dpl9ty___.jpeg
    88.2 KB · Views: 37
  • issamichuzi___BoyO6Dpl9ty___.jpeg
    issamichuzi___BoyO6Dpl9ty___.jpeg
    88.2 KB · Views: 32
Umeishia darasa la ngapi mkuu..?? Maana mchango wako hapa ni wa kama wa mtu wa darasa la tatu B...
Hii the so called CCM mpya itazidi kuwafanya vijana kuwa mazezeta. Wanajaribu kurejesha propoganda zilizopitwa na wakati za enzi za ujamaa. Sasa unasikia hata viongozi wao wanatamka majukwaani 'mabepari' (watakiona kijinga cha moto), mabeberu, nk. Hizi propoganda zilikuwa na maana wakati wa vita baridi za kiitikadi kati ya ubepari vs usoshalisti. Lakini dunia imebadilika na kila mmoja (ikiwa ni pamoja na Tanzania, China, Urusi, nk) amekumbatia itikadi ya soko huria. Sasa propoganda za enzi za ujamaa hazina mashiko katika zama hizi za soko huria.. Ni kuapotosha vijana. Wanabakia kuimba vitu visivyokuwepo!!
 
Waziri wa mambo ya ndani Mh Kangi Lugola ni kama amepugwa ganzi vile. Hajasikika kokote, kwa kulaani na kuonesha mkakati wa kumpata Tajiri Mo.

Kama tujuavyo kwa kila tukio Nchini, lazima waziri huyu atoke hadharani na kusema chochote.

Je Waziri amejiepusha na huu mchezo mchafu?
Au Hataki kushiriki kwenye ishu ya kitoto?
Au sio level yake kusemea hili?
 
Waziri wa mambo ya ndani Mh Kangi Lugola ni kama amepugwa ganzi vile. Hajasikika kokote, kwa kulaani na kuonesha mkakati wa kumpata Tajiri Mo.

Kama tujuavyo kwa kila tukio Nchini, lazima waziri huyu atoke hadharani na kusema chochote.

Je Waziri amejiepusha na huu mchezo mchafu?
Au Hataki kushiriki kwenye ishu ya kitoto?
Au sio level yake kusemea hili?
Na anavyopenda ujiko, inashangaza kuwa kimya mpaka sasa. Au naye kaminywa na mwana wa mfalme jiwe?
 
Bosi wake - Mkuu wa mkoa ameshatoa tamko, sasa unafikiri atasema nini zaidi?
 
Bosi wake - Mkuu wa mkoa ameshatoa tamko, sasa unafikiri atasema nini zaidi?
'Kama huna taarifa kamili kaa kimya'.......Albert Bashite. Lugola ametii bila shuruti ndo maana yupo kimya.
 
Back
Top Bottom