Dar: Mwandishi Bollen Ngetti adaiwa kutekwa tena na watu wasiojulikana; apatikana

Mtu anatekwa kisha anapata muda wa kumjulisha mke au ndugu kuwa katekwa na sababu anatoa, sasa hapo anakuwa katekwa au kajiteka, mtekaji anayekuruhusu ufanye mawasiliano huyo ni mtekani au mshikaji tu? Tuwe serious basi, hiyo itakuwa ni movie ya van dame.
 
Kuwa hiyo Mkuu Salary Slip unahafiki Jeshi la Polisi kufanzia kazi taarifa/tetesi za mitandaoni?
Je unahafiki waanzishaji wa taarifa mitandaoni kuwa kama sehemu ya ushaidi?
 
Kama nchi imemshinda jiwe ajiuzulu tu. Hatutaki upuuzi wake wa kutulazimishia machafuko anaotuletea.
 
Kwani wewe uko msumbiji?
 
JPM amechaguliwa kihalali . Kama una ubavu toka nyuma ya keyboard upinge nenda hata mahakamani basi. Tunampenda raisi wetu
 
Kutekana tena kwa wale wanaoandika usiyoyapenda wewe ni ushamba na upumbavu. Haya mambo ya kijima sana
Andika kwa Lugha ya hoja na si matusi. Kwa nini kutukana kudhalilisha na kuvunja heshima ya mtu. Pinga kwa hoja utaeleweka
 
Watz tuna maneno mengi vitendo zero. Haya mambo tulitakiwa kuyakataa tokea zamani siyo sasa. Watu kama tundu lissu walipigwa lisasi zaidi ya 30. Tena ndani ya sensitive government areas, watu kimya. Watu wamepotea, wamepigwa lisasi hadharani kama mwangosi na akwilina watu kimya. Leo hii tumejificha nyuma ya id fake tunapekecha maneno yasiyo na tija. Bora tukubali wajanja waendelee kufanya watakayo, tukubali hatuna uwezo wa kufanya chochote hivy tuache kelele.
 
Leo wananchi wenye kazi ya kusifu na kuabudu na kutetea kazi zote huyu muumiani mbona wako kimya sana
 
Wo shi niubi,
Uwana harakati au siasa ni huo wa kuhoji mantiki ya serikali kuteka raia wakati watu wameshuhudia na report inasema alikuwa kwenye bodaboda na akavamiwa na wahuni waliokuwa kwenye harrier na mkubwa wa polisi akasema hawakumteka ila walimkamata.

Sisi tunaona walimteka na polisi wanaona walimkamata. Lakini ajabu uko wapi? wakati polisi wetu wanaweza kusema risasi iliyomuua Aquilina ilipigwa juu na ikapinda kona na kumpiga marehemu yaani waliyasema haya mchana kweupeee. Labda ile senema ya sisitivi na picha zile imesahaulika.

Kama mtu ni Mtanzania kweli na ukafa ukaenda mbinguni na ukamkuta polisi mmoja tu wa kibongo huko, aisee toka mbio sana utakuwa umekosea geti la kuingilia
 
Hivi inawezekana vipi atekwe halafu haohao watekaji wamruhusu mateka wao afanye mawasiliano na mke wake.
 
Au ndo wanapelekwa kwenye lile jumba alilosema rafiki yetu Britanicca. Utawala huu utekaji umekuwa kama kazi ya malipo na marupurupu ni kama vile kuna reward ukiteka unapewa zawadi nono...Teka upate fedha.

Utekaji huu unalichafua Taifa SANA tena katika utawala huu ...kinachoumiza ni tuliemkabidhi Nchi hajawahi kutoka hadharani akalikemia lakini nakumbuka kuna mwana CCM Mwanza aliuwawa na wananchi akaagiza mara moja wahusika kukamatwa ...Rais wetu jitokeze ukemee utekaji huo kama Kikwete alivyokuwa anakemea ujambazi kipindi chake ..
 
Hivi inawezekana vipi atekwe halafu haohao watekaji wamruhusu mateka wao afanye mawasiliano na mke wake.
Kama upo kwenye gari yako binafsi na umeona NISSAN NYEUPE ...zinaweka roadblock ...na unajua real situation kwamba hawa ni wale unkown person lazima tu wanataka kufanya kidnapping ... muda huo unajua uliwahi kufuatiliwa huko nyuma kwa nini usifanye mawasiliano na mtu wako wa karibu...kwa kuhofia usalama wako..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…