Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

Naingia kwenye mada moja kwa moja. Mvua kubwa sana inanyesha hapa Dar sijapata kuona. Tangu nizaliwe sijawahi kushuhudia mvua kubwa kiasi hiki.

View attachment 2878125
Serikali ijiandae kukabiliana na athari za mafuriko zitakazosababishwa na mvua hii kwani kadri muda unavyoenda mvua inazidi kuongezeka

Mara ya mwisho mvua iliponyesha ilingo'a madaraja na kuua watu watatu. Safari hii tujiandae kwa maafa zaidi.

Tuambie mahali ulipo hali ikoje na nini tutarajie baada ya mvua hii.


Pia soma: Mvua ilivyoacha maumivu mmoja adaiwa kufa Dar

UPDATES

*Mawasiliano kati ya Tegeta na Kunduchi yamekatika baada ya daraja la Kunduchi-Mtongani kukatika. Magari, nyumba na mali za raia zimesombwa na maji. Nguzo za umeme zimeanguka na baadhi ya raia wamefariki. Tatizo watu wamejenga karibu na mto kwa kupewa vibali na maofisa ardhi wa Serikali.

*Hadi sasa mvua inaendelea kunyesha baadhi ya maeneo hapa Dar. Serikali itoe tahadhari kwa wananchi na ichukue hatua kukabiliana na mafuriko.

*Serikali inaendelea kufanya tathmini ya uharibifu na hasara iliyojitokeza. Madhara ya mafuriko haya mpaka sasa ni kama unavyoyasikia kutoka kwenye rekodi hapo chini iliyoripotiwa na Radio One Stereo. Katika rekodi hii utamsikia mwananchi akilalamika kupoteza Tsh 5,000,000 ambazo zote zimesombwa na mafuriko. Hakufanikiwa kuokoa hata shilingi moja.

* Nyumba 7, magari na mali za wananchi zimesombwa na maji, mtu mmoja amefariki na madaraja kadhaa yamevunjika na kukata mawasiliano ya barabara.

*Raia mmoja ameokota gari lillilosombwa na mafuriko lakini watu wenye roho mbaya wamemzuia kulichukua.


View attachment 2879043
*Wakandarasi wanaendelea kuzibua barabara zilizozibwa na maji, mawe na magogo ili kurejesha mawasiliano.

Nitaendelea kuwapa updates na picha kadri nitakavyozipata.........
Raia mmoja ameokota gari lillilosombwa na mafuriko lakini watu wenye roho mbaya wamemzuia kulichukua.😢😢😢
 
Mvua za Mwaka 2011 uliziona wewe?
Ilikuaga 2012 nakumbuka kama sio 2010 kuna kombe la dunia lilikua linachezwa aisee ilianzaga mvua nakumbuka nilitoka muhimbili mpaka kimara kwa mguu
Jangwani pale maji yashafika ukingoni hapo mvua ilianzaga kama saa 10 hivi hio 12 jioni aisee mvua ilinyesha siku 3 kama sio4 mfululizo wallah sisahau
 
Leo 22/01/2025 naona kuna mvua itanyesha mpaka 30/01/2025 waambieni wa mabondeni waondoke
Yeah. Wahame mapema vinginevyo wakikaidi kama Mbowe watakumbwa na mafuriko ya Tundu Lissu.
 
Hapa mjini kati ya Dasalama mvua imekung'uta tangu usiku wa manane Tundu Lissu aliposhinda uchaguzi hadi sasa inaendelea kupiga mkuu. Kama ulikuwa na mpango wa kuja mjini, ahitisha kabisa.
Mkoa wa Dasilamu nyuma ya Eyapoti
Mvua kiasi tu wala sio ya kutisha
 
Back
Top Bottom