Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Zile tunazoona ktk movies za ki - Nigeria zinaweza anza kuwa practiced taratibu hapa....

Watu hali ngumu ya kifedha na kimaisha kwa ujumla, wanatafuta "shortcuts" za kujipatia fedha....

Wanawavizia wenye mkwanja watu sampuli ya hawa kina Dewji.....

Wanakuteka na kukuhifadhi sehemu....

Wanalazimisha mabadilishano ya uhai wako na ukwasi wenu.....

Most likely, hii ina sura ya namna hii.....

Hata hivyo wanaweza kufanikiwa kupata watakacho kama tu wamefunzwa mikakati ya kujipatia fedha kwa njia hiyo....

Vinginevyo, watanaswa tu na wasipate hata senti!!
Sio rahisi hivo hayo mambo..tena kwa mtu mzito kama Dewji
 
Hili suala sio dogo, lonaweza kuwa dogo ila likitokea katika familia yako au jamii yako nadhani utaongea vya msingi kuhusu hili, na tuache tuone vyombo vya usalama vinasemaje. Tuwe positive kidogo
 
Kufunga maana yake si kuzidisha ukaguzi Na kuongeza ulinzi? Haimaanishi isiingie Ndege wala kutoka Ndege..


Hapana, kufungwa maana yake kufungwa, airport zimefungwa . Plain and simple.

Wamefunga airport kwa sababu mtu mmoja katekwa, tukihoji tunaambiwa familia nyingi zinamtegemea, basi tumtoe jela Singasinga wa Escrow, Mzee Rugemalila ane import ma Heineken kwenye ma baa yote nchini, na Hans Pope anaesafirisha mafuta ya bandari yetu kwenda Zambia nae tuache kumtafuta. Wote hawa ni matajiri wakubwa, familia nyingi zinawategemea. Tajiri akitekwa njia zote za nchi zinafungwa.

Ndio kuwekwa mfukoni kwenyewe huko.
 
Ninasikitika Mwekezaji Mkubwa nchi hii ametekwa. Ni tikisiko kwa uchumi na jamii kwa ujumba wale ambao wameajiriwa katika makampuni yake. Ninaamini familia iko imara katika kuhakikisha hakuna kitakachoenda vibaya katika makampuni kwa kuwa MD hayupo. Huu ndiyo uzuri wa wenzetu wenye ngozi nyeupe kwa kuwa succession plan iko vizuri. Cha kusikitisha ni kwamba huyu ni tajiri mkubwa sana nchini na alitakiwa awe na ulinzi binafsi kabisa kama ule wa viongozi wetu. Yaani MO anashindwa na celebrities kama Chibu wenye mabauza na walinzi wa nguvu. Yeye MO alitakiwa kabisa awe na gari la walinzi wakati wote mchana awapo kazini na usiku pia na nyumbani ndiyo usiseme. Pia gari yake nayo inatakiwa iwe na vifaa vya usalama n.k. Hapa kuna uzembe mkubwa na pengine alijiamini sana kitu ambacho kwa dunia ya sasa si rafiki tena kwa kuwa wenye wivu wapo, washindani wapo kwa upande wa biashara, na wenye roho mbaya tu wapo.

Mungu epusha mabaya yote kwa Mwekezaji huyu hodari Tanzania.
Hili ni movie LA ccm
 
bashite acha kuwatisha watu na kauli za kijinga. Aliyekuambia uongee kabla ya vyombo vya usalama nani?
Huu upuuzi wa bashite na genge lako has to stop mmeterrorize WaTz vya kutosha enough is enough wee mkosa utu kwa WaTz.
Mkuu wa nchi tuambie WaTz hili genge la hawa wahuni nini kiko nyuma yake
bashite you must go!
 
Tuanzishe Maandamano ya kwenye mitandao kama yale ya Free ROMA ili kusaidia na yeye aachiwe kama alivyopona ROMA.
 
Nimemsikiliza Makonda vizuri kwenye ile clip hakuna sehemu kasema kuwa Mo kapatikana..Waandishi wa habari na wenyewe wasipende kushindana kupost taarifa kwa uharaka tena taarifa kubwa kama hizi..
je unafkiri ilitokea kwa baatimbaya?
ivi kwa nn wasitoe security footage
ili watu wanaowajua wawasaidie?
ni vipi waljua ni wazungu wakati mashuuda wanasema watekaji walvaa kininja?
hawawezi kusema uraia wao sabab itaathiri mahusiano ya kidiplomasia kama ni uwongo...

joto lmezidi so atapatikana sjui lini lkn myb watekaji wakitimiza adhma yao
 
Pamoja na polisi wetu kuonyesha udhaifu mkubwa kwa namna wanavyshughulikia uhalifu kwa mifano (Matukio yaliyovuma sana ya watu kutekwa na kuuwawa, na tukio la kupigwa risasi Mb. Tundu Lissu), kwa hili tuwashauri polisi yakipita masaa 24 hajapatikana, basi waombe msaada vyombo vya nje ikiwepo interpol/FBI watusaidie kuwasaka hawa watekaji. Kwa tukio hili nchi inaweza kupata hasara kubwa sana, ukizingatia huyu Mo anatambulika kimataifa na network yake inalipa taiafa hadhi kubwa kuliko sisi maskini ambao hata tukipotea mia moja serikali inaweza kufumba macho na maisha yakaendelea kama hakuna kilichotokea.
 
Viwanda waliua wenyewe sasa aunge mkono upuuzi huu wa vyerehani vinne?

Huu ni ujinga
"Matajiri wataishi kama mashetani"aliyetoa kauli hii number one suspect...Mo kawekeza 20 billions Simba kuna mijitu imenuna kwa nini asiunge mkono Sera ya viwanda...mpaka SAA sita usiku hajapatikana ..watu wote msako nyumba kwa nyumba hata kama ya serikali...
 
Hili neno la hapa kazi tu yawezekana lilitumika wakati wakitimiza azma yao ili iwe nchi ya viwanda
 
Itakuwa ni bashite tu anataka kuwakamua hela ndugu za Mo na kumlazimisha Mo ahamishe fedha kwenda akaunti za bashite za offshore.
 
Huyo nina uhakika hajatekwa, yupo mikono salama, cha muhimu ni kusubiri muda ufike tukutane naye mahakamani, tatizo kuna idara zinakiuka taratibu, TISS kazi yake si kukamata wala kufanya upelelezi wa makosa ya jinai, wao wakiona shwala linahatarisha usalama wa nchi na wakawa na uhakika juu ya ishu hiyo hupeleka kwenye chombo husika ambao ni polisi kwa ajili ya kufanya upelelezi na kupeleka shauri kwa DPP au mahakamani, huyo atakuwa chini ya TISS na ndio maana usikute polisi hawana taarifa yoyote na ukamataji wake umekuwa kama wa kutekwa maana wao hawana mamlaka ya kumkamata mtu na kumuweka kizuizini
 
Back
Top Bottom