Dar: Polisi wakamata watu 32 kwa wizi wa Bil 2.082, ndani ya benki ya NMB

Dar: Polisi wakamata watu 32 kwa wizi wa Bil 2.082, ndani ya benki ya NMB

Hali mbaya posho hawapewi vyeo hawapandishwi mshahara wanacheleweshewa wataacha kuiba?subirini awamu ya pili muone hadi mabom nayo yataanza kuibiwa kabisa
 
Wezi gani wapumbavu hivi?
Yani walishindwa hata kwenda Malawi.
Unaiba 2bil unaenda Mbeya?
Pumbavu.
[/QUO
Huo ndiyo ulikuwa uwezo wao wa kufikiri, kwa hiyo tusiwalaumu. Mtu hajawishika hata milioni 2 lazima apate kiwewe cha kushika fedha nyingi kama hizo.
 
Hawa wezi wasipewe adhabu kali kwa kuwa wameiba bali wapewe adhabu kali kwa kuiba kwa uzembe! Wapigwe kipigo cha mbwa koko
 
Hawakutumia akili kujificha. Wanakimbilia kununua mali bila kujipanga namna ya kuzima swala.
 
Watu tunashida na pesa wao wanafanya mchezo mchezo kwani wanapitiaga wapi? Ngoja wakalime huko mpaka wakome wajinga sana hao watu
 
Kuna usemi unasema "hatua zote tisa"

Umeamua kutenda kitu hiyo ni hatua ya kwanza, kwanini usimalizie tisa?

Ushaamua kuiba kiasi kama hicho, unachotakiwa umalizie hatua za kukata mawasiliano na ndugu, kupotea nchini, kuacha ujinga, kuacha kuwaza nini kitatokea usipowaona ndugu zako...

Sasa umefanya hatua ya kwanza, zinazofuata ni kununua power tiller, sanlg na flat screen ya Sunda? Upo sawa kweli?
[emoji23][emoji23] umasikini kitu kibaya sana
 
Security Company za Bongo ni aibu tupu, pesa inatunzwa kwenye trunker kama ya wanafunzi ?? Bora hawa Gardaworld Wazungu wamekuja wawasaidie hawa wahi ndi bahili kwenye security.
 
Aisee hizi kampuni za ulinzi now zinapoteza Credibility kabisa
Unalimpa mtu 200,000 mshahara alafu huyo Huyo unambebesha fedha mabilion asafirishe, kama mtu una tamaa utaingia kingi

Ova
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA WATU 32 KWA TUHUMA ZA MABILIONI YA BENKI YA NMB JIJINI DSM.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu 32 kwa tuhuma za wizi wa fedha kiasi cha Tsh Tsh Bil 2.082.00

Mnamo tarehe 08/06/2020 majira ya saa tisa mchana huko katika Benki ya NMB tawi la Mbezi

Beach wafanyakazi watano wa kampuni ya ulinzi ya SECURITY GROUP OF AFRICA @ SGASecurity Tanzania Limited wakiwa na gari namba T 853 DPX MITSUBISH CANTER walikabidhiwa kiasi cha fedha Tsh Tsh 2 /= kwa maelekezo ya kuzisafirisha kutoka NMB tawi la Mbezi Beach ili wazipeleke tawi la NMB Benki House - CASH CENTRE iliyopo maeneo ya Posta Mpya.

Mara baada ya kukabidhiwa fedha hizo wafanyakazi hao badala ya kuzipeleka walipoelekezwa, walitoweka na fedha hizo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM siku hiyo ya tarehe 08/06/2020 majira ya saa 12 jioni lilibaini kutelekezwa kwa gari hilo maeneo ya Mbagala rangi tatu jirani na Shule ya SAINT MARY.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum kupitia kikosi kazi chake cha kupambana na ujambazi lilianza ufuatiliaji mara moja ikiwa ni pamoja na kufika eneo lilipoonekana gari hilo na kubaini kuwa wafanyakazi hao watano wamekula njama na kuiba kiasi cha fedha Tsh kutoka kwenye sanduku moja la chuma kati ya masanduku manne waliyokabidhiwa.

Aidha, masanduku matatu yaliyokutwa katika gari hilo yalifunguliwa na kukutwa na kiasi cha fedha Tsh 1,302,000,000 /= pia katika gari hilo zilikutwa silaha mbili aina ya Short gun Pump Action yenye risasi 12 na Short gun Protector yenye risasi 05, pamoja na sare za kampuni hiyo.

Watuhumiwa hao walikamatwa Mkoa wa Mbeya na Kigoma wakiwa wamenunua vitu vifuatavyo:-

(i).Trckta Power Tiller aina ya TRA-Change Model 7C/15 lenye thamani ya Tsh 20,000,000/=

(ii),Pikipiki moja aina ya SANLG

(iii).TV flat screen moja aina SUNDA na vitu mbalimbali vya matumizi ya ndani kama kitanda, godoro,jiko la gesi,rnakochi n.k

Mpaka sasa katika shauri hili Jumla ya Tsh 1,497,680,000/= zimeokolewa, mbali na thamani ya vitu vilixyonunuliwa kutoka sehemu ya fedha zilizoibiwa.

Jumla ya "'atillnuniwa 32 wamekamatwa na kuendelea kuhojiwa juu ya ushiriki wao kuhusiana na tukio hili

Aidha Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali ili kuwakamata watuhumiwa wote waliohusika na tukio hili.

ONYO KUHUSU MAANDAMANO YANAYOHAMASISHWA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es salaam linatoa onyo kali kwa kikundi au mtu yeyote atakayeshiriki maandamano hayo batili tarehe 07/07/2020 kwa madai ya kudai Tume huru ya uchaguzi waaache mara moja vinginevyo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

LAZARO B. MAMBOSASA- SACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

06/07/2020
View attachment 1498964View attachment 1498965
View attachment 1498948View attachment 1498950View attachment 1498951
Labda kumbukumbu zangu haziko sawa... Ni lini kumekuwa na maandamo halali yanayo mwambia ukweli YESU!!!
 
Back
Top Bottom