Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Hiyo No.6 ni tatizo kubwa kwenye matukio kama haya. Kumbuka katika tukio hili mtu huyohuyo alitoa taarifa kwamba Mo ameshapatina kitu ambacho siyo kweli. Kachukuliwa hatua gani kwa kusababisha mkanganyiko huo? Huyu haguswi ingawaje siyo mtu makini kwenye matukio anayoshiriki. Ni mtu ambaye hawezi kuficha vitendo dhanifu vya uhalifu (conduct) baada ya kutenda.
 
Mo hapendagi makuuu...anaweza ata kula ugali dagaa/maharagwe na wafanyakazi wakeee..
Ni kweli ndugu,
Hapajawahi kutokea tajiri kijana na anayejishusha kama MO,
Kazini tunaishi naye kama mfanyakazi wa kawaida. ukiacha baadhi ya siku anazokuwa siriazi kidogo.
Mpirani tunashangilia naye pamoja, na wanaoomba kupiga picha naye anawakubalia tu.
Katika masula ya kijamii tupo naye bega kwa bega
Hakika MO ni mtu wa watu sana ndio maana hatembei na walinzi muda wote.
Matajiri wengi wanajifungia na hawaonekani, wanajitenga na watu hasa wa kima cha chini lakini MO, anatutembelea huku mtaani mara kwa mara.
Tunakula naye na kucheza naye na kutaniana naye.
Kwa kweli tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vijitahidi kumpata ndugu yetu MO.
MO anamchango mkubwa kwa taifa hili.
Ninauhakia analipa kodi kubwa, na pia ameajiri watanzania wengi sana, na ni mfadhiri wa mambo mengi ya wananchi.
Nina uhakika mkono wa dola ya serikari yetu una nguvu kubwa ya kumpata MO.
Tuna imani na Serikali yetu.
 
Mzee baba unafananisha USA na ushuzi wa tz ..
 
Moyoni mwako una jambo unalotaka kulisema lakini unashindwa. Kuna kitu gani cha kushangaza kwamba ametekwa na watu wasiojulikana? Kama wewe unawajua si uwataje? Hapo hapo polisi wamesema kuna Wazungu wanaotuhumiwa kuhusika na utekaji huo. Wewe unakanusha vikali habari hiyo kama vile una uhakika Mzungu hawezi kufanya hivyo. Huu ni upungufu wa fikra kuanza kushabikia kitu ambacho wala huna habari kamilifu kuhusiana na suala husika.
 
Ukitumia akili ya ziada unagundua ni kwa jinsi gani siku za karibuni Bashite amekuwa akijiweka karibu sana na Simba. Ameweza kuwa win confidence kiasi hata Simba day wanamualika kumbe ana lake jambo.
Kila aliyepatwa na dhahma alianza nao urafiki was nguvu sana. Ona Clouds! jee wasanii! Hata wale aliowataja madawa ya kulevya?
Huyo ni nyoka ndani ya Nyumba
 
Soko la mbaazi limeua sana uchumi wa wakulima hasa wa kwetu Ruvuma.
Kwa sasa
Gunia la mahindi linauzwa Tsh 20,000/
Dumla ya Mbaazi ilikuwa inauzwa Tsh 12,000/-
Hivyo Gunia la mbaazi liliuzwa zaidi ya Tsh 500,000/-
Kama ni ukweli Manji ndiye aliyekuwa ananunua Mbaazi basi jinsi alivyoshughulikiwa wakati ule ameathiri sana kipato cha wakulima wa kusini mwa Tanzania.
Leo Manji yupo huru, ina maana hakuwa na hatia.
Lakini wakulima wamekosa soko la mazao yao.
Hapo nani kapata hasara ?
Naiomba Serikali inapo washughurikia hawa matajiri wanao changia uchumi wa wa wananchi basi iwa shughulikie kwa STAHA.
Soko la mbaazi lilianza kuturudisha vijijini sisi tunao kwepa umasikini na kukimbilia mjini.
Tulianzisha mashamba vijijini, tukainua JEMBE, tena la mkono na tukanufaika.
Leo ni kilio kila mahali. Mbaazi inaozea mashambani, vijana wanakuja tena mjini kufafuta fulsa.
Jamani tunapo washugulikia hawa matajiri, basi tuwashughulike kwa staha.
Leo Manji yupo huru ila wakulima ndio wapo hoi.
Wakulima ndio wapo Jela Bosi yupo uraiani.
Jamani tunapo washughulikia hawa matajiri basi tuwashughulikie kwa staha.
Matajiri akina Manji, Bakhresa, Mengi, MO, Rostam Azizi na wengineo.
Naomba Radhi kama nimekosea mahali.
 
Tangu waseme wale police waliopiga watu ukonga hawakuwa police ni wahuni wna gari za pt tangu waseme risasi ilipigwa juuu ikakata kona huwa sinaga muda kumsikikiza mambosasa najichefua moyo bure
Mambosasa hafai kabisa na genge lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…