Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

Dar ni slum Tu , ule mji haufai kwa watu wengi kuishi , ni maeneo machache sana ambayo yalikuwa designed kuishi watu humo ,tangia enzi za mjerumani
Sasa wabongo mmejazana kama sisimizi humo , lazima hata miundo mbinu izidiwe + poor uban planning ya serikali ya wapumbavu ccm
Kazi mnayo
Wapi Tanzania sio slum?



Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Hapa Moshi kwa sasa inanyesha.
Kuna mtu kajiokotea mke kwenye mafuriko
1705945346710.png
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Mvua kubwa sana inanyesha hapa Dar sijapata kuona. Tangu nizaliwe sijawahi kushuhudia mvua kubwa kiasi hiki.

View attachment 2878125
Serikali ijiandae kukabiliana na athari za mafuriko zitakazosababishwa na mvua hii kwani kadri muda unavyoenda mvua inazidi kuongezeka

Mara ya mwisho mvua iliponyesha ilingo'a madaraja na kuua watu watatu. Safari hii tujiandae kwa maafa zaidi.

Tuambie mahali ulipo hali ikoje na nini tutarajie baada ya mvua hii.


Pia soma: Mvua ilivyoacha maumivu mmoja adaiwa kufa Dar

UPDATES

*Mawasiliano kati ya Tegeta na Kunduchi yamekatika baada ya daraja la Kunduchi-Mtongani kukatika. Magari, nyumba na mali za raia zimesombwa na maji. Nguzo za umeme zimeanguka na baadhi ya raia wamefariki. Tatizo watu wamejenga karibu na mto kwa kupewa vibali na maofisa ardhi wa Serikali.

*Hadi sasa mvua inaendelea kunyesha baadhi ya maeneo hapa Dar. Serikali itoe tahadhari kwa wananchi na ichukue hatua kukabiliana na mafuriko.

*Serikali inaendelea kufanya tathmini ya uharibifu na hasara iliyojitokeza. Madhara ya mafuriko haya mpaka sasa ni kama unavyoyasikia kutoka kwenye rekodi hapo chini iliyoripotiwa na Radio One Stereo. Katika rekodi hii utamsikia mwananchi akilalamika kupoteza Tsh 5,000,000 ambazo zote zimesombwa na mafuriko. Hakufanikiwa kuokoa hata shilingi moja.

* Nyumba 7, magari na mali za wananchi zimesombwa na maji, mtu mmoja amefariki na madaraja kadhaa yamevunjika na kukata mawasiliano ya barabara.

*Raia mmoja ameokota gari lillilosombwa na mafuriko lakini watu wenye roho mbaya wamemzuia kulichukua.


View attachment 2879043
*Wakandarasi wanaendelea kuzibua barabara zilizozibwa na maji, mawe na magogo ili kurejesha mawasiliano.

Nitaendelea kuwapa updates na picha kadri nitakavyozipata.........
Hii mvua kubwa inayonyesha leo haijawahi kutokea. Nimeipa jina la Tundu Lissu.
 
Kuna nabii alitabiri, Dar kufikia mwezi Mei mwaka huu, itafunikwa na maji, kwamba kuna Tsunami itaipiga Dar.
Huenda hizi mvua ni maonyo ya mwisho. Watu wa Mungu watamuuliza Mungu ukweli wa unabii huu. Ila walio wengi waliposikia unabii huo, walimdhihaki mtoa unabii.

Biblia inasema "msiutweze unabii, bali zipimeni roho kama zimetokana na Mungu au la!
Utapeli tu, hakuna cha unabii wala nini.
 
Back
Top Bottom