Yes, mwanangu alianza daraza la saba na miaka 5 na miezi michache sana. Alimaliza darasa la Saba na miaka 12 kasoro. Form One aliingia na miaka 12, miaka 13 form two na three kidogo, miaka 13 form tree na form four kidogo, akamaliza na miaka 14. Form five miaka 14 na 15 ikamkutia hapo, akamaliza form Six na miaka 16 kasoro. Inategemea na jinsi ulivyomwahisha mtoto shule na jinsi Mungu alivyomjalia mtoto. Kwa misingi hii mwanangu huyu alinza kupenda kuandika akiwa mdogo mno alipoona wenzake wanaenda na kutoka shule wakiwa wanafanya home work naye anakaa mezani anaanza kuandika yake, mwishowe akawa anachukua kitabu anaigiliza moja nyingi sana, number 4, 6 na 9. Nikaona bora awahi tu huko day care. Kule akafanye vizuri na pre unit alisoma kidogo sana shule yake wakanishauri aanze darasa la kwanza na ni mvulana. Nilipinga sana ila mwalimu alisema akiendelea kusoma pre unit ataone kila kitu ni rahisi na haikuwa sababu na ataona kama ni marudio yaani kwa kifupi angekinai. Kweli nikakubali akaanza darasa la kwanza kishingo upande. Sijutii kwa kuwa aliendelea kufanya vizuri na yuko mbali mno kiuwezo kitaaluma kuliko hata ndugu zake nilioanzisha wakiwa na miaka 6 na 7 kasoro.